Na Joyce Kasiki,Dodoma
WAZIRI wa Madini Anthony mavunde wamewaonya wadau wa madini kutojihusisha na utoroshaji wa madini nchini huku akisema kuwa, atakayebainika atachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni katika maeneo yote ambayo muhusika anafanya shughuli zake za madini hapa nchini.
Mavunde ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa chama cha Mabroka katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma huku akisema wadau hao wanapaswa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha seta ya madini inawanufaisha watanzania na Taifa kwa ujumla.
“Nataka niwahahakikishie kwamba najua michezo hii inafanyika sana katika mkoa wa Morogoro na ninafahamu, mliniona juzi Kahama nilifika usiku kwenye utoroshaji ,na niwape salamu tu,hao ambao wanakiuka utaratibu watanikuta huko ,na Mimi staili yangu ni moja tu maana Sheria inasema vizuri na mimi nipo hapa kwa mujibu Sheria, unakiuka masharti ya leseni naupa ‘suspension’ sijiulizi mara mbili nasimamisha leseni,kwa hiyo Katibu Mkuu naamini hilo tutalisimamia vizuri.”
Ameomba ushirikiano kutoka kwa wadau hao kuhakikisha wanashirikiana na Serikali Ili kukuza sekta ya Madini hapa nchini Ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali la kutaka sekta hiyo ikusanye kiasi Cha shilingi Trilioni Moja .
“Hili linahitaji ushirikiano na uadilifu katika sekta hii,tushirikiane kuhakikisha rasilimali hii inatufaisha,ninyi ndio wadau wakubwa mtakaotusaidia katika hili la utoroshaji maana nyie ndio mnaowapelekea madini ,kwa hiyo mnawafahamu,msinikwaze kwa kushirikiana na ‘dealers’ kutorosha madini na nikimkamata mmoja nafuatilia mnyororo mzima simuachi hata mmoja,
“Hivi tunavyozungumza kuna watu nimewashikilia Chunya na Geita na mtawaona mahakamani muda si mrefu ,baada ya maamuzi ya mahakama na ikatoa maamuzi ya kwamba umethibitika nafuta leseni na ninaku-‘black list’ hufanyi tena biashara ya madini.amesema Mavunde na kuongeza kuwa
“Juzi nimekwenda Kahama nimekuta mzigo wa kilo 4.3 wenye thamani ya shilingi milioni 562 nimesimamisha leseni ya muhusika,na sasa hivi nikikuta unatorosha madini kwanza nasimamisha leseni zako nchi nzima wakati tunasubiri uamuzi wa mahakama,nawaomba kama hii ndio biashara yako fuata Sheria tukifanya hivyo tutaisaidia nchi yetu.”
Waziri Mavunde amewaasa wadau hao kutoa maoni yao ama unahitajika kufanyika marekebisho ama katika sera au sheria za madini Ili kuwawezesha kufanya biashara ya madini na kuisaidia serikali katika kukusanya mapato na siyo kutorosha madini.
“Nimesema milango ipo wazi njoo uniambie tatizo lipo wapi ili tuboreshe na kufanya marekebisho yatakayowawezesha kufanya biashara ya Madini bila udanganyifu.”
Awali Mwenyekiti wa CHAMMATA Jeremia Kituyo ameeleza changamoto zinazoikabili CHAMMATA ambapo amesema ni pamoja na leseni kukatwa kila mkoa,baadhi ya madini kama Tanzanite kuzuiwa kuuzwa katika mikoa mingine,Mabroka kukosa mikopo katika taasisi za kifedha ,wageni kusogelea maeneo yao ya uchimbaji hasa katika maeneo ya Maganzo,Mahenge na Mererani .
Aidha ametaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa zahanati ndani ya ukuta wa Mererani.
Ametumia nafasi hiyo kuishauri Serikali kurudisha soko laadini Mererani lakini pia kuangalia upya suala.la ukataji leseni na kwamba badala ya kukatwa kila.mkoa basi leseni zikaywe kwa Kanda.
Kwa mujibu wa Kituyo kitendo cha Tanzanite kuuzwa Mererani pekee yake kimedororesha biashara ya madini .
"Kwa.mfano soko la Arusha ni la kitaifa linapokea madini kutoka mikoa yote nchini,sasa kitendo Cha Tanzanite kuzuiwa kuuzwa mikoa mingine kimefifisha biashara."amesisitiza Kituyo
Ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuiachia Tanzanite iendee kuuzwa katika masoko huku wakiithibitishia Serikali liyalibda madini hayo.
xxxxxx