
Mtoto akiwa katika banda la VETA kitengo cha ushauri
Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM
WAZAZI wameaswa kutokatiza vipaji na ndoto za watoto wao kwa kuwachapa au kuwakanya wasirudie kufanya kitu ambacho wao wanadhani ni uharibifu kumbe ndiyo kipaji Cha mtoto ambacho kinapaswa kiendelezwe.
Akizungumza Julai Mosi 2025 katika maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba katika Banda la VETA kitengo cha ushauri,Mwalimu anayefundisha somo la electronics Rick Sambo kutoka VETA amesema ,mtoto anapofanya kitu labda amevunja au amefungua radio ,ina maana anaanza kuonyesha mapema kuwa hicho ndiyo kipaji chake.
"Kwa mfano, kuna mtoto anayeonekana ni mtundu kila mara anafungua redio, pasi, au vifaa vya umeme vilivyo karibu,kwa macho ya mzazi, hilo linaweza kuonekana kama utundu au uharibifu wa mali,
" Mara nyingi, matokeo yake ni mtoto kuchapwa au kukemewa,lakini kwa macho ya VETA, hapo ndipo vipaji vinapojificha,mtoto huyo anahitaji kuelekezwa, si kukataliwa."amesema Mwalimu huyo
Amesema,kufuatia hali hiyo,katika Banda lao ,wameanzisha kitengo cha ushauri ili waweze kuwasaidia katika kugundua vipaji vya watoto na kuwaelekeza wazazi cha kufanya ili kuendeleza vipaji vya watoto hao.
"Katika banda letu, tunapokea watu wa rika mbalimbali kutoka watoto wadogo hadi watu wazima ambao hawana elimu rasmi ya ufundi lakini wana vipaji vya asili,
"Na kwa sababu watoto wengi wanakuwa wameshasoma mambo mengi kwa nadharia,wakifika hapa tunawaonyesha vifaa vya umeme na electronics na kuwapa ushauri kuhusu namna ya kuanza kujifunza taaluma hizo kwa usahihi na usalama."amesisitiza Mwalimu huyo
Vile vile amewaasa wazazi kuangalia nini mtoto anahitaji kusoma ili mtoto asipoteze muda kwa kusomea kitu ambacho anakitaka mzazi.
"Unakuta mtoto anahitaji kusomea fani Fulani,lakini mzazi hataki hiyo anataka mwanae asomee kitu kingine kabisa na anachotaka mtoto,sasa wazazi kama hao wakifika kwenye Banda letu wakiwa na watoto wao tunawashauri na mambo ya naenda sawa." amesisitiza na kuongeza
" Kwa hiyo tunawaleta wazazi na watoto pamoja ili kuwasaidia kuelewana mzazi asikilize ndoto ya mtoto, na mtoto apewe mwongozo wa kitaaluma. Kwa kufanya hivyo, tunamjenga mtoto kuwa mtaalamu bora wa baadaye
No comments:
Post a Comment