Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Latangaza Uongozi Mpya
DKT. Tulia aiagiza kamati ya IPU kushughulikia mgogoro wa israel na Parestina
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameielekeza Kamati inayoshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati ya Umoja huo kutembelea eneo hilo mapema katika juhudi za kutafuta suluhusho linaloweza kuhakikisha amani na usalama vinapatikana kufuatia mgogoro unaoendelea baina ya Israel na Parestina.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 30 Novemba, 2023 Jijini Tel Aviv nchini Israel mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili iliyompa fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Israel na Mamlaka ya Parestina.
"Nimekuja kutembelea maeneo ya Parestina na Israel ambao wote hawa mabunge yao ni Wanachama wa IPU lakini muhimu zaidi kuwafahamisha kuwa tupo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na Kamati yetu inayoshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati itakuwa hapa siku zijazo kutafuta uhalisia wa mgogoro huu na kuleta taarifa ambayo tutapata nafasi ya kuijadili ili tuone huko mbele tunakokwenda tunawezaje kuwa na amani na usalama kwa watu wote." Dkt. Tulia
Amefafanua kuwa, moja ya msingi wa IPU ni kuhakikisha uhai wa kila binadamu unalindwa na Umoja huo utafanya kila linalowezekana ili dunia iwe sehemu salama na ya amani kwa binadamu wote bila kujali rangi, itikadi, imani na maeneo wanayotoka.
Aidha amesisitiza kuwa, Mpango mkakati wa Umoja huo ni kuutumia Mwaka 2024 pamoja na mambo mengine kujadili kwa kina suala la Amani na Usalama kama ajenda muhimu kwenye Mikutano yake Mikuu ya mwezi Machi na Oktoba mwakani.
Katika ziara hiyo Dkt. Tulia na ujumbe wake amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Mamlaka ya Palestina Jijini Ramallah akiwemo Waziri Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhe. Muhammad Shtayyeh pamoja na Spika wa Baraza la Mamlaka ya Palestina Mhe. Rawhi Fattouh.
Vilevile Dkt. Tulia alipata fursa ya kutembelea Kijiji cha Kfar Aza Kibbutz kati ya vijiji vilivyoshambuliwa na wanamgambo wa Hamas Oktoba 7, 2023 na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Israel (Knesset) Mhe. Amir Ohana, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Vijiji Mhe. Avi Dicter na Wabunge Wawakilishi wa Knesset kwenye IPU walioongozwa na Mhe. Danny Daddon.
DKT. Yonazi-Viongozi wa dini tumieni majukwaa yenu kuhamasisha waumini na jamii katika mwitikio wa UKIMWI”
Na Mwandishi wetu -Morogoro
VIONGOZI wa dini nchini wamehimizwa kuwaelimisha na kuwajenga vijana katika maadili mema, kuwaepusha na maambukizi ya VVU na kudhihirisha jitihada za pamoja kati ya Taasisi za dini na Serikali katika kulinda na kuhamasisha vijana kutambua hali zao za maambukizi ya VVU na kupata elimu ya Afya ya Uzazi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi katika ufunguzi wa Mdahalo kati ya Vijana na Viongozi wa dini uliofanyika Novemba 29, 2023 mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazoendelea kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI itakayofanyika Desemba Mosi mwaka huu.
Dkt. Yonazi amesema kufanyika kwa mdahalo huo iwe chachu ya kuhamasisha na kutetea mitazamo chanya katika kupinga unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na kuwa na mkakati maalumu kuhakikisha kuwa Nyenzo na Miongozo iliyopo inatumika ipasavyo.
“Takwimu zinaonesha kuwa moja ya makundi yaliyo nyuma katika kufikia malengo yaliyowekwa ya Sifuri tatu ni kundi la VIJANA. Hii ni kwa kuwa pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kwenye afua za VVU na UKIMWI, vijana wengi wenye umri wa miaka 15-24 hawajui hali zao za maambukizi ukilinganisha na watu wenye umri mkubwa,”Amesema Dkt. Yonazi.
Pia ameongeza kwamba Katika kufikia lengo la sifuri ya maambukizo mapya kama nchi, maambukizi mapya yameendelea kushuka mwaka hadi mwaka, akisema hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa takribani watu 54,000 waliambukizwa VVU mwaka 2021 nchini ambapo ni sawa na takribani watu 4,500 kwa mwezi au watu 150 kwa siku.
“Vijana wenye umri wa miaka 15-24 ndio kundi ambalo linaonesha kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizo mapya, kwani katika watu wote wanaopata maambukizi mapya ya VVU kila mwaka, takribani asilimia 35 ni vijana wenye umri wa miaka 15-24 (yaani katika kila watu 10 wanaopata maambukizo mapya ya VVU watatu ni vijana wa umri huu na takribani asilimia 74 ni wasichana,”Amefafanua.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amebainisha baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya UKIMWI kwa vijana kuwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa Dini kuwazuia watu wanaoishi na VVU kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi kutokana na imani kwamba maombi pekee au uponyaji wa kimiujiza pekee ndivyo vinavyokubalika.
“Baadhi ya watu wanaoishi na VVU huacha matibabu kutokana na mafundisho na matamko ya baadhi ya viongozi wa Dini, Baadhi ya viongozi wa Dini kutotoa tahadhari ya kutosha kuhusu mahitaji maalum ya vijana wanaoishi na VVU na changamoto wanazokumbana nazo zinazohusiana na matibabu,” Ameeleza.
Vivile Dkt. Yonazi ametoa rai kwa viongozi wa Dini akiwataka kutumia majukwaa yao kutoa elimu ili kusaidia kuhamasiaha waumini na jamii ambao ni watoto, vijana na watu wazima katika mwitikio wa UKIMWI hatua itakayosaidia kuongeza uelewa katika jamii kuhusu ufuasi mzuri wa dawa na matibabu, kuhamasisha upimaji na kwa baadhi ya wazazi ambao hawawaweki wazi watoto wao ambao wapo kwenye matumizi ya dawa, na kusaidia katika mapambano dhidi ya unyanyapaa na ubauguzi na ukatili wa kijinsia.
“Hii itaiwezesha nchi yetu kufikia malengo ya TISINI NA TANO (95%) TATU ifikapo 2025 katika mapambano dhidi ya VVU na Asilimia 95 ya watu wanaoishi na VVU wawe wamejua hali zao za maambukizo; asilimia 95 ya waliopimwa VVU na kugundulika kuwa wana maambukizo watumie dawa za kufubaza VVU (ARV) na asilimia 95 ya watu wanaotumia dawa wawe wamefubaza VVU),”Amesema Dkt. Yonazi.
Ikumbukwe maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu Kitaifa yatafanyika mkoani Morogoro Desemba Mosi mwaka 2023 chini ya kauli mbiu isemayo “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI”
WALIMU WANAOFUNDISHA SOMO LA ENGLISH WATAKIWA KUSAMBAZA UJUZI WA SOMO HILO KWA WENGINE
Na Mwandishi Wetu,Pwani
Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Kassim Mchatta ametoa wito kwa Walimu wa msingi wa Somo la English kusambaza ujuzi wa somo hilo kwa wenzao hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inatarajia kutekeleza mtaala mpya ifikapo Januari 2024.
Mchatta ametoa wito huo Novemba 22 alipofungua mafunzo ya kusimamia na kutekeleza muhtasari wa Somo la English kwa Shule za Msingi kulingana na Mtaala mpya wa Elimu ya Msingi unaotarajiwa kuanza kutekelezwa Januari 2024.
Amesema, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania na OR-TAMISEMI chini ya ufadhili wa Shirika la la Maendeleo la Uingereza UK-International Development kupitia mradi wa "Shule Bora" imeandaa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) kuhusu Muhtasari wa Somo la English kulingana na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika mitaala mipya.
Aidha, Mchatta amesema, lengo la mafunzo haya ni kukuza uwezo wa walimu wa Somo la English wa Shule za Msingi kutekeleza Mtaala Mpya, kuimarisha umahiri wa washiriki katika kutumia mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa Somo la English ili kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wote.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Bi. Sara Mlaki amesema, kupitia mafunzo haya kwa Walimu wa Msingi wa Somo la English katika Wilaya ya Chalinze yataenda kuleta mabadiliko chanya katika ufundishaji na ujifunzaji na kuongeza ufaulu hasa katika somo hilo.
Pia, Bi Mlaki amesisitiza walimu kupeleka ujuzi walioupata kwa walimu wengine ili iwe chachu ya kuongeza ufaulu katika Wilaya ya Chalinze hasa katika Somo la English.
Naibu Waziri Nderiananga ahimiza kamati za maafa kuendelea kujipanga katika kukabiliana na maafa
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kujenga uwezo kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa Mkoa wa Lindi kuhusu hatua za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho. |
Viongozi watakiwa kutumia takwimu kutoka kwa watakwimu wao
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akisalimiana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa katika viunga vya Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma. |
BAADHI ya wadau wa Takwimu waliofika katika maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika jijini Dodoma |
Na Joyce Kasiki,Dodoma
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt.Albona Chuwa amewataka watakwimu katika sekta mbalimbali kufanya kazi ya ziada ya kuwapatia ViongozI wao takwimu sahihi zizlizopata kibalo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ili waweze kuzitumia katika kuleta maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla.
Dkt.Chuwa ametoa kauli hiyo leo Nov 21,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya 33 ya siku ya Takwimu Afrika .
“Watakwimu wa Halmashauri, Wizara, Idara naTaasisi za umma mnapaswa kufanya kazi ya ziada kwa kuwapatia viongozi wenu takwimu sahihi ambazo zimepata kibali kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu pale wanapowasilisha taarifa kwa wananchi au viongozi wa juu ili kuepuka upotoshaji wa takwimu.”amesema Chuwa
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ameelezea umuhimu wa Takwimu huku akisema ,Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotoa Takwimu bora na zinazoaminika ulimwenguni .
Senyamule ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Ofisi ya Takwimu hapa nchini (NBS) kusambaza taarifa za kitawimu kwenye Halmashauri hapa nchini kwani Takwimu zinatakiwa kutumiwa kwenye kutafsiri mipango ya maendeleo kwa sekta zote.
Aidha amesema Takwimu zinasaidia nchi za Afrika kufahamu idadi ya rasilimali watu iliyopo na makundi yake.
Kwa upande wae Kamisaa wa Sensa Zanzibar Balozi Mohamed Ally Hamza amesema maadhimisho hayo yamelenga kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu matumizi ya sensa pia ushirikishwaji wa jamii unasaidia kuongeza thamani ya Takwimu hapa nchini.
Wachambuzi mifumo ya TEHAMA watakiwa kuongeza elimu
Na Mwandishi Wetu
Wachambuzi wa mifumo ya TEHAMA ‘Business Analysts’ katika taasisi za umma, wametakiwa kuongeza elimu na kupata maarifa mapya mara kwa mara, ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa mabadiliko ya teknolojia mpya zinazoibuka, ikiwemo ujuzi katika uchambuzi wa takwimu pamoja na akili bandia.
Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja wa Ushauri na Uelekezi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bi.Joan Valentine, wakati akifungua mafunzo ya siku sita kwa Wachambuzi wa mifumo ya TEHAMA yanayofanyika katika ofisi za Kambarage Tower jijini Dodoma.
Aidha, Bi. Joan aliwataka Maafisa hao kujifunza stadi mbalimbali ikiwemo teknolojia ya akili bandia na uchambuzi wa takwimu, ili ziwasaidie kupambana na mabadiliko ya teknolojia yanayoibuka duniani mara kwa mara na kuhakikisha teknolojia hizo zinasaidia ukuaji wa taasisi zao.
“Kwa sasa dunia inazungumza kuhusu akili bandia, hivyo wachambuzi wa mifumo lazima muwe na ujuzi wa hizi teknolojia ili kuzisaidia taasisi zenu katika utendaji kazi wa kila siku”, alisema Bi.Joan.
Vilevile, aliwataka maafisa hao kuona umuhimu wa kujifunza stadi tepe ‘soft skills’ ili ziweze kuwasaidia katika kupambana na mabadiliko yanayoendelea kutokea katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ulimwengu kote.
“Kwa sasa TEHAMA inatoka kuwa fani saidizi ‘supporting tool’ hadi kuwa fani wezeshi ‘enabling tool’ hivyo, mnatakiwa muwe wajuzi zaidi katika sekta ya TEHAMA ili kuzisaidia taasisi zenu katika kupiga hatua katika utendaji kazi wa kila siku”, alisisitiza.
Mratibu wa Mafunzo hayo Bw.Ceaser Mwambani ambaye pia ni Mchambuzi wa Mifumo ya TEHAMA e-GA, alisema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa hao, katika maeneo ya Uchambuzi wa Mifumo ya TEHAMA, Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA, Miongozo, Viwango, Usimamizi, Ubora na Usalama wa Mifumo ya TEHAMA Serikalini.
“Kupitia mafunzo haya, tunaimani kuwa, washiriki wote hapa watakuwa na uelewa zaidi kuhusu uchambuzi wa mifumo na miradi ya TEHAMA Pamoja na kuweza kutoa mchango mzuri kwenye taasisi zao ili kuwa na miradi yenye tija kwa taifa”, alifafanua.
Mafunzo hayo yanayotarajiwa kukamilika Novemba 25, mwaka huu ikiwa ni muendelezo wa jitihada za e-GA za kuhakikisha inashirikiana na kuzijengea uwezo taasisi za umma katika kukuza Serikali Mtandao.
Shekimweri afungua Kongamano la maadhimisho ya sikubua Takkwmu Afrika
Na Joyce Kasiki, Dodoma
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amefungua Kongamano la maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika(AFCFTA)mchango wa Takwimu rasmi na'big data'katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya afrika.
Akifungua Kongamano hilo Mkuu huyo wa wilaya amesema,Ofisi za Taifa za Takwimu Barani Afrika hazina budi kuendelea kuzalisha takwimu rasmi ,zenye ubora na kuzisambaza kwa wakati Ili kuiwezesha Serikali kufanya maamuzi hasa katika eneo la kuleta maendeleo ya watu kwa wakati Barani Afrika
Kwa maananhiyo Ofisi za Taifa za Takwimu hazina budi kuboresha mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili Takwimu ziweze kuwafikia wadau kwa urahisi na na kwa kuzingatia matumizi ya njia rahisi za usambazaji wa Takwimu husika.
Kwa mujibu wa Shekimweri Ofisi za Taifa za Takwimu barani afrika zinawajibu mkubwa wa kusaidia Nchi kufanya maamuzi yanayohusu sera kuhusiana na eneo huru la biashara afrika.
" Takwimu zinakuwa na maana pale ambapo zinatolewa taarifa kwani zinakwenda kukidhi mahitaji kwa usahihi na idadi husika ya watu."
Akizungumza katika Kongamano hilo Kaimu Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu NBS Emilian Karugendo
amesema kuwa matumizi ya Takwimu rasmi ndio msingi wa kila kitu katika maisha,katika mipango na katika kufuatilia programu mbalimbali na utekelezaji wake.
Karugendo ametaja mada za Kongamano hilo kuwa ni pamoja na uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa eneo huru la biashara la Afrika(AFCFTA),mchango wa Takwimu rasmi na'big data' katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika.
Ametaja mada nyingine ni matokeo ya sensa ya watu na makazi mwaka 2022 na mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanawezaje kutumika kwa pamoja na matokeo ya tafiti nyingine ili kuongeza matumizi na thamani ya Takwimu rasmi katika sekta ya kilimo nchini.
Naye Mhadhiri chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Godfrey Saga amesema lengo kubwa la kongamano hilo ni kuweka ufahamu katika tasnia ya Takwimu kuanzia shughuli za ufundishaji masuala ya utafiti na masuala ya ushauri wa kitaalamu pamoja na kutumia taarifa hizo zinazotokana na takwimu mbalimbali.