DCEA:Hali ya dawa za kulevya nchini yazidi kuimarika,wanaotangaza ,kuhamasisha dawa za kulevya kukiona



Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki, DAR ES SALAAM

KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas  Lyimo, amesema hali ya dawa za kulevya nchini Tanzania inaendelea kuimarika, huku matumizi na upatikanaji wa dawa hizo ukipungua kwa kiasi kikubwa kufuatia operesheni endelevu za Mamlaka hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Kamishna Lyimo alisema dawa aina ya heroin na cocaine zimepungua kwa kiwango kikubwa na sasa hazipatikani kwa urahisi hata katika vijiwe ambavyo awali vilikuwa vimeathirika zaidi.

“Hali hii ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali, ikiwemo kuwapeleka waraibu waliokuwa wameathirika katika vituo vya tiba kwa ajili ya kupata matibabu, ambayo yanatolewa bure kote nchini,” alisema Kamishna Jenerali Lyimo.

Aidha , Kamishna Jenerali Lyimo alisema Mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaofika kwenye Banda lao na kupewa Elimu kuhusu aina mbalimbali za dawa za kulevya pamoja na athari zake, sambamba na kuwaeleza wananchi kuhusu sheria zinazohusiana na matumizi, usambazaji na biashara ya dawa hizo haramu.

Aidha, alieleza kuwa DCEA ipo katika operesheni maalum ya kutoa elimu katika ngazi zote za elimu  kutoka shule za msingi, sekondari hadi vyuo kwa lengo la kuwakinga vijana na vishawishi vya kujiingiza kwenye matumizi au biashara ya dawa za kulevya.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa ndani ya kipindi kifupi, tatizo la dawa za kulevya linatokomezwa kabisa nchini, na kila mwananchi anakuwa na uelewa wa kutosha juu ya madhara na athari za dawa hizo,” alisema.

Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya bora ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Akitangaza msimamo mkali wa Serikali, alisema wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya hawatasalimika huku akisema hakuna namna watakuwa salama.

 “Mkono wa chuma utawafikia, na pumzi ya moto itawaelekea.”alisisitiza

Vilevile, aliwaonya watu wote wanaotangaza, kusifia au kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya kupitia mavazi, nyimbo au njia nyingine yoyote, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha  alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto wao na kuwafundisha madhara ya dawa za kulevya, ili kujenga kizazi bora na kuimarisha uchumi wa Taifa kwa msingi wa rasilimali watu wenye afya na maadili.

Maonesho ya 49 ya Sabasaba yanaendelea kuvutia maelfu ya wananchi, huku DCEA ikiendelea kutumia jukwaa hilo kutoa elimu, hamasa na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.