Waziri Silaa ataka minara yote 758 iwashwe ifikapo Mei 12 mwaka huu


Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi Wetu

WAZIRI  wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa (Mb), ameelekeza kuwa ifikapo tarehe 12 Mei 2025, saa 6 usiku,  ujenzi wa minara ya mawasiliano vijijini uwe umekamilika na minara yote 758 iwe imewashwa, ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano.

Waziri Silaa alitoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini katika kijiji cha Kidete, Kata ya Chanzuru, Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro.

“Rais Samia ametenga kiasi cha fedha Bilioni 126 kwa ajili ya ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, ambapo kukamilika kwake kutapunguza changamoto ya mawasiliano nchini,” alisema Waziri Silaa.

Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidijitali wa miaka 10, (2024-2034) ambao una nguzo sita, ikiwemo Nguzo ya kuboresha miundombinu ya mawasiliano.

Mnara wa Idete ni moja ya minara iliyopo katika mradi wa minara 758. Mnara huu unajengwa na kampuni ya Airtel, baada ya kupata rukuzu ya serikali, na unatarajiwa kukamilika tarehe 1 Aprili 2025. Huduma zinazotarajiwa kutolewa katika mnara huu ni 2G, 3G, na 4G, hivyo wanakijiji wa kijiji cha Idete na vijiji jirani ndani ya Kata ya Chanzuru wanatarajia kupata huduma hizi mara baada ya mnara huu kukamilika.

Pia, Waziri Silaa alielekeza kuwa mnara huu uwe umewashwa ifikapo tarehe 1 Aprili 2025, na makabidhiano yafanyike tarehe 15 Aprili 2025 kama ilivyopangwa.

Hadi sasa, katika mradi wa Tanzania ya Kidijitali, minara 304 imeongezwa nguvu na imeshakamilika kwa asilimia mia moja. Aidha, katika ujenzi wa minara 758, tayari minara 420 imeshakamilika, ikiwa ni zaidi ya asilimia 55 ya utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa minara ya 758 ya mawasiliano vijijini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unatarajiwa kunufaisha wananchi wapatao milioni 8.5 waishio vijijini.
Share:

Related Posts:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.