BRELA yajipambanua ilivyoboresha utendaji wao wa kazi

 

 
 
 
 
 

 

                            Na Joyce Kasiki,Geita

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameziagiza Mamlaka zote zinazosimamia masuala ya leseni uhakikisha hakuna vikwazo katika usajili wa biashara kwa lengo la kuvutia wawekezaji hapa nchini.

Naibu Waziri Kigahe ameyasema hayo katika semina ya wadau wa madini kwenye maonesho ya madini yanayoendelea katika mji wa Geita.

Amesema,kuondoa vikwazo katika usajili wa biashara ni nyenzo muhimu katika kuvutia wawekezaji ambao husababisha upatikanaji wa maendeleo wa haraka.

Naye Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)  Jubilate Muro amesema,kufuata sheria ,kanuni na taratibu zilizopo hapa nchini ni muhimu wa wafanyabiashara ili waweze kufanya biashara zao kwa uhuru.

Amesema hatua hiyo inamwezesha mfanyabiashara kutambulika na benki mbalimbali na kuweza kupata sapoti ya biashara zao.

Kwa mujibu wa Muro , mfanyabiashara ni lazima afuate hatua stahiki katika mfumo wa usajili kwa kutimiza vigezo muhimu vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kuwa na kitambulisho cha Utaifa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vyaTaifa (NIDA).

“Hata kama ni mbia kutoka kwenye kampuni au Mkurugenzi wa kampuni, lazima uwe na kitambulisho cha NIDA na namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN ya nchi husika,hapa utaweza kufanya biashara kwa uhuru kabisa.”amesisitiza Muro

 Naye Mkuu wa Idara ya Miliki BRELA Loy Mhando amesema,katika uhakikisha huduma ya usajili inafanyika kwa haraka,hivi sasa huduma hizo hutolewa kwa njia ya mtandao.

“Hivi sasa tumerahisisha huduma zetu ambapo mfanyabiashara sasa anajisajili mwenyewe kwa njia ya mtandao mahali alipo na siyo mpaka aende kwenye ofisi za BRELA.”amesema Mhando

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.