Watafiti UDOM wavumbua njia ya haraka ya kugundua dawa kwa akili mnemba

Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi wetu

 CHUO  Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeibuka na ubunifu mpya wa kiteknolojia unaotumia akili mnemba (AI) katika mchakato wa kugundua tiba za magonjwa mbalimbali yanayoikumba jamii, hatua inayotarajiwa kurahisisha kazi ya watafiti na kuchochea upatikanaji wa tiba nchini.

Teknolojia hiyo, inayojulikana kama ConizuroAI.com, imewasilishwa katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo, mtafiti kutoka UDOM, Jospeter Jonathan, amesema mfumo huo wa ConizuroAI umetengenezwa mahususi kusaidia watafiti wa tiba kupata njia rahisi, ya haraka na ya gharama nafuu katika kugundua dawa, tofauti na mbinu za zamani zilizohitaji muda mrefu, utaalam wa hali ya juu na rasilimali kubwa.

 “Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa njia mbadala katika tafiti za tiba,kupitia ConizuroAI, daktari anaweza kutumia akili mnemba kuchambua taarifa mbalimbali za magonjwa na kuibua suluhisho la kitabibu kwa urahisi zaidi,” amesema Jonathan.

Amefafanua kuwa licha ya uwepo wa wataalamu wengi nchini, wengi wao wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kutopata zana wezeshi katika tafiti zao, jambo linalorudisha nyuma juhudi za kugundua tiba mpya.

Amesema,teknolojia hiyo tayari imeanza kutumika na watafiti ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, na kwa sasa inavutia taasisi mbalimbali zilizotembelea banda la UDOM katika maonesho hayo, huku baadhi ya watafiti wakionyesha nia ya kuanza kuitumia katika kazi zao.

 “Lengo letu ni kuwa na idadi kubwa ya watafiti wanaoitumia teknolojia hii ndani ya mwaka mmoja au miwili. Hii itasaidia kuharakisha upatikanaji wa tiba  kwa magonjwa sugu au yasiyo na tiba ya moja kwa moja,” aliongeza.

Uanzishaji wa ConizuroAI unatajwa kuwa hatua muhimu katika mageuzi ya tafiti za kitabibu nchini, hasa kwa kuzingatia azma ya Tanzania ya kujitegemea katika sekta ya afya na kupunguza utegemezi wa dawa kutoka nje.
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.