UWT yalaani Mwenezi BAWACHA kushambuliwa


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,Dodoma
UMOJA  wa Wanawake wa  Chama cha Mapinduzi Taifa (UWT), umelaani shambulio la kudhuru mwili alilofanyiwa Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Sigilaga Mligo, ambalo limesababisha maumivu makali hadi kupelekea kulazwa hospitalini huku akishangazwa na uongozi wa CHADEMA Taifa kukalia kimya suala hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa UWT  Taifa Mary Chatanda amesema  kuwa shambulio hilo ni aina ya unyanyasaji, ukandamizaji, na uonevu dhidi ya mwanamke lakini pia na mfumo dume uliopo katika chama cha CHADEMA

Amesema kitendo hicho kinakwenda kinyuma na madhumuni ya UWT, kama inavyoelezwa katika kifungu (f) cha katiba yake, kinachotamka kuwa Umoja huo ni chombo cha ukombozi wa wanawake wa Tanzania dhidi ya unyanyasaji, unyonyaji, ukandamizaji, na mila zote zinazorudisha nyuma maendeleo ya wanawake.

UWT imeeleza masikitiko yake kuhusu mazingira ya tukio hilo, ambapo inadaiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, alikuwepo lakini hakuchukua hatua yoyote.

Umoja huo umehoji ukimya wa viongozi wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) kuhusu shambulio hilo, hasa kwa kuwa mhanga ni kiongozi wa ngazi ya juu katika baraza hilo.

Kadhalika, UWT imeitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufuatilia kwa karibu uanzishwaji wa madawati ya jinsia ndani ya vyama vya siasa, kama inavyotakiwa na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2023. Umoja huo unataka madawati hayo yawe na mamlaka na uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, na ukandamizaji wa kijinsia katika siasa.

Katika hatua nyingine, UWT imewataka wanawake kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi pindi muda utakapofika, ikisisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wa kikatiba na unapaswa kuwa huru na wa haki.

UWT imetoa pole kwa Bi. Sigilaga Mligo na kumtakia uponyaji wa haraka, huku ikihimiza hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika katika shambulio hilo.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.