Na Joyce Kasiki,Geita
KAMPUNI ya FEMA Mining and Drilling LTD inayojihusisha na uchimbaji,uchongaji na ulipuaji wa madini nchini iliyopo Munekeze-Katoro Mkoani Geita wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kwa kuwapa fursa kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi iliyopo nchini.
Hayo
yamesemwa na Mratibu mradi kutoka Kampuni hiyo Mhandisi Jacquline Mtei waati
akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya sita ya kimataifa ya
Teknolojia ya Madini yanayofanyika
katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.
Amesema, kwa sasa milango ya kufanya kazi wazawa na kupewa kazi mbalimbali hasa kwenye sekta ya madini ni dhahiri kuwa sekta hiyo inazidi kukua siku hadi siku.
" Napenda kumshukuru Rais Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuweza
kutengeneza Mazingira ya uwezekano wa wazawa 'makampuni mama' kuweza kufanya
kazi katika migodi yetu hii ya kati pamoja na Migodi mikubwa,Kupitia kampuni yetu ya FEMA sisi ni kampuni zawa kampuni ya
kitanzania kwa hiyo tumeona mama
alivyotengeneza mazingira ambayo imetuwezesha kapata zabuni katika migodi ya
kati na mikubwa" Amesema Jacquline
Amesema Sekta ya madini inaoongoza kwakuchangia uchumi wa nchi hivyo inapotokea milango inapofunguliwa kwa wazawa kufanya kazi katika migodi hii pia itasaidia kukua zaidi kwani watatanguliza uzalendo katika nchi yao.
Aidha
amewaaalika wanawake kusoma masomo ya sayansi hasa kuhusu miamba na madini kuwa
wasiogope kazi zipo pia waondoe dhana potofu kuwa kazi zinazohusu madini ni
wanaume pekee.
"Fursa za ajira kwa wanawake katika sekta ya madini zipo sisi kampuni yetu imeweza kutusaidia sisi wanawake kupata ajira zaidi ya wanawake kumi na tano wamepata ajira nikiwemo mimi kwa hiyo wanawake wenzangu msiogope tuje huku"amewahasisha Jacquline
Kwa upande wake Afisa manunuzi na usambazaji kutoka FEMA Mining and Drilling LTD Frank Joseph amesema hao kama FEMA wameweza kushirikiana na makampuni tano tofauti katika kuwapa zabuni katika kampuni yao kama vile usambazaji wa vipuri,mafuta na virainisha kwa ajili ya mashine zao pia pamoja na huduma zingine ikiwemo usafi,chakula na huduma nyingine za kijamii.
Aidha ameongeza pia katika katika kurudisha shukrani kwa jamiii kwa kile wanachokipata pia wameweza kusaidia kununua madawa katika zahati zinazo zunguka mgodi sanjari na kujenga shule na kukarabati vyumba vya madarasa ikiwemo kuzalisha ajira kwa vijana zaidi ya miamoja wanaozunguka mgodi.
No comments:
Post a Comment