Na Joyce kasiki,Geita
WAZIRI wa Madini Antony Mavunde ametoa rai kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya uwepo wa sheria ya wawekezaji wazawa (Local Content) ili waweze kuongeza tija katika shughuli zao na hivyo kuchangia katika pato la Taifa.
Akizungumza katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani humo alipomtembelea mmoja kati ya wawekezaji wazawa katika mkoa huo Athanas Inyasi ,Mavunde amesema uwepo wa sheria hiyo umewanufaisha na unaendelea kuwanufaisha wawekezaji walioamua kuwekeza hapa nchini.
Mavunde ameonesha kufurahishwa na kuridhishwa na uwekekzaji unaofanywa na Mwekezaji huyo na kutumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi wengine kujikita katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali hapa nchini..
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan itaendelea kusimamia sheria hii ili kuhakikisha watanzania wanaendelea kunufaika na rasilimali zao zikiwemo za kwee sekta ya madini.”amesema Mavunde
“Nitoe rai kwa watanzania kuendelea kufanya uwekezaji,Serikali ya awamu ya sita imeboresha mazingira ili wats wengi zaidi wakiwemo wazawa wanafanya uwekezaji ,kwa hiyo tunahitaji kuwaona akina mzee Inyasi wengi zaidi na mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini katika maisha ya watanzania .”amesisitiza Mavunde
Naye Mwenyekiti wa Makampuni ya Blue Coast Athanas Inyasi amesema sheria ya local Contect imesaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuleta mafanikio makubwa kwa watanzania,huku ajira 360 zikiwa zimetolewa na kampuni hiyo.
Ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya uwekezaji huku akiahidi kuendelea kufanya uwekezaji wenye tija kwa maslahi ya jamais na Taifa kwa ujumla.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Coast Ndahilo Athanas amesema kampuni hiyo pamoja na mambo mengine Pia imekuwa ikichangia katika shughuli za Maendeleo ambapo mpaka sasa wameshajenga miundombinu ya madarasa na kununua madawati kwa shule za msingi Nyamalembo na Mseto zilizopo katika mkoa wa Geita.
Aidha amesema kampuni imekuwa ikilipa kodi kwa weledi na hivyo kupata tuzo ya mlipaji bora wa kodi na hatimaye kuwekwa kwenye kundi la walipa kodi wakubwa.
No comments:
Post a Comment