MBUNGE wa Geita Mjini Costantine Kanyasu |
Na Joyce Kasiki,Geita
MBUNGE wa Geita Mjini Costantine Kanyasu ameiasa kamati ya Maandalizi ya maonesho ya Madini mkoani Geita kuangalia namna ya kuwafikia wachimbaji wadogo wa kuhakikisha wanakuwa na teknolojia za kisasa zitakazorahisisha kazi yao ya uchimbaji kwa ujumka.
Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kutembelea mabanda katika maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita 2023.
“Naipongeza sana kamati ya maandalizi wa kuandaa maonesho haya ambayo yamekuwa na tija kwa wachimbaji lakini hata hivyo bado walengwa ( wachimbaji wenyewe ) bado hawajafikiwa kiasi cha kutosha.”ameongeza
" Ziko Kampuni ambazo lazima wawafuate wachimbaji wadogo kule chini, kwa sababu maonesho haya siyo kwa ajii ya Makampuni makubwa ya uchimbaji kama GGM, Bakrifu, au Sota Mining na wengine ,bali yanalenga wachimbaji wadogo kwa hiyo tuangalie namna ya kuwafuata wale wachimbaji wadogo kule chini hasa kwenye kuwapelekea Teknolojia, mitaji, kuwawekea bima, Kwa sababu mabosi ndio wamekuja hapa, lakini wale wachimbaji wenyewe wako kwenye mashimo, ambao hata hawajapata nafasi ya kuja kuona Maonyesho haya, na ndio wanaokufa Kwa kuangukiwa na miamba" amesema Kanyasu
Aidha amesema ipo haja ya kutafuta teknolojia ya kuokoa misitu kutokana na kukatwa miti kwa ajii ya shughuli za uchimbaji huku akisema Geita ya sasa siyo ya zamani kwani miti mingi imekatwa .
“Inavyoonekana Geita ya leo siyo ile Geita ya zamani, kuanzia Kasama mpaka Geita mjini ,palikuwa na msitu Mkubwa sana, lakini miti yote imekwisha kwa sababu ya Uchimbaji wa madini ( Matumizi ya Matimba) lazima tutafute Teknolojia itakayookoa Misitu itakayobaki ili tusiendelee kukata miti yote na uharibu hali ya hewa.”amesema na uongeza kuwa
"Kuna uhusiano mkubwa wa hali ya hewa ya Kanda ya ziwa na Misitu ya asili iliyokuwepo, kwa hiyo tuchimbe Madini tutengeneze pesa, zile pesa zirudi kupanda miti, kazi nzuri imefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii pale mbele ya Katolo ule msitu wa Bihalamulo wamepanda hekta 69,000 pale wamepanda msitu mkubwa, ifanyike hivyo kwenye maeneo yote yaliyokua na msitu wa asili lakini imevunwa kwenda kwenye madini.”
Ametumia nafasi hiyo kuiomba Wizara ya madini kuhakikisha kwenye Maonyesho kama hayo mwakani,kuwe na Banda linaloonyesha bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kutokana na mawe ya madini ya aina mbalimbali kama mikufu, Mikanda, shanga, heleni, shanga, vitu vingi mbalimbali ambao waliletwa na Wizara ii wananchi wajifunze wa kusikia na kuona uhaisia wa vitu vinavyotengenezwa na madini yao.
Pia ameiomba Tume ya Madini kuwasaidia kuja na Teknolojia ya kuanza kukamata Silva, dhahabu, pamoja na madini mengine ili utajiri huo usitupwe kwenye matope na Madini mengine .
" Sasa hapa tuna Madini yanayotupwa, kule wanaofanya uchechuaji wanakamata zaidi Dhahabu na Silva, maana Silva nyingí inabaki kwenye tope, waje na Teknolojia ya kukamata silva inayobaki kwenye tope, kwasababu sokoni tunahitaji Silva lakini sio koo kwa mchimbaji, mchimbaji anatafutwa dhahabu kwa hiyo asilimia anayopatikana baada ya kuchenjuliwa ni ile ambayo imekamatwa Kwa bahati mbaya.
Kwa upande wake mfanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Tanzanite ya Franone Mining & Gems Company Ltd Furaha Mshai amesema ujio wao kwenye Maonyesho hayo ni fursa pekee ya kutangaza Madini aina ya Tanzanite ambayo wa dunia nzima yanapatiana nchini Tanzania tu hadi hivi sasa.
“Duniani kote madini haya yanapatikana nchini Tanzania tu ,kwa hiyo huu ni utajiri wetu ambao watanzania tunajivunia na hata hapa katika maonesho haya yamekuwa ni kivutio kikubwa kwa watu mbalimbali wanaotembeea banda letu.”
xxx
No comments:
Post a Comment