CPB yawahakikishia wakulima soko la mazao yao

 

AFISA masoko na usambazaji  kutoka Bodi  ya Nafaka  na Mazao  mchanganyiko (CPB) Francisco Amos

 


 

BIDHAA mbalimbali katika soko la CP

 

                                      Na Joyce Kasiki,Geita

AFISA masoko na usambazaji  kutoka Bodi  ya Nafaka  na Mazao  mchanganyiko (CPB) Francisco Amos amesema kuwa bodi  imejipanga kumuondolea mkulima changamoto ya soko ya mazao yao iliyokuwa inamkabili mkulima huko nyuma

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA  Bobambili mkoani Geita,Amos  amesema kuwa Serikali ilianzisha bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ili iwe jukwaa la wakulima kuuza mazao yao pindi wanapopata changamoto katika masoko au mavuno yao.

"Naweza kusema kwamba tumeshiriki  maonyeaho haya tukiwa na lengo la kuonyesha bidhaa bora zinazozalishwa na bodi hiyo kupitia viwanda vyake mbalimbali hapa  nchini pamoja na kuwafahamisha fursa mbalimbali ambazo bodi ya nafaka wanazitoa kwa wakazi wa Geita  ikiwemo kuuza mazao yao katika bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko  huduma za uwakala   usambazaji na vilevile tunatoa  ushauri wa kitalaamu wa maswala ya kilimo na mambo mengine kama hayo "Amesema Amos

Nakuongeza kuwa "Tunawaomba wakulima mkoani Geita na wale wote wanaofika katika maonyesho kutembelea  banda letu ili  kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya kilimo hususani katika suala zima lakuongeza thamani ya mazao ambapo kimsingi  ndio jukumu mama la bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko."Amesisitiza  Amos

Pia ameongeza kuwa wao pamoja na wadau wengine wa sekta binafsi wananunua mazao katika bei shindani ambapo amewasisitiza wakulima kuendelea kulima kutokana na soko la mazao lipo na wao kama CPB wapo tayari kununua.

 Ametoa msisitizo kwa wakazi wa Kanda ya ziwa kuendelea kulima zao la mpunga wakutosha nakwamba Bodi ya nafaka  ipo tayari kununua kwa bei shindani hivyo muhimu kutembelea banda hilo kujua namna gani mazao yao yanaweza kupata vigezo vya kununuliwa na bodi hiyo kutokana na kuwa na viwango vyao vya ubora.

Hata hivyo amewataka wakulima nchini  kuwa na  utaratibu wakukutana na wataalamu wa ubora  ambapo watawapa ushauri kwa ni namna gani walime kuanzia shambani kuvuna ili mazao yao yanapoingia sokoni yawe na ubora unaotakiwa yaweze kuwa shindani katika soko.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.