Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa  Brigedia Jenerali Mstaafu Balozi Mndolwa atoa wito kwa Waandishi wa Habari kuwa Wazalendo



Published from Blogger Prime Android App




Na Joyce Kasiki

 MMOJA wa Mashujaa waliopigana vita ya Kagera Brigedia Jenerali mstaafu na Balozi Francis Mndolwa amewaasa  waandishi wa habari nchini kuandika habari zenye kuijenga jamii, kuleta heshima kwa Taifa, na kukuza uzalendo ikiwa ni sehemu ya ujenzi juhudi za mashujaa hao pamoja na waasisi wa Taifa la Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa nchini , Balozi Mndolwa aliwataka kuenzi kazi yao kama sehemu ya mchango mkubwa kwa Taifa.

"Waandishi muandike habari ambazo zitawainua na kuwaheshimisha. Waandishi wote wa habari mnapaswa kuwa wazalendo,nchi hii imetoka mbali, inahitaji msaada wa kila mmoja wenu ili tuendelee kuwa na amani.”

Balozi Mndolwa aliwakumbusha waandishi kuhusu historia ya taifa, akitaja jinsi viongozi waasisi kama Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume walivyoweka msingi wa mshikamano wa kitaifa, amani na maendeleo. 

Alisisitiza kuwa Tanzania imeweza kudumisha utulivu wa muda mrefu licha ya changamoto zinazozikumba nchi nyingi jirani.

"Nchi nyingi zinazotuzunguka zimebomoka, zimepata matatizo, lakini tuwashukuru taasisi zetu, Mwalimu Nyerere, Mzee Karume, kwa kuwaandaa wananchi ambao sasa wanaendelea na juhudi zao na nchi kuwa na amani,” amesema

Mndolwa pia alitoa wito kwa waandishi na Watanzania kwa ujumla kujiepusha na kuiga migogoro ya mataifa makubwa duniani.

"Msiwe na mwendo wa upinzani wa dunia, tunawaona Warusi, Wachina wakigombana na Marekani ,huo ni ugomvi wao wa dunia, hatuutaki. Tunataka hivi tulivyo, lazima tushirikiane,” aliongeza kwa msisitizo.

Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ni wakati wa kukumbuka na kuthamini mchango wa watetezi wa taifa waliopigania uhuru, usalama, na heshima ya nchi. 




---


Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.