TMDA yaendelea kuhakikisha Usalama wa Dawa Sokoni — Mkurugenzi Mkuu



Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

 
MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA), Dkt. Adam Fimbo, amesema kuwa TMDA inaendelea kuhakikisha kuwa dawa zinazosambazwa na kutumiwa na wananchi nchini ni salama, zenye ubora unaokubalika na zinafanya kazi iliyokusudiwa bila kusababisha madhara kwa binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3,2025  katika Banda la TMDA kwenye Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Dkt. Fimbo alisema moja ya majukumu makuu ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa kila dawa inayotumiwa na binadamu haimdhuru, bali inamponya kwa mujibu wa madhumuni ya matumizi yake.

 “Dawa yoyote inayotumiwa na binadamu haipaswi kumdhuru, Jukumu letu kama TMDA ni kuhakikisha dawa hiyo inafanya kazi iliyokusudiwa , yaani inatibu, siyo kuleta madhara,” alisisitiza Dkt. Fimbo.

Alieleza kuwa TMDA hufuatilia kwa ukaribu madhara yanayoweza kujitokeza kwa watumiaji wa dawa baada ya matumizi na huchukua hatua stahiki ili kuzuia madhara zaidi kwa umma.

 Aidha, alisema mamlaka hiyo imewekeza katika maabara za kisasa ambazo zimethibitishwa kimataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO), na ni miongoni mwa maabara chache zenye uwezo mkubwa wa kupima ubora wa dawa barani Afrika.

 “Tunapima bidhaa za dawa kwenye maabara zetu zilizoidhinishwa na WHO,maabara yetu ni miongoni mwa maabara Bora Afrika zenye viwango vya kinataifa"amesisitiza

Ni maabara chache za aina hii, na sisi ni miongoni mwao. Hivyo, tunaruhusu dawa tu ambazo zimekidhi viwango vilivyowekwa kimataifa,” alieleza.

Mbali na udhibiti wa dawa amesema , TMDA pia inasimamia bidhaa za tumbaku, kwa lengo la kuwalinda wananchi dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa hizo.

 Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi ya kudhibiti usambazaji na matumizi holela ya bidhaa hizo ili kuhakikisha usalama wa afya ya jamii.

 Dkt. Fimbo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na TMDA kwa kutoa taarifa za dawa au bidhaa zinazohisiwa kuwa na madhara, ili kuchukua hatua za haraka.

Aidha Fimbo ametumia nafasi hiyo kuwaasa  wananchi wote kufika katika banda hilo  kupata elimu kuhusu usalama wa dawa, vifaa tiba, na vitendanishi .

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.