NA JOYCE KASIKI,GEITA
KATIBU Mkuu,Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo wa Zanzibar
Fatma Hamad Rajab amewaasa Wanawake wachimbaji kusambaza elimu ya
uchimbaji kwa vijana hususan wa kike ili waweze kujitegemea na kumudu mahitaji
katika familia.
Rajab ameyasema hayo alipotembeea katika banda la Chama cha Wachimbaji
Madini Wanawake (TAWOMA) katika maonesho ya Madini yanayoendeea katika
viwanja vya Bombambii katika mji wa Geita mkoani Geita.
“Changamoto mnazokutana nazo katika shughuli zenu mnapaswa
mzichukulie kama fursa ,lakini pia muendelee kutoa taaluma hasa kwa
vijana wa kike kwa sababu wao ndiyo wahitaji zaidi ili mwisho wa siku waweze
kupambana wenyewe kuhudumia familia badala ya kuwategemea wanaume,
“Mjitahidi kuonyesha ujasiri, kupambana na kuonyesha wanawake tunaweza
bila kumtegemea mwanaume,tufuate mfano mzuri wa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu
Hassan ambaye anaonyesha kwa vitendo kwamba wanawake tunaweza ,na
atakayebisha hilo huyo atakuwa ana chuki zake binafsi.”amesisitiza Rajab
Awali Katibu wa TAWOMA Salma Ernest ameelezea mafanikio ya chama hicho
katia kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia huku akisema,chama kimeweza
kufanya programu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kupitia sekta ya Madini.
Amesema,chama hicho kina wanachama mikoa 21 ya Tanzania na wanatarajia
kuongeza mikoa mingine lakini pia wapo katika wilaya 41 na wana matawi au
programu ya vijana ambao mpaka sasa wana vikundi 14 vya vijana ambao
wamejiajiri kwa kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia madini yenye ubora wa
chini ambayo hayana soko.
Aidha amesema,chama hicho kinaendesha vikundi 34 vya
kusaidia jamii ambapo 17 vipo Tanga na 12 kutoka Morogoro vijijini
ambavyo hukopeshana na hivyo kumudu kusaidia familia .
Katika hatua nyingine amesema chama hicho kinatimiza miaka 25 ya chama
chao na wamekuja na programu iitwayo Malkia wa Madini ambapo wameandaa programu
migodini pamoja na afya ya mama na mtotom,utunzaji umbuumbu ,eimu ya
miopo,vifaa na tenoojia ambapo pia wameungana na maundi maaum waemavu
ambao wapo nao wenye programu hiyo.
Amesema,Sherehe hizo zitafanyika Septemba 29 mwaka huu ambapo
watakuwa na matembezi ya Hisani kutoka ukumbi wa Halmashauri mpaka kwenye
viwanja vya maonesho huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Maendeeo ya
Jamii,Jinsia na Maundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima huku uzinduzi wa proramu hiyo
ukipangwa kutafanyia Otoba 30 .
Katika sherehe hizo mgeni rasmi atazindua na kumvisha taji
malkia wa Madini Tanzania 2023.
No comments:
Post a Comment