UWT yalaani Mwenezi BAWACHA kushambuliwa


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,Dodoma
UMOJA  wa Wanawake wa  Chama cha Mapinduzi Taifa (UWT), umelaani shambulio la kudhuru mwili alilofanyiwa Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Sigilaga Mligo, ambalo limesababisha maumivu makali hadi kupelekea kulazwa hospitalini huku akishangazwa na uongozi wa CHADEMA Taifa kukalia kimya suala hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa UWT  Taifa Mary Chatanda amesema  kuwa shambulio hilo ni aina ya unyanyasaji, ukandamizaji, na uonevu dhidi ya mwanamke lakini pia na mfumo dume uliopo katika chama cha CHADEMA

Amesema kitendo hicho kinakwenda kinyuma na madhumuni ya UWT, kama inavyoelezwa katika kifungu (f) cha katiba yake, kinachotamka kuwa Umoja huo ni chombo cha ukombozi wa wanawake wa Tanzania dhidi ya unyanyasaji, unyonyaji, ukandamizaji, na mila zote zinazorudisha nyuma maendeleo ya wanawake.

UWT imeeleza masikitiko yake kuhusu mazingira ya tukio hilo, ambapo inadaiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, alikuwepo lakini hakuchukua hatua yoyote.

Umoja huo umehoji ukimya wa viongozi wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) kuhusu shambulio hilo, hasa kwa kuwa mhanga ni kiongozi wa ngazi ya juu katika baraza hilo.

Kadhalika, UWT imeitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufuatilia kwa karibu uanzishwaji wa madawati ya jinsia ndani ya vyama vya siasa, kama inavyotakiwa na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2023. Umoja huo unataka madawati hayo yawe na mamlaka na uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, na ukandamizaji wa kijinsia katika siasa.

Katika hatua nyingine, UWT imewataka wanawake kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi pindi muda utakapofika, ikisisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wa kikatiba na unapaswa kuwa huru na wa haki.

UWT imetoa pole kwa Bi. Sigilaga Mligo na kumtakia uponyaji wa haraka, huku ikihimiza hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika katika shambulio hilo.
Share:

SOS Children's Village yakabidhi Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji, Uendeshaji na Usimamizi wa makao ya watoto


Published from Blogger Prime Android App



Na WMJJWM- Dodoma 

KATIBU  Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amepokea ugeni kutoka  Shirika la Watoto la SOS Children's Village  ambapo ugeni huo ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo  Aisha Salim Ali leo Machi 27, 2025 katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Dkt Jingu amelipongeza Shirika hilo kwa jitihada zake za kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha  wanadhibiti changamoto ya watoto kuishi na kufanya kazi mitaani baada ya Shirika hilo kukabidhi Mwongozo wa Taifa wa Uanzishaji, Uendeshaji na Usimamizi wa makao ya watoto nchini.

Aidha Dkt. Jingu ametoa wito kwa jamii kuimarisha taasisi ya familia na kuepuka migogoro kwani tafiti zinaonesha hivi karibuni kumekua na kuvunjika kwa ndoa nyingi  na  kupelekea kupatikana kwa wimbi la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SOS Children's Village   Aisha Salim Ali ameahidi ushirikiano kati ya Shirika lake na Wizara katika kuhudumia Watoto katika Makao ya Watoto kwa kuweka namna nzuri ya Utoaji wa huduma na Malezi katika Makao hayo.

Mwisho.
Share:

RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA



Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


 
Na WMJJWM- Dodoma 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewafuturisha Watoto wanaolelewa katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo Dodoma katika Kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 
Akizungumza wakati wa Iftari hiyo kwa niaba yake, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis alitoa shukurani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi yenye lengo la kuondoa kabisa changamoto zinazowakabili watoto walio katika mazingira hatarishi. 

“Kipekee kabisa, ninamshukuru tena Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kufuturisha watoto wanaoishi katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo pamoja na maeneo mengine ya nchi hususani Watoto wa Mkoa wa Arusha na Dar Es Salaam”. ameeleza Naibu Waziri Mwanaidi.

Aidha aliongeza kuwa Wizara inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na wadau kwa lengo la kuhakikisha watoto walio katika mazingira hatarishi wanapatiwa huduma ya malezi ya muda mfupi katika Makao ya Watoto.

“Serikali na Wadau tutaendelea kushirikiana kutoa huduma kulingana na sheria, kanuni na miongozo tuliyojiwekea, nitumie fursa hii kuwaomba wamiliki wa makao ya kulelea watoto kuhakikisha mnatoa huduma kwa mtoto kwa kuzingatia maslahi mapana ya mtoto”. amesema Naibu Waziri Mwanaidi.

Mhe. Mwanaidi alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi, walezi na watendaji wa Wizara kwa kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa afua za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika makao yote hapa nchini. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu amewasihi watoto waishio katika makao hayo kuishi kwa upendo na amani huku wakiweka bidii katika masomo yao na stadi za kazi kwa ujumla ili waweze kufikia malengo yao ya baadae.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Abbot fund Edna Hauli ameipongeza Serikali kwa juhudi zake katika kuhakiksha watoto wanakuwa salama na kuahidi  kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao muhimu  na kuweza kufikia utimilifu wao kama binadamu.

Sanjari na hilo katika tukio hilo pia kuliambatana na tukio la kukabidhi mashine ya kufulia 4, printer na photocopy mashine 1, vitabu 1670 friji 2 nguo na mahitaji mengine ambavyo vilitolewa na Shirika la Abbot Fund vikiwa na thamani ya shiling Milioni 88 ili viweze kurahisisha majukumu ya utendaji kazi ndani ya Makao hayo.
 
MWISHO
Share:

TANESCO kuifanya SGR kuwa mkoa wa KI-TANESCO

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



NA MWANDISHI WETU,DODOMA

URUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema Shirika hilo lipo mbioni kuanzisha mkoa wa ki-TANESCO wa njia ya treni ya umeme (SGR)  ambao utakuwa na kazi moja tu ya kushughulikia njia ya treni hiyo ili kuondoa changamoto za kuzimika njiani.

Mhandisi Nyamo-Hanga ametoa kauli hiyo leo Machi 26 mwaka huu jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Shirika hilo katika kipindi Cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

Amesema hatua hiyo ni kufuatia changamoto zilizojitokeza awali za kukatika kwa umeme katika treni hiyo kipindi Cha awali treni hiyo  ilipoanza safari zake.

"Changamoto zilizojitokeza awali kwenye treni ya SGR kuzimika njiani , ni kwa sababu tulikuwa ndio tumeanza uendeshaji wake  na hivyo walikuwa na hatua nyingi za kujifunza kwa TANESCO  na hata kwa upande  wa SGR,kitu kinapokuwa kipya yumkini kinaweza kuleta shida kwa sababu ya ugeni wake ."amesema Mhandisi huyo

Hata hivyo amesema laini ya umeme ya SGR sasa ipo madhubuti na huduma  ya usafiri wa treni inaendelea vizuri .

"Kama shirika ,tutahakikisha SGR tunaichukulia kama mkoa ,kwamba tunaweka menejimenti na Utawala maalum kwa ajili ya mkoa huo..,katika level za kitanesco,katika kila mkoa huwa tuna Meneja wa mkoa ambaye anakuwa na timu ya watu wengi kuanzia ' registration', mafundi,mpaka wahandisi kwa ajili ya kuangalia huduma ya umeme katika mkoa huo."alisema na kuongeza kuwa 

"Timu hiyo itakuwa na kazi ya kushughulika na SGR tu lengo ni kuhakikisha kwamba umeme katika uendeshaji wa treni unakuwa wa uhakika na imara"


Share:

JK AWASILISHA UJUMBE MAALUMU KWA RAIS WA SENEGAL KUTOKA KWA RAIS SAMIA


Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi wetu

RAIS Mstaafu  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha  ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Senegal, Mhe. Bassirou Diomaye Faye jijini Dakar.

Katika mazungumzo  yao ya kirafiki,  Rais Mstaafu alieleza dhamira ya dhati ya Rais Samia na Serikali anayoiongoza ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Senegal.

Pamoja na masuala ya ushirikiano wa kiserikali, Rais Mstaafu pia alisisitiza umuhimu wa kukuza uhusiano baina ya wananchi wa mataifa haya mawili kupitia sekta za elimu, biashara, utalii, na maendeleo ya vijana na wanawake.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Tanzania kuimarisha uhusiano wa kimataifa na mataifa ya Afrika Magharibi, huku ikiweka msisitizo kwa diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa watu kwa watu.
Share:

Wizara ya Nishati yataja vipaumbele vya bajeti yake mwaka wa fedha 2025/2026

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



*📌 Rukwa, Kagera, Lindi. Mtwara kuunganishwa na gridi ya Taifa.*

*📌 Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kuendelea kuhamasishwa*

*📌 Serikali kuendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi, Mashirika  chini ya Wizara ya Nishati,*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametaja  vipaumbele vya Wizara  ya Nishati katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji,  usambazaji  umeme na kufikisha gridi ya Taifa katika Mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara;

Akiwasilisha vipaumbele hivyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Njshati na Madini, leo jijini Dodoma, Dkt. Biteko amesema  vipaumbele hivyo vimezingatia mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 hadi 2030.

“Mhe. Mwenyekiti vipaumbele hivi vimezingatia mpango wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025 - 2030 (National Energy Compact 2025 - 2030) utakaosaidia upatikanaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi, kuongeza mchango wa nishati jadidifu katika uzalishaji wa umeme na ushiriki wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya Sekta ya Nishati ”. Amesema Dkt. Biteko

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema Serikali imewajengea wazawa uwezo mkubwa wa kutekeleza miradi ya umeme huku akitolea mfano wa ajira kwenye miradi ya umeme kufikia idadi ya  53,000.

Amesema  Dunia inahitaji nishati na mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka kwa kasi hivyo Serikali itaendelea kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme ili kukidhi mahitaji ya Watanzania.

Awali, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu alisema kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika Wizara itaendelea kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project) pamoja na kufanya matengenezo na ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme;

“Mhe. Mwenyekiti tutandelea na usambazaji wa nishati katika Vitongoji, maeneo ya migodi, kilimo, viwanda na pampu za maji pamoja na vituo vya afya ili kuwezesha shughuli za
uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.” Aliongeza Lyatuu

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Lyatuu alisema Serikali itaendelea kuhamasisha na kuwezesha watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034) na mpango wa Taifa ya Nishati wa mwaka 2025 - 2030 (National Energy Compact 2025 - 2030).

Aliongeza  kuwa Serikali itaendelea na shughuli za utafutaji, uendelezaji na usambazaji wa mafuta na gesi asilia pamoja na kutekeleza miradi ya kielelezo na kimkakati ya mafuta na gesi asilia
ikiwemo Mnazi Bay Kaskazini, Eyasi - Wembere, pamoja na mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas - LNG Project).

Mradi mwingine ni ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP).

Vile vile, amesisitiza kuwa Serikali itaendela kuimarisha utendaji wa Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya TANESCO, REA, TPDC, PBPA, EWURA na PURA pamoja na Kampuni Tanzu ili yatoe huduma bora kwa wadau, kuimarisha mapato pamoja na tija na ufanisi katika uendeshaji;

Amesema lengo lingine ni kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa umeme kutoka cha sasa cha asilimia 78.4 hadi kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo ameipongeza Serikali kwa kuja na vipaumbele vitakavyowawezesha watanzania kuwa na nishati ya uhakika.
Share:

TBS lateketwza bidhaa zisizokidhi viwango za sh.bilioni 1.5


Published from Blogger Prime Android App


Joyce Kasiki,Dodoma

SHIRIKA  la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa mbalimbali zisizokidhi viwango ya ubora  vyenye thamani ya Shilingi bilioni 1.5 kati ya Julai na Disemba 2024, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kuzuia uingizaji wa bidhaa hafifu nchini.

Hayo yamesemwa Jana jijini Dodoma na Mkurugenzi  Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo hasa katika kipindi Cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Katunzi alisema  kuwa, bidhaa hizo ziliteketezwa baada ya kukutwa na kasoro mbalimbali, zikiwemo kutokuwa na viwango vya ubora vinavyotakiwa, kuwa na viambato hatarishi kwa afya, ama kuingizwa nchini bila kufuata taratibu za kisheria.

“Katika kipindi cha miezi sita, tumeteketeza bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.5, ikiwa ni hatua madhubuti ya kuzuia bidhaa zisizofaa kufika kwa watumiaji,hii ni sehemu ya mkakati wa TBS wa kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa na bidhaa salama na bora kwa wananchi,” alisema Dkt. Katunzi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,  bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku, chakula kilichoisha muda wake, vifaa vya umeme visivyokidhi viwango, pamoja na bidhaa nyingine zisizo na usajili wa ubora kutoka TBS.

Alisema, shirika hilo limeendelea kuimarisha mifumo yake ya ukaguzi wa bidhaa zinazoingia nchini, ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia za kisasa katika maabara zake 12 ambazo zote zimepata ithibati ya kimataifa. 

Dkt. Katunzi aliongeza kuwa hatua hii imewezesha kubaini kwa haraka bidhaa hafifu na kuzuia zisifike kwa watumiaji.

Mbali na ukaguzi wa bidhaa zinazoingizwa nchini,  pia TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wazalishaji wa ndani ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora unaokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

 Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, shirika hilo limeandaa viwango 1,823 vya sekta mbalimbali na kutoa vyeti na leseni za ubora 2,402 kwa wazalishaji, wakiwemo wajasiriamali wadogo 1,066.

Aidha, TBS imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali, vyuo vikuu, na mashirika ya kimataifa ili kuhakikisha mifumo yake ya udhibiti ubora inazidi kuwa na ufanisi mkubwa.

Kwa upande wa wananchi, Dkt. Katunzi aliwataka kuwa makini wanaponunua bidhaa kwa kuhakikisha zinakuwa na alama ya ubora ya TBS na kuepuka bidhaa zisizo na usajili wa shirika hilo. Pia alihimiza wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapobaini bidhaa zisizokidhi viwango zikiuzwa sokoni.

Alisema, TBS   litazidi kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wanaoingiza au kusambaza bidhaa hafifu nchini, ikiwa ni pamoja na kutaifisha na kuteketeza bidhaa hizo, pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote.


Share:

TANZANIA, BARBADOS KUIMARISHA USHIRIKIANO


Published from Blogger Prime Android App



📌 Dkt. Biteko afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Barbados

📌 Wakubaliana kuwekeza katika Ushirikiano Sekta ya Utalii na Maji 

📌 Nishati Safi ya Kupikia, M300 kivutio cha mazungumzo
 
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Barbados, Mhe. Mia Mottley ambapo wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo yamefanyika  katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mia Mottley, Jijini Bridgestone, nchini Barbados.

Waziri Mkuu Mia amesema, kuna umuhimu wa kuwa na mkakati wa pamoja na kushirikiana kwa lengo la kukuza utalii kati ya Barbados na Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla. Amesema kuna maeneo mengi ya vivutio vya utalii ambavyo vinaweza kuzinufaisha pande hizo mbili yakiwemo masuala ya ukarimu.

Maeneo mengine ya ushirikiano ni katika utoaji wa mafunzo maeneo ya ufundi kati ya nchi za Carib (Caribbean) na nchi mbalimbali za kiafrika huku akisisitiza kuwa umuhimu wa uboreshaji wa masoko na kubadilishana wataalam katika sekta mbalimbali kwa makubaliano maalum.

Aidha, amesema upo uhitaji wa wataalam katika sekta ya maji na miundombinu na hivyo kuna uwezekano wa kubadilishana wataalam ili kujengeana uzoefu katika sekta mbalimbali kulingana na makubaliano yatakayofikiwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Biteko amesema mapendekezo hayo ni mazuri na yanaweza kuwa matokeo chanya baada ya kuchambuliwa na watalaam katika sekta husika kupitia Wizara zinazohusika na masuala ya kidiplomasia.

Dkt. Biteko amesema Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendeleza kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia ambayo inalenga kuwawezesha asilimia 80 ya watumiaji wa nishati kuondokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi ifikapo mwaka 2034.

Katika utekelezaji wa mpango huo, amesema Tanzania inatembea kifua mbele kunadi mkakati huo wa miaka 10 ambao pamoja na mambo mengine unakusudia kupunguza madhara kwa watumiaji wa nishati isiyokuwa safi inayopelekea uchafuzi wa mazingira, magonjwa ya kupumua pamoja na vifo.

“Januari mwaka huu tumekuwa na mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika (M300) uliofanyika jijini Dar es Salaam ukilenga kuwa wezesha watu milioni 300 barani Afrika ambao hawajaona umeme kuweza kupata haki hiyo ikiwa ni miaka mitano kuanzia sasa na baada ya hapo itaweka namna tunavyoweza kusonga mbele kulingana na matokeo yanayofikiwa” amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko amefafanua kuwa, hatua ya Tanzania kushiriki katika mkutano wa nishati endelevu kwa wote (SEforALL) uliofanyika nchini Barbados, ni kuthibitisha nia yake thabiti inayolenga matokeo chanya. Hivyo, amesema yapo maeneo mengi ya kushirikiana na kuwezesha wananchi wa pande zote mbili kupata maendeleo na ustawi wa pamoja.

Mkutano wa Dkt. Biteko Waziri Mkuu wa Barbados, umehitimisha ziara ya kikazi nchini humo ambako alishiriki katika Kongamano la kimataifa la nishati endelevu kwa wote pamoja na mikutano ya wadau mbalimbali iliyojikita katika uboreshaji wa sekta ya nishati kwa manufaa ya nchi hizo mbili. 

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, alifuatana na Waziri wa Maji, Nishati na Mhe. Shaib Kaduara, Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Humphrey Polepole, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi Mramba na Mshauri wa Rais katika masuala ya Nishati na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Angellah Kairuki.

Mwisho.
Share:

NAIBU WAZIRI MWANAIDI APONGEZA KAMATI YA MTAKUWWA KARATU



Published from Blogger Prime Android App


Na WMJJWM - Karatu- Arusha

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwananidi Ali Khamis, ameridhishwa na Maendeleo ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kwanza wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22)

Amesema hayo Machi 14, 2025 akiwa katika ziara Wilaya ya Karatu  kwa lengo la ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa programu za malezi mbadala pamoja na programu ya uwezeshaji wa uchumi wa familia na vijana zinazotekelezwa na Shirika la SOS katika Mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri Mwananidi amepongeza Kamati za MTAKUWWA katika ngazi zote kwa kuendelea kuwa waadilifu katika kusimamia na kutekeleza majukumu yenu kikamilifu na kuimarisha ulinzi wa mwanamke na mtoto.

"Endeleeni kuzingatia matakwa ya Mwongozo wa MTAKUWWA na kuanzisha kamati katika ngazi ya Wilaya, Kata na Mitaa kwa lengo la kupunguza aina zote za vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto" amesema Naibu Waziri Mwananidi.

Ameongeza kwamba Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana Wizara za Kisekta inatekeleza Mpango Kazi wa Pili wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II 2024/25 hadi 2028/29 kwa lengo kupunguza aina zote za ukatili kwa asilimia 50.

Akiyataja mafanikio ya utekelezaji wa  Mpango Kazi wa Kwanza wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) amesema Mpango huo umesaidia kuongezeka kwa huduma za mikopo yenye masharti nafuu kupitia mifuko tofauti. Mfano mikopo ya asilimia10 inayotokana na ya mapato ya ndani ya Halmashauri kutoka Shilingi Bilioni 15.6 mwaka 2017/28 hadi Shilingi Bilioni 35.6 mwaka 2021/22.

Mafanikio mengine ni kupungua kwa vitendo vya ukatili wa  kingono kwa Wanawake kutoka asilimia 17 mwaka 2015 hadi asilimia 12 mwaka 2022, pamoja na kuongezeka kwa Vituo vya kulelea Watoto Wadogo mchana (ECD Centers)  kutoka 1,103 hadi 2,649.

Aidha, Naibu Waziri Mwananidi amelipongeza Shirika la SOS kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kuimarisha kamati za MTAKUWWA kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Vijjijini pamoja na kuwaomba viongozi wa Kamati hizo kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo stahiki ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi mzuri zaidi.


Share:

WAZIRI SILAA ASHIRIKI KUPANDISHA VIFAA UJENZI WA MNARA WA MAWASILIANO


Published from Blogger Prime Android App

Na Mwandishi Wetu, WMTH Morogoro 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), leo Machi 14, 2025, ameshiriki zoezi la kupandisha vifaa vya ujenzi wa Mnara wa Mawasiliano katika kijiji cha Idete, Kata ya Chanzuru, Kilosa, Mkoani Morogoro.

Mnara huu ni miongoni mwa minara 758 ya Mawasiliano inayojengwa na Serikali kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, kwa lengo la kuboresha huduma za mawasiliano katika vijiji vya mbali na maeneo yenye changamoto za miundombinu.

Kati ya minara 758 inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini, minara 69 inajengwa katika Mkoa wa Morogoro, ambapo minara 26 ipo katika hifadhi mbalimbali na mbuga za wanyama. Kwa upande wa Wilaya ya Kilosa pekee imenufaika kwa kupata minara 17.

Aidha, kuwepo kwa mnara wa simu katika Kijiji cha Idete unaojengwa na Kampuni ya Simu ya Airtel kutasaidia kupunguza changamoto za huduma za mawasiliano katika kijiji hicho na kunufaisha wananchi zaidi ya 7,000, hivyo kuboresha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema kuwa mnara huo unatarajiwa kukamilika na kuwashwa tarehe 1 Aprili, 2025 na kukabidhiwa rasmi tarehe 15 Aprili, 2025.

Ameongeza kuwa, hadi sasa, jumla ya minara 420 kati ya 758 imekamilika na inatoa huduma. Hii ni sawa na asilimia 55 ya utekelezaji wa mradi huo.
Share:

Waziri Silaa ataka minara yote 758 iwashwe ifikapo Mei 12 mwaka huu


Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (Mb), ameelekeza kuwa ifikapo tarehe 12 Mei 2025, saa 6 usiku,  ujenzi wa minara ya mawasiliano vijijini uwe umekamilika na minara yote 758 iwe imewashwa, ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano.

Waziri Silaa alitoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini katika kijiji cha Kidete, Kata ya Chanzuru, Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro.

“Rais Samia ametenga kiasi cha fedha Bilioni 126 kwa ajili ya ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, ambapo kukamilika kwake kutapunguza changamoto ya mawasiliano nchini,” alisema Waziri Silaa.

Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali wa miaka 10, (2024-2034) ambao una nguzo sita, ikiwemo Nguzo ya kuboresha miundombinu ya mawasiliano.

Mnara wa Idete ni moja ya minara iliyopo katika mradi wa minara 758. Mnara huu unajengwa na kampuni ya Airtel, baada ya kupata rukuzu ya serikali, na unatarajiwa kukamilika tarehe 1 Aprili 2025. Huduma zinazotarajiwa kutolewa katika mnara huu ni 2G, 3G, na 4G, hivyo wanakijiji wa kijiji cha Idete na vijiji jirani ndani ya Kata ya Chanzuru wanatarajia kupata huduma hizi mara baada ya mnara huu kukamilika.

Pia, Waziri Silaa alielekeza kuwa mnara huu uwe umewashwa ifikapo tarehe 1 Aprili 2025, na makabidhiano yafanyike tarehe 15 Aprili 2025 kama ilivyopangwa.

Hadi sasa, katika mradi wa Tanzania ya Kidijitali, minara 304 imeongezwa nguvu na imeshakamilika kwa asilimia mia moja. Aidha, katika ujenzi wa minara 758, tayari minara 420 imeshakamilika, ikiwa ni zaidi ya asilimia 55 ya utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa minara ya 758 ya mawasiliano vijijini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unatarajiwa kunufaisha wananchi wapatao milioni 8.5 waishio vijijini.
Share:

DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS


Published from Blogger Prime Android App



Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi Wetu


NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Climate Investment Funds (CIF) Bi. Tariye Gbadegesin Mjini Bridgetown, Barbados.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Machi 14, 2025 kando ya Mkutano wa Kimataifa wa kuhusu upatikanaji wa Nishati endelevu kwa wote (Energy ForAll)

Dkt. Biteko amesema kuwa, Wizara ya Nishati iko tayari kukuza ushirikiano na Taasisi hiyo ili kuunganisha juhudi za pamoja kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan maeneo ya Vijijini.

Aidha, Katika mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mshauri wa Rais Masuala ya Nishati Safi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Angellah Kairuki, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole.
Share:

Wanaofoji vyeti vya JKT waonywa


Published from Blogger Prime Android App
Na Joyce Kasiki,Dodoma








JESHI la Kujenga Taifa limetoa onyo kwa wananchi wanaoghushi vyeti vya Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa ajili ya kujitafutia  ajira huku likisema kwa waliobanika na watakaobainika kufanya hivyo kwa matumizi yoyote  watachukuliwa hatua kali za kisheria .

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitokeza kwa vitendo vya kughushi vyeti hivyo,Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala (JKT) Kanali Juma Mrai alisema vyeti hivyo vinapatikana kwa njia ya kufanya mafunzo na kuhitimu na siyo kughushi.

"Nafasi za kujiunga na Mafunzo ya JKT ,zinatolewa kila mwaka kwa vijana wa kitanzania wenye sifa ,ili wamalizapo Mafunzo ya JKT ,waweze kupata cheti cha kuhitimu Mafunzo ya JKT kihalali."alisema Kanali Mrai

Taarifa hiyo ya JKT imekuja kufuatia kubainika kuwepo kwa vyeti vya kughushi vilivyotumika na baadhi ya vijana ambao siyo waaminifu ili kujipatia ajira katika Taasisi na Makampuni yanayohitaji watendaji waliopitia Mafunzo ya JKT.

Alisema ,nafasi za kujiunga na JKT  zinatolewa kwa kutangazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii hapa nchini ,hivyo wananchi waepuke kutapeliwa kwa namna yoyote ile ikiwemo kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu zao,kupigiwa simu na kutakiwa kutoa kiasi Fulani change cha fedha ili kupata nafasi hizo.

Ametumia nafasi hiyo kutoa Rai kwa wananchi kwamba,kwa yeyote atakayepokea   ujumbe wa namna hiyo atoe taarifa haraka katika kambi yoyote ya Jeshi au kituo chochote Cha polisi kilicho karibu naye.

 Aidha Kanali Mrai alisema,JKT lipo tayari kutoa ushirikiano kwa Taasisi na Makampuni yote yanayohitajibuhakikibqa vyeti vya JKT kwa watumishi wao waliopitia Mafunzo ya JKT.
xxxx

Share:

Wananchi wa Ngombo  watakiwa  wajitokeze kuchukua fidia zao


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


📍 TAWA yaagizwa kurejesha Hifadhi ya Kilombero katika uasili wake

Na Mwandishi wetu - Malinyi.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Wakili Sebastian Waryuba amewataka wananchi waliohama kwa hiyari kutoka katika Kijiji cha Ngombo ambacho awali  kilikuwa ndani ya Pori la Akiba Kilombero ambao bado hawajalipwa fidia zao wajitokeze na kufika katika Kata ya Biro kufanya uhakiki ili kulipwa stahiki zao kabla ya mwezi Juni 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 13, 2025 wilayani humo Mhe. Wakili Sebastian Waryuba amesema Serikali ilitenga kiasi cha zaidi ya shillingi bilioni 6.9 Kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi hao huku akithibitisha kuwa zoezi la kulipa fidia hizo limekwenda vizuri    ambapo mpaka sasa Serikali imeshalipa jumla ya Kaya 998  Kati ya Kaya 1056  na kubaki Kaya 58 ambazo bado hazijalipwa, na  wanufaika wa makaburi 104 Kati ya 133  na kwa fedha zilizokwishalipwa mpaka sasa ni asilimia 97.66

"Sasa changamoto tunayoipata ni kwamba hao wanaotakiwa kulipwa hawapatikani kwa simu wala Kwa posta na hawaeleweki wako wapi. Sasa nitoe rai na wito Kwa wananchi wangu wa Ngombo ambao walistahili kulipwa fidia na hawapatikani wajitokeze waje katika Kijiji cha Biro watamkuta Mtendaji Kata atachukua takwimu na kumbukumbu zao zote ili uhakiki uendelee na waweze kulipwa, fedha za fidia za makazi na makaburi zipo, Rais Samia ameziachia zipo waje kuchukua" amesema Mhe. Sebastian.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewataka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kuendeleza Kasi ya kusafisha maeneo ya Pori la Akiba Kilombero hasa  kwenye maeneo waliyohama wananchi hao ili kurejesha uasilia wa Hifadhi hiyo ikiwemo kuondoa magofu/mahame yaliyoachwa hifadhini humo.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewashukuru wananchi hao waliofanya maamuzi ya kuhama Kwa hiyari yao wenyewe ili kupisha shughuli za uhifadhi akitaja  kitendo hicho kuwa ni cha kizalendo kinachopaswa kupigiwa mfano.

Nao wananchi waliohamia vijiji jirani kutoka Kijiji cha Ngombo  wameishukuru Serikali Kwa kuwalipa fidia zao ambazo zimewawezesha kuanza maisha mapya na kuwahamasisha wenzao 58 ambao hawajajitokeza kuchukua fidia zao, kujitokeza ili kupata stahiki zao.

"Tumetoka Ngombo tumehamia Kijiji jirani, fidia yangu nimepata na michakato ya kuhama tumefika salama na wale wenzangu ambao hawajachukua pesa naomba waende kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Biro watapata pesa zao wasiwe na hofu" amesema Maganga Mkumba aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Ngombo ambaye sasa amehamia Kijiji cha Biro.
Share:

Makamu Mwenyekiti CUF apokelewa Kondoa


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi Wetu, Kondoa 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara)  Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua  wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho ili wakazuie bajeti zinazowakandamiza Watanzania. 

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani Dunga aliwataka wananchi kuchagua wabunge na madiwani ili wakazuie bajeti zinaxowakabili wananchi. 
Alisema kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani. 

Alisema kuwa kwa sasa asilimia 99 ya wabunge wanatatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Alisema kuwa iwapo wananchi watakichagua chama hicho, watauza mazao yao vizuri,tofauti na sasa wananchi wanalazimishwa kuuza mazso kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wamekuwa wakiuza kwa mkopo. 

"Hospitali nyingi zimejengwa lakini  hakuna huduma,hakuna dawa  lakini CUF itahakikisha huduma zinaboreshwa hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa wakipata adha kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, "alisema 

Alisema kuwa umaskini wa wananchi sio laana ya Mungu , CUF  ikishika dola itafanikisha mambo mengi ikiwemo wazee watapata posho ya kujikimu kila mwezi, "alisema. 

Alisema kuwa elimu bure haijaleta matokeo mazuri kwa wananchi kutokana na shule nyingi kuwa na michango mingi inayozidi hata ada zilizoondolewa. 

Katika mkutano huo zaidi ya wanachama wapya 20 walikabidhiwa kadi. 
Mkazi wa Kondoa, Hamidu Mkopi alitaka wananchi kuziishi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan. 

Wakati huo huo  mtu  mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa  bendera na mabango ya Chama cha CUF  wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho  Dunga 

Wakizungumzia tukio hilo,  Mjumbe wa kamati tendaji CUF wilaya ya Kondoa, Ayubu Hamisi alisema kuwa asubuhi ya Machi 7 mwaka huu, wakati wakiwa katika maandalizi ya kumpokea Makamu Mwenyekiti Othuman Dunga kulitokea  jambo la kusikitisha ambapo  vijana wanaosadikiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  waliingia mitaani na kung'oa bendera 13 na mabango 25 .

Alisema kuwa baada ya kufanya msako waliweza kumkamata kijana mmoja ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliofanya uhalifu huo na sasa anashikiliwa na Jeshi la polisi. 

Mwanachama wa Chama hicho, Hadija Selemani alisema kuwa kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimewasikitisha sana. "Tulikuwa tumejiandaa vizuri wanachama wamefika wakiwa wamevalia sare zao vizuri kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao lakini kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimetusikitisha sana," alisema na kuongeza. 

"Jambo hili limetusikitisha sana kwani kwa mara ya kwanza Kondoa inapata kiongozi  mwenye wadhifa mkubwa, lakini wasiotutakia mema ,wameshusha bendera, waking'oa mabango  ,kinachofanyiika ni mbinu za kuua siasa za upinzani jambo ambalo  limeleta taharuki,"alisema

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kupokelewa wilayani Kondoa Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga,, alisema hiyo ni mara ya pili bendera za chama hicho zinang'olewa wakati chama hicho kikiwa na mikutano.

Alisema kuwa tukio  kama hilo lilitokea Julai mwaka jana wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipofika Kondoa ambapo bendera zaidi ya 60 ziling'olewa siku moja kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano.

"Huo ni uoga tushindane kwa hoja na sio kung'oa mabango na kuleta taharuki, "Alisema 
Dunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kondoa 

"Wakati wengine wakihangaika kushusha bendera sisi  tunahangaika kutafuta wanachama wapya wajiunge na chama. 
Nyie ng'oeni bendera  sisi tutaiba nyoyo za watu ili wajiunge kwa wingi na CUF, "alisema. 

Alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, George Katabazi alisema kuwa taarifa kamili hazijamfikia anafuatilia suala hilo na atatoa taarifa .


Share:

BUWSSA NA MIKAKATI YA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI KUTOKA ASILIMIA 64 HADI 32.









Published from Blogger Prime Android App

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

MKURUGENZI Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda Bi. Ester Gilyoma ameeleza Mikakati ya kupunguza Upotevu wa maji katika mjinhuo ambapo amesema mwaka 2021 upotevu ulikuwa asilimia 64 lakini kwasasa ni asilimia 32 kutokana na maboresho ya bomba chakavu na ubadilishaji wa mita goi goi.

Bi Ester ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Machi 6,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan. 

Na kuongeza kuwa upotevu wa maji wa asilimia 64 ulitokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kutoka mwaka 1972 lakini Serikali ya awamu ya sita ilitoa fedha na kufanya matengenezo ya bomba hizo pamoja na mita.

"Upotevu wa maji kwa 2021 ulikuwa wastani wa asilimia 64 kutokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972,baada ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita za kutoa fedha na kubadili bomba chakavu na mita goi goi upotevu wa maji kwasasa ni asilimia 32 na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika".

Aidha amesema kuwa tangu awamu ya sita kuingia Madarakani Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imepitishiwa 
miradi ya thamani ya TShs 28,180,572,033.71 na Tshs 11,894,976,776.81 taryari zimepokelewa 
na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.
 
Mamlaka hiyo pia imenufaisha wakazi 195,848  mwaka 2024 kati  ya hao Asilimia 85 yenye sawa na wakazi 165,613 wamepata huduma ya maji ya bomba  Kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa  Dkt samia.

Ambapo amebainisha chanzo cha maji hayo kuwa ni ziwa vikitoria ambapo kuna umbali wa kilomita 24.8 kutoka katika kijiji cha Nyabehu na uzalishwaji wake ni wastani wa mita za ujazo 2976m3 kwa siku.

Pamoja na kupambana na usafi wa mazingira  kwa sasa Mamlaka ya maji safi Bunda inaujenzi wa mradi wa miundombinu ya majitaka katika eneo la Butakale ,kwa ajili ya usafi wa  mazingira na mradi utakamika ndani ya mwaka huu wa fedha 2024/2025.

 Vile vile  Mwenyekiti wa bodi ya maji safi bunda  Bwana Jushua chacha Merumbe, ameeleza kuwa hali iliyopo sasa hivi bunda ni bora kuliku hapo awali pia amesema kwa kata 13 zilizopatiwa maji zinaendelea kutumia na  kufurahia huduma hiyo ambayo awali ilikuwa ni changamoto kwa wakazi wa mji wa Bunda.
Share:

Wahifadhi Wanawake wa TAWA Watembelea Pori la Akiba Wami-mbiki 

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


📍 Wahamasisha utalii wa ndani 

Na. Joyce Ndunguru- Morogoro.

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake , wahifadhi wanawake wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapaori Tanzania (TAWA) wametembelea Pori la Akiba Wamimbiki lililopo katika Mikoa ya Morogoro na Pwani kwa lengo la kuhamamisha utalii wa ndani.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, iliyofanyika Machi 1, 2025, Afisa Mhifadhi Mkuu, Zuwena Kikoti alisema wahifadhi wanawake wa TAWA wanaungana na wanawake wote nchini katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii duniani.

"Tumeungana na jitihada hizo kama wanawake kwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuvitangaza na kuwahamisha wanawake wa Mkoa wa Morogoro na Mikoa ya jirani kutembelea hifadhi ya Wamimbiki katika kusheherekea siku ya wanawake duniani" aliongeza Afisa Mhifadhi Kikoti.

Kwa upande wake, akimwakilisha Kamanda wa Pori la Akiba Wamimbiki Afisa Utalii, Gregory Kalokole alisema hifadhi ya Wamimbiki ni mpya na ya kimkakati yenye vivutio vingi vya utalii ikiwemo vivutio vya asili na vivutio vya utamaduni.

"Pori la Akiba Wamimbiki lina mandhari nzuri iliyozungukwa na miti ya miombo, wanyamapori kama vile Tembo, Simba, Viboko, Chui, Fisi, Tandala, Swala pala na Kulo na asilimia takribani 20 ya Mto Wami umepita ndani ya hifadhi" aliongeza Afisa Utalii Kalokole.

Sambamba na hilo, Kalokole alitoa shukrani zake kwa wahifadhi wanawake kutembelea hifadhi hiyo na alitoa rai kwa makundi mbalimbali ya wanawake na watanzania wote kwa ujumla kuja kutembela hifadhi hii. 

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake yamepangwa kufanyika Kitaifa Jijini Arusha Machi 8,2025 na kauli mbiu ya mwaka huu ni Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.