GAVANA wa Benki Kuu (BoT)
Emmanuel Tutuba amesema,moja ya majukumu ya Benki hiyo ni pamoja na kushiriki
katika masuala ya uchumi ambapo hununua dhahabu kwa ajili ya kutunza akiba za
nchi badala ya kutunza kama fedha.
Tutuba ameyasema hayo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la BoT kwenye maonyesho ya
Madini mkoani Geita kwenye viwanja vya EPZA kata ya Bombambili.
Amesema lengo la kununua
dhahabu kuziuza nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na hivyo kuwezesha
kusapoti uchumi wan chi.
“Kwa hiyo ushiriki wetu katika
masuala ya kiuchumi ni pamoja na kununua dhahabu ikiwa ni namna mbadala ya
kuendelea kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha taslimu lakini pia
tunanunua dhahabu ili tupate fedha za kigeni baada ya kuuza nje na fedha ziweze
kusapoti uchumi wa nchi.”amesema Tutuba
Akizungumzia kuhusu kuadimika
kwa dola Tutuba amesema,changamoto hiyo ni kutokana na kuadimika kwa dola
kwenye mzungu wa uchumi kidunia .
Hata hivyo amesema,pamoja na
changamoto hiyo BoT bado ina dola za kutosha kugharamia shughuli za kiserikali
pamoja na shughuli za kipaumbele kwa wakati huo.
“Hii ni kutokana na ‘reserves’
ya Dola ilitunzwa na BoT,lakini sasa watu wengine wanachanganya, wakisikia
reserves za nchi wanadhani ni fedha ambayo ya kuwagawia watu ,lakini kimsingi
hizi reserves ndio zinasaidia nchi katika kipindi kama hiki ambacho dola
imeadimika.”amesisitiza Tutuba na kuongeza kuwa
“Kwa hapa tunaendelea na
utekelezaji wa miradi mikubwa serikali kwa kuwa tunayo fedha ya kutosha kutekeleza
miradi malimbali kwa mwaka mzima..,lakini hata pakitokea hatari na mipaka
ikifungwa zile fedha tunaweza kuzitumia kwa mwaka mzima.”
Gavana Tutuba ametumia nafasi
hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa Filamu yake ya Royal Tour ambayo
imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza Dola kutokana na watalii wengi kuja
kutalii hapa nchini.
“Kwa hiyo katika mzunguko
kitakwimu dola inaendelea kuongezeka na hivyo kuondoa kikwazo cha kuzuia
uchumi uendelee.”
Akizungumza kuhusu uwepo wao
katika maonesho hayo amesema,wameshiriki kikamilifu kwa lengo la kutoa
elimu kwa wadau wanaohitaji kujua namna BoT inavyoshiriki kwenye sekta ya
madini.
Aidha amesema ,BoT ina dhamana
ya kusimamia masuala ya ukuaji wa uchumi na uhimilivu wa bei pamoja na
mzunguko na thamani ya fedha .
“Sisi tumefika katika maonesho
haya ikiwa ni mojawapo ya mikakati yetu ya kutoa elimu kwa wadau wa madini na
wananchi kwa ujumla kuhusu BoT na kushiriki katika masuala ya ukuaji wa
uchumi.”amesisitiza Gavana huyo
No comments:
Post a Comment