


Na Mwandishi Wetu, Kondoa
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa (Bara) Omar Dunga amepokelewa katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma huku akiwataka Watanzania kufanya mabadiliko ya kuwachagua wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho ili wakazuie bajeti zinazowakandamiza Watanzania.
Akizungumza na wananchi katika uwanja wa stendi ya zamani Dunga aliwataka wananchi kuchagua wabunge na madiwani ili wakazuie bajeti zinaxowakabili wananchi.
Alisema kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.
Alisema kuwa kwa sasa asilimia 99 ya wabunge wanatatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Alisema kuwa iwapo wananchi watakichagua chama hicho, watauza mazao yao vizuri,tofauti na sasa wananchi wanalazimishwa kuuza mazso kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo wamekuwa wakiuza kwa mkopo.
"Hospitali nyingi zimejengwa lakini hakuna huduma,hakuna dawa lakini CUF itahakikisha huduma zinaboreshwa hasa vijijini ambapo wananchi wamekuwa wakipata adha kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, "alisema
Alisema kuwa umaskini wa wananchi sio laana ya Mungu , CUF ikishika dola itafanikisha mambo mengi ikiwemo wazee watapata posho ya kujikimu kila mwezi, "alisema.
Alisema kuwa elimu bure haijaleta matokeo mazuri kwa wananchi kutokana na shule nyingi kuwa na michango mingi inayozidi hata ada zilizoondolewa.
Katika mkutano huo zaidi ya wanachama wapya 20 walikabidhiwa kadi.
Mkazi wa Kondoa, Hamidu Mkopi alitaka wananchi kuziishi 4R za Rais Samia Suluhu Hassan.
Wakati huo huo mtu mmoja anashikikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kukamatwa aking'oa bendera na mabango ya Chama cha CUF wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Dunga
Wakizungumzia tukio hilo, Mjumbe wa kamati tendaji CUF wilaya ya Kondoa, Ayubu Hamisi alisema kuwa asubuhi ya Machi 7 mwaka huu, wakati wakiwa katika maandalizi ya kumpokea Makamu Mwenyekiti Othuman Dunga kulitokea jambo la kusikitisha ambapo vijana wanaosadikiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliingia mitaani na kung'oa bendera 13 na mabango 25 .
Alisema kuwa baada ya kufanya msako waliweza kumkamata kijana mmoja ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliofanya uhalifu huo na sasa anashikiliwa na Jeshi la polisi.
Mwanachama wa Chama hicho, Hadija Selemani alisema kuwa kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimewasikitisha sana. "Tulikuwa tumejiandaa vizuri wanachama wamefika wakiwa wamevalia sare zao vizuri kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao lakini kitendo cha kung'oa mabango na bendera za CUF kimetusikitisha sana," alisema na kuongeza.
"Jambo hili limetusikitisha sana kwani kwa mara ya kwanza Kondoa inapata kiongozi mwenye wadhifa mkubwa, lakini wasiotutakia mema ,wameshusha bendera, waking'oa mabango ,kinachofanyiika ni mbinu za kuua siasa za upinzani jambo ambalo limeleta taharuki,"alisema
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kupokelewa wilayani Kondoa Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa (Bara) Othuman Dunga,, alisema hiyo ni mara ya pili bendera za chama hicho zinang'olewa wakati chama hicho kikiwa na mikutano.
Alisema kuwa tukio kama hilo lilitokea Julai mwaka jana wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipofika Kondoa ambapo bendera zaidi ya 60 ziling'olewa siku moja kabla ya kiongozi huyo kufanya mkutano.
"Huo ni uoga tushindane kwa hoja na sio kung'oa mabango na kuleta taharuki, "Alisema
Dunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kondoa
"Wakati wengine wakihangaika kushusha bendera sisi tunahangaika kutafuta wanachama wapya wajiunge na chama.
Nyie ng'oeni bendera sisi tutaiba nyoyo za watu ili wajiunge kwa wingi na CUF, "alisema.
Alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, George Katabazi alisema kuwa taarifa kamili hazijamfikia anafuatilia suala hilo na atatoa taarifa .
No comments:
Post a Comment