MAENDELEO YA TRILIONI 5.6 YABADILI SURA YA MWANZA




Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dodoma


MKOA wa Mwanza umeendelea kung’ara kimaendeleo baada ya kupokea zaidi ya Shilingi trilioni 5.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kuanzia Novemba 2020 hadi Aprili 2025.

Akizungumza jana jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mkuu wa mkoa huo Said Mtanda alisema fedha hizo zimetumika katika sekta muhimu zikiwemo afya, elimu, maji, miundombinu, usafirishaji, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi pamoja na kuimarisha sekta ya utalii na biashara, na hivyo kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi.

Afya na Elimu zilivyoimarika

Alisema,katika kipindi hicho, Serikali imetoa jumla ya Shilingi bilioni  63.2 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya na shilingi bilioni 196.8 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu. 

Mtanda alisema Uboreshaji wa miundombinu ya shule na vituo vya afya umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani, kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya na kuongeza ari ya walimu na wanafunzi shuleni.

Aidha, ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vituo vya afya umechangia kupunguza umbali kwa wanafunzi na wagonjwa wanaotafuta huduma muhimu, hali iliyoboresha kwa kiasi kikubwa ustawi wa wananchi.

Huduma ya maji ntafikia vyuo,vijiji na majumbani

Katika eneo hilo alisema,moka umepiga   hatua kubwa ambapo jumla ya Shilingi bilioni 264.8 zimetumika kuongeza upatikanaji wa maji mijini na vijijini. 

"Takwimu zinaonesha huduma ya maji mijini imeongezeka kutoka asilimia 57 mwaka 2020 hadi asilimia 85 mwaka 2025, huku vijijini ikiongezeka hadi asilimia 77.8."alisema na kuongeza kuwa 

"Mradi mkubwa wa ujenzi wa chanzo na kituo cha kutibu maji cha Butimba umegharimu Shilingi bilioni 71.6 na kuzalisha lita milioni 48 za maji kwa siku."

Alisema mradi huo unatarajiwa kupunguza tatizo la uhaba wa maji katika maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Igoma, Buhongwa na Kisesa.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.