Na Joyce Kasiki,Geita
NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania BoT kwa kununua dhahabu kwa ajili ya kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha huku akisema ni ndoto ambayo Serikali ilikuwa inaitamani kwa muda mrefu.
Aidha ametoa wito kwa BOT kushirikiana kwa karibu na Wizara ya madini pamoja na taasisi zake ili waweze kumfikia kila mchimbaji kwa sababu kuna watu ambao hao wanaleta pesa wanakusanyiwa wanapelekewa dhahabu .
Akizungumza mkoani Geita katika maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita alipotembelea katika Banda hilo amesema kuwa kwa sasa nchi inahitaji fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi ambapo kwa upande wa dolla imekuwa changamoto kwa kila nchi duniani hivyo lazima zitumike rasimali za nchi katika kupata dolla na hawawezi kuipata bila kutumia dhahabu.
"Nia
yetu ni kuona kwamba eneo linalotupatia fedha za kigeni kwa wingi bado
itabaki kuwa sekta ya madini na sekta ya madini ikileta dolla
kwa wingi hizo stress nyingine mnazoziona kama mafuta madawa na bidhaa zote
tunazo ziagiza kutoka nje kwakutumia dolla tutaweza kuzipata ili
tuhudumie watanzania kwa hiyo hongereni sana kwa hatua hiyo"amesema Biteko
ma kuongeza kuwa
"Ni imani yangu baada ya miaka kadhaa na sisi kama nchi tuseme tuna akiba ya dhahabu tani kadhaaa kama ilivyo nchi nyingine kubwa na kuwapongeza wafanyazi wa BOT kwa hatua waliochukua ya ununuzi wa dhahabu."
Kwa
upande wake Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Masoko ya Fedha BOT,Dkt Anna Lyimo
amesema kuwa mbali kununua dhahabu bado wanaangalia namna ya kuwasaidia
wachimbaji wadogo na wa kati kutokana na changamoto zinazowakabili .
Ametaja baadhi ya changamoto hizo ni mitaji ,elimu na teknolojia huku akisema wameamua kushirikiana na STAMICO ambao itasimamia wachimbaji hao kuungana kupitia vikundi ambapo BOT itawezesha kupata mikopo na kuondokana uchimbaji mdogo na kuinuka zaidi katika uchumi wao binafsi na hivyo kuchangia katika uchumi wa Nchi.
Aidha amesema katika maonesho hayo ya madini BoT wanatoa elimu kuhusu sheria ya fedha za kigeni ya mwaka 2022 ambapo inataka matumizi na mapato yote yanayopatikana katika mauzo ya nje ya nchi basi yaweze kurudishwa nchini ndani ya siku tisini huku akisema mapato hayo na hivyo kuongeza akiba za fedha za kigeni.
Ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini yanuongozi thabiti wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana bega kwa bega na BoT na hivyo kutekeleza majukumu yake
No comments:
Post a Comment