Watafiti UDOM wavumbua njia ya haraka ya kugundua dawa kwa akili mnemba

Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi wetu

 CHUO  Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeibuka na ubunifu mpya wa kiteknolojia unaotumia akili mnemba (AI) katika mchakato wa kugundua tiba za magonjwa mbalimbali yanayoikumba jamii, hatua inayotarajiwa kurahisisha kazi ya watafiti na kuchochea upatikanaji wa tiba nchini.

Teknolojia hiyo, inayojulikana kama ConizuroAI.com, imewasilishwa katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo, mtafiti kutoka UDOM, Jospeter Jonathan, amesema mfumo huo wa ConizuroAI umetengenezwa mahususi kusaidia watafiti wa tiba kupata njia rahisi, ya haraka na ya gharama nafuu katika kugundua dawa, tofauti na mbinu za zamani zilizohitaji muda mrefu, utaalam wa hali ya juu na rasilimali kubwa.

 “Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa njia mbadala katika tafiti za tiba,kupitia ConizuroAI, daktari anaweza kutumia akili mnemba kuchambua taarifa mbalimbali za magonjwa na kuibua suluhisho la kitabibu kwa urahisi zaidi,” amesema Jonathan.

Amefafanua kuwa licha ya uwepo wa wataalamu wengi nchini, wengi wao wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kutopata zana wezeshi katika tafiti zao, jambo linalorudisha nyuma juhudi za kugundua tiba mpya.

Amesema,teknolojia hiyo tayari imeanza kutumika na watafiti ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, na kwa sasa inavutia taasisi mbalimbali zilizotembelea banda la UDOM katika maonesho hayo, huku baadhi ya watafiti wakionyesha nia ya kuanza kuitumia katika kazi zao.

 “Lengo letu ni kuwa na idadi kubwa ya watafiti wanaoitumia teknolojia hii ndani ya mwaka mmoja au miwili. Hii itasaidia kuharakisha upatikanaji wa tiba  kwa magonjwa sugu au yasiyo na tiba ya moja kwa moja,” aliongeza.

Uanzishaji wa ConizuroAI unatajwa kuwa hatua muhimu katika mageuzi ya tafiti za kitabibu nchini, hasa kwa kuzingatia azma ya Tanzania ya kujitegemea katika sekta ya afya na kupunguza utegemezi wa dawa kutoka nje.
Share:

VETA kuanzisha mafunzo ya stadi za mikono kwa watoto wadogo,hatua mpya ya Kuijenga Tanzania ya viwanda



Published from Blogger Prime Android App
Mkufunzi wa VETA Faulata Mtalemwa akiwa na watoto waliotembelea  Banda la VETA kona ya watoto kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.






Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM


MAMLAKA  ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeandaa mpango kabambe wa kuanzisha programu maalum ya kuwafundisha watoto wadogo stadi za mikono, ikiwa ni hatua ya kimkakati katika kukuza vipaji na kuandaa kizazi cha Tanzania ya viwanda inayojitegemea.

Hayo yamesemwa Julai 4 ,2025 na Mkufunzi kutoka VETA Songea Faulata Mtalemwa katika Banda la VETA ,kona ya watoto ambapo amesema kitengo hicho kimeanzishwa Ili kutambulisha Mpango huo. 

Amesema Mpango huo unaotarajiwa kuanza rasmi mwakani na kwamba utatekelezwa katika vyuo vyote vya VETA nchini, ambapo kila kituo kitapanga muda maalum katika kipindi cha likizo kwa ajili ya kuwafundisha watoto mbinu mbalimbali za ufundi stadi ambapo  Wazazi watachangia gharama ndogo tu, hususan kwa ajili ya chakula na huduma za msingi wakati wa mafunzo hayo.

Kuibua vipaji mapema

Mtalemwa amesema wa lengo la programu hiyo ni kuanza kuwaandaa watoto kuifahamu thamani ya kazi za mikono wakiwa katika umri mdogo, hatua itakayosaidia kukuza vipaji na uwezo wa ubunifu kabla hata hawajafikia umri wa ujana.

“Tunatamani kuibua mafundi, wahandishi, wabunifu na wajasiriamali kuanzia utotoni,na katika umri mdogo, mtoto ana uwezo mkubwa wa kushika na kukumbuka jambo,tukiwapa maarifa mapema, tunawajengea msingi imara wa maisha yao ya baadaye,” amesema.

Maeneo ya Mafunzo

Mafunzo yatakayofundishwa kwa watoto yamegawanywa kulingana na mahitaji ya msingi na usalama wa mtoto lakini pia kulingana na umri wa mtoto husika , yakiwemo:

Ujenzi wa vitu vidogo kama nyumba za matofali ya matope au mfano wa upakaji rangi,umeme wa majumbani mfano, namna ya kutumia swichi kwa usalama, kutambua waya hatarishi, na mbinu rahisi za kuhifadhi vifaa vya umeme.

Vile vile amesema watafundishwa ushonaji mfano kufunga vifungo, kurudishia nguo zilizochanika, kukukunja nguo vizuri,utunzaji wa mavazi kwa ujumla pamoja na Stadi za maisha kama kupamba meza, kupanga vitu, kusuka nywele, usafi wa mazingira, na kazi ndogo ndogo za kusaidia nyumbani.

Kuibadilisha Mitazamo ya Jamii

Mtalemwa amesema mpango huo pia ni sehemu ya juhudi za VETA kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu elimu ya ufundi stadi, ambayo kwa muda mrefu imeonekana kuwa ni ya watu waliokosa nafasi nyingine.

“Jamii nyingi za magharibi zimepiga hatua kwa sababu waliwekeza katika stadi za mikono, Tanzania tuna uwezo, tuna vijana wengi wenye vipaji tunachohitaji ni kuviendeleza mapema,” amesisitiza

Kona ya watoto maonyesho ya Kitaifa

Kufuatia hali hiyo amesema,katika kuhamasisha jamii na kuonyesha mwelekeo mpya, katika maonyesho ya mwaka huu kwa mara ya kwanza VETA ambayo  hii inalenga kuwaonesha Watanzania kuwa vipaji vya watoto vinaweza kulelewa mapema na kuzaa mafanikio makubwa.

"Watoto wanaopata nafasi ya kupiga katika Kona hii, walionyesha kazi mbalimbali, zikiwemo kazi za ufundi, uchoraji, kushona, na hata kubuni bidhaa rahisi kwa kutumia vifaa vya kawaida jambo lililowagusa na kuwatia moyo wazazi wengi waliotembelea banda hilo."amesema Mtalemwa

Aidha Mkufunzi huyo amesema hatua hiyo itasaidia kujenga Taifa imara kwa Msingi Imara

“Hili ni jibu kwa changamoto ya kizazi kinachokua bila maarifa ya msingi ya maisha maana wazazi tumekuwa tunahangaika kutafuta fedha, lakini tusisahau msingi wa kulea watoto. Kupitia VETA, tunatengeneza jamii yenye ujuzi, yenye kujiamini, na inayoweza kulibeba Taifa kwa maendeleo,” 








Share:

Baba Levo Atoa Hamasa Banda la TTCL Maonesho ya Sabasaba



Published from Blogger Prime Android App




Na Mwandishi Wetu

MSANII na mtangazaji maarufu nchini, ambaye pia ni Balozi wa Kampeni ya Walete inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, ametembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Baba Levo alitumia fursa ya kuzungumza na wateja wa TTCL, kuhamasisha matumizi ya huduma za shirika hilo, pamoja na kueleza mchango wa TTCL katika kuleta mapinduzi ya kidijitali nchini. Aidha, alitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa juhudi zake katika kuhakikisha shirika hilo linaendelea kuwa mhimili mkuu wa mawasiliano nchini.

Akizungumza akiwa katika banda hilo, Baba Levo alisema "TTCL ni alama ya taifa. Tunapaswa kujivunia kuwa na taasisi ya kizalendo inayohakikisha mawasiliano ya Watanzania yanakuwa salama, ya uhakika na ya gharama nafuu.”


Pia aliwapongeza wataalamu wa TTCL kwa mafanikio ya kiteknolojia waliopiga hatua nayo, ikiwemo usambazaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kuanzishwa kwa Kituo cha Kuhifadhi Data Kimtandao (Data Center), utoaji wa huduma za intaneti ya kasi, huduma za simu pamoja na bidhaa za kisasa kama vile modemu, MiFi, na huduma ya faiba mlangoni inayowezesha matumizi ya teknolojia ya kisasa majumbani.

Ziara hiyo ya Baba Levo ilivutia umati mkubwa wa wananchi na mashabiki, waliokusanyika kwa wingi kushuhudia msanii huyo akishirikiana na watumishi wa TTCL kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali za shirika hilo la kihistoria.

Kwa upande wake, Meneja wa Banda la TTCL ambaye pia ni Meneja wa Bidhaa, Bi. Janeth Maeda, alisema ujio wa Baba Levo ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya taasisi za umma na watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii.

"Tunamshukuru Baba Levo kwa kutenga muda wake kututembelea. Hii ni ishara kuwa jamii inatambua umuhimu wa TTCL kama taasisi ya umma inayotekeleza dhamira ya Serikali ya kuwafikishia Watanzania wote huduma za mawasiliano,” alisema Bi. Maeda.



Share:

SADC YAITAJA TANZANIA KINARA UTEKELEZAJI AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA*




Published from Blogger Prime Android App



📌 *Rais Samia aendelea kupongezwa kwa kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia Afrika*

📌 *Mhe. Kapinga ataka mikakati, ubunifu utekelezaji nishati safi ya Kupikia Jumuiya ya  SADC*

📌 *Asisitiza uelimishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia kupewa nguvu*

📌 *SADC yapongeza Tanzania mkutano wa Misheni 300*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa kinara namba moja wa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Afrika na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya  Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 3, 2025 na Viongozi mbalimbali na Wataalam kutoka Nchi nane za (SADC) ambao wamekutana jijini Harare nchini Zimbabwe katika Mkutano  unaolenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji.

Akizungumza Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Serikali imeendelea kuwezesha, kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia (2024 – 2034).

Kuhusu utekelezaji wa nishati safi ya kupikia kwa jumuiya hiyo, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka dhamira na mikakati ya utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kuwafikia watu wengi zaidi SADC. 

Vilevile, amesisitiza SADC kuwa wabunifu katika matumizi ya nyenzo mbalimbali zitakazowezesha na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku akitolea mfano matumizi ya mkaa mbadala kama vile wa rafiki briquettes katika matumizi ya kupikia kama njia ya kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo kwa wananchi. 

Pia, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka nguvu zaidi katika uelimishaji na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuwataka wanachama wa SADC kuweka mkakati utakaowezesha unarahisisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kuwa muhimu kwa uchumi endelevu katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kapinga amepokea pongezi zilizotolewa na Wanachama wa SADC kwa Tanzania kwa  kuandaa, kuwa mwenyeji na kufanikisha mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Nishati wa Afrika (Misheni 300 - M300) kwa ufanisi mkubwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Naye, Waziri wa Nishati wa Malawi, Mhe. Ibrahim Matola amempongeza Rais Samia kwa uthubutu wake wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania. Mhe. Matola ameitaka SADC kuitumia Tanzania kama balozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika jumuiya hiyo.

Mkutano huo umehudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa  Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na  Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Share:

Elimu ya VETA yamsaidia kijana kujikwamua kiuchumi na kuajiri wengine




Published from Blogger Prime Android App

Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

MWANAFUNZI  aliyekuwa akisoma kozi ya Hoteli na Utalii katika Chuo cha VETA Njiro Fredrck Mlay , amefanikiwa kuibadili kabisa hali yake ya kiuchumi na kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine kwa kujiajiri mwenyewe baada ya kuhitimu masomo yake.

 Fredrick alianza kozi hiyo mwaka 2023 na kuhitimu Mei 2025 akiwa na Cheti na Diploma, elimu ambayo imekuwa nguzo kubwa ya mafanikio yake ya sasa.

Kupitia kiwango cha cheti, alipata maarifa kuhusu jinsi ya kuongeza idadi ya watalii wanaovutiwa na mbuga za wanyama  huku kiwango cha diploma kikimuwezesha kuelewa mbinu za ubunifu na uuzaji wa vinywaji mbalimbali katika hoteli  ikiwa ni pamoja na vinywaji vikali na laini vinavyotengenezwa kwa matunda.

Akizungumza Julai 2,2025  katika Banda la VETA kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya 49  Fredrick amesema,"Elimu ya VETA imenipa ujuzi ambao umeniwezesha kujiamini, kujiendeleza na sasa kuajiri vijana wenzangu,”

Fredrick amesema kwa   anatengeneza vinywaji kama juisi , cocktails na pombe kali , akitumia matunda na viambato halali. Vinywaji hivyo hutumika katika hafla mbalimbali kama harusi na matamasha.

Aidha amesema, alichagua kozi hiyo ili aweze kuitumia kama daraja la kujiajiri. "Katika kozi hii nimejifunza mengi  ikiwemo namna ya kuhudumia wageni, masoko, usimamizi wa shughuli, pamoja na kutengeneza cocktails kwa kutumia matunda na alcohol,” anaeleza.

Mbali na kujiajiri amesema elimu hiyo imemsaidia pia kuwa sehemu ya suluhisho kwa vijana wasiokuwa na ajira ambapo kwenye shughuli zake, huwashirikisha vijana ambao wengi wao hawakuwa na ujuzi, lakini sasa wanajifunza, wanapata uzoefu na kipato.

“Katika kazi zangu, hasa kwenye matukio kama harusi na sherehe, huwa nachukua vijana kufanya kazi nami. Hii imenisaidia mimi kiuchumi na pia kuwapa wao fursa ya kipato na maarifa. Wengine wameendelea na kazi hadi sasa,” anasema kwa fahari.

Kijana huyo amesema,mpango wake wa baadaye ni kufungua mgahawa mkubwa wa kisasa, ambao utatoa ajira kwa vijana wengi zaidi wakiwemo wale ambao hawakubahatika kusoma VETA kutokana na changamoto mbalimbali.

Anahitimisha kwa kuwasihi vijana wa Kitanzania kujiunga na vyuo vya VETA ili wapate ujuzi wa kuwasaidia kujiendeleza kimaisha na kuchangia katika maendeleo ya taifa. “Ujuzi ndio msingi wa mafanikio ya kweli, na VETA ndio sehemu sahihi ya kuanzia,” amesema.













Share:

TMDA yaendelea kuhakikisha Usalama wa Dawa Sokoni — Mkurugenzi Mkuu



Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

 
MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA), Dkt. Adam Fimbo, amesema kuwa TMDA inaendelea kuhakikisha kuwa dawa zinazosambazwa na kutumiwa na wananchi nchini ni salama, zenye ubora unaokubalika na zinafanya kazi iliyokusudiwa bila kusababisha madhara kwa binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3,2025  katika Banda la TMDA kwenye Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Dkt. Fimbo alisema moja ya majukumu makuu ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa kila dawa inayotumiwa na binadamu haimdhuru, bali inamponya kwa mujibu wa madhumuni ya matumizi yake.

 “Dawa yoyote inayotumiwa na binadamu haipaswi kumdhuru, Jukumu letu kama TMDA ni kuhakikisha dawa hiyo inafanya kazi iliyokusudiwa , yaani inatibu, siyo kuleta madhara,” alisisitiza Dkt. Fimbo.

Alieleza kuwa TMDA hufuatilia kwa ukaribu madhara yanayoweza kujitokeza kwa watumiaji wa dawa baada ya matumizi na huchukua hatua stahiki ili kuzuia madhara zaidi kwa umma.

 Aidha, alisema mamlaka hiyo imewekeza katika maabara za kisasa ambazo zimethibitishwa kimataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO), na ni miongoni mwa maabara chache zenye uwezo mkubwa wa kupima ubora wa dawa barani Afrika.

 “Tunapima bidhaa za dawa kwenye maabara zetu zilizoidhinishwa na WHO,maabara yetu ni miongoni mwa maabara Bora Afrika zenye viwango vya kinataifa"amesisitiza

Ni maabara chache za aina hii, na sisi ni miongoni mwao. Hivyo, tunaruhusu dawa tu ambazo zimekidhi viwango vilivyowekwa kimataifa,” alieleza.

Mbali na udhibiti wa dawa amesema , TMDA pia inasimamia bidhaa za tumbaku, kwa lengo la kuwalinda wananchi dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa hizo.

 Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi ya kudhibiti usambazaji na matumizi holela ya bidhaa hizo ili kuhakikisha usalama wa afya ya jamii.

 Dkt. Fimbo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na TMDA kwa kutoa taarifa za dawa au bidhaa zinazohisiwa kuwa na madhara, ili kuchukua hatua za haraka.

Aidha Fimbo ametumia nafasi hiyo kuwaasa  wananchi wote kufika katika banda hilo  kupata elimu kuhusu usalama wa dawa, vifaa tiba, na vitendanishi .

Share:

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

Published from Blogger Prime Android App


🔴🔴Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

📍  Milango ya uwekezaji bado iko wazi

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuimarisha mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hatua inayolenga kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta mbalimbali, hususan sekta ya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa TAWA, Bw. Beatus Maganja, amesema taasisi hiyo inaendelea kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza  katika maeneo mbalimbali ikiwemo utalii wa picha na uwindaji wa kitalii.

“Tunawaambia Watanzania na wawekezaji  wote kwa ujumla kuwa TAWA ni mahali sahihi kwa uwekezaji, unapotaka kuwekeza unakaribishwa sana. Ikumbukwe kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa mazingira wezeshi Kwa wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi yetu ” alisema Maganja.

"Kama alivyofanya Mhe. Rais na sisi tunamuunga mkono Kwa kuhakikisha kwamba fursa hizi zinakuwa wazi Kwa wawekezaji wote na ndio maana tuko hapa kuwatangazia waje kuwekeza katika hii taasisi" amesisitiza Afisa Habari huyo.

Aidha Maganja ameongeza kuwa TAWA inasimamia maeneo yenye rasilimali adimu, vivutio vya kipekee, na mandhari ya kuvutia ambayo yanatoa fursa kubwa ya uwekezaji endelevu kwa maslahi ya taifa na uhifadhi wa maliasili.

Bw. Maganja alitaja baadhi ya maeneo yaliyo  tayari kwa uwekezaji kuwa ni Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park (Arusha), Wami-Mbiki (Morogoro), Mpanga/Kipengere (Mbeya na Njombe), Tabora ZOO, Ruhila ZOO na maeneo mengine mengi yenye fursa mbalimbali.

Kwa upande wake, Afisa Mhifadhi Mkuu kutoka TAWA, Dkt. Gladson Mlay, aliwahamasisha wananchi kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho hayo, ambapo wanaweza kujionea wanyamapori hai wakiwemo simba, chui, fisi, mamba na spishi mbalimbali za ndege.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaalika wananchi kuonja na kununua kitoweo cha nyamapori choma kilichoandaliwa kwa umahiri, akisema kuwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha matumizi ya rasilimali za maliasili kwa njia endelevu.

“Kwa wale ambao wanasema hawajawahi Kula nyamapori choma, nyama hiyo ipo hapa, mishikaki pia ipo na nyama ya kupeleka nyumbani nyumbani. Kwahiyo watu  wote mnakaribishwa mje kuonja, Kula na kuona ka
Kweli maliasili ni za kwetu wote” alisema Dkt. Mlay
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.