INEC YAHIMIZA viongozi wa siasa kufanya kampeni za kistaarabu

Published from Blogger Prime Android App


Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) , imekutana na viongozi wa vyama vya siasa  kwa lengo la kujadiliana kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kubadilishana uzoefu, na kujenga uelewa wa pamoja wa mchakato wa uchaguzi.

Akizungumza jijini Dodoma leo Julai 27,2025 katika Makao Makuu ya INEC  na viongozi wa vyama vya siasa nchini,Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, amesema kikao hicho kinalenga kuwapa wadau taarifa rasmi kuhusu maandalizi ya uchaguzi, na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia ratiba rasmi na masharti ya kisheria, hususan wakati wa utoaji wa fomu na uteuzi wa wagombea.

Jaji Mwambegele alieleza kuwa Tume itazingatia Katiba, Sheria na Kanuni ili kuhakikisha kila mgombea mwenye sifa anapata haki ya kuteuliwa kwa kufuata utaratibu. Aidha, alivitaka vyama vya siasa kuendesha kampeni kwa amani na ustaarabu, akionya kuwa joto la kisiasa lisiposimamiwa linaweza kuhatarisha utulivu wa nchi.

Ameongeza kuwa Tume italinda usawa kwa vyama vyote kwa kuhakikisha kila chama kinapata fursa ya kunadi sera zake kwa mujibu wa ratiba rasmi.

Katika kuelekea uchaguzi huo, ametaja kuwa kutakuwa na jumla ya majimbo 272 ya uchaguzi, ambapo 222 yako Tanzania Bara na 50 Zanzibar, baada ya kuongezwa majimbo nane mapya Bara. Vilevile, kata zitakazoshiriki uchaguzi wa madiwani zimefikia 3,960 baada ya kuongezeka kwa kata tano mpya zilizoundwa na TAMISEMI.

Kwa mujibu wa ratiba, kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28 kwa Tanzania Bara, na hadi Oktoba 27 kwa Zanzibar. Katika kipindi hicho, wagombea na vyama vyao watatumia fursa hiyo kueleza sera na ilani kwa wananchi.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima, amesema maandalizi ya vifaa vya uchaguzi yanaendelea vizuri, na kwamba Tume imeweka utaratibu utakaowezesha wapiga kura waliotoa taarifa mapema kupiga kura ya urais katika vituo tofauti na walivyojiandikisha, ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki ya kupiga kura.
Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.