Baba Levo Atoa Hamasa Banda la TTCL Maonesho ya Sabasaba



Published from Blogger Prime Android App




Na Mwandishi Wetu

MSANII na mtangazaji maarufu nchini, ambaye pia ni Balozi wa Kampeni ya Walete inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, ametembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Baba Levo alitumia fursa ya kuzungumza na wateja wa TTCL, kuhamasisha matumizi ya huduma za shirika hilo, pamoja na kueleza mchango wa TTCL katika kuleta mapinduzi ya kidijitali nchini. Aidha, alitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa juhudi zake katika kuhakikisha shirika hilo linaendelea kuwa mhimili mkuu wa mawasiliano nchini.

Akizungumza akiwa katika banda hilo, Baba Levo alisema "TTCL ni alama ya taifa. Tunapaswa kujivunia kuwa na taasisi ya kizalendo inayohakikisha mawasiliano ya Watanzania yanakuwa salama, ya uhakika na ya gharama nafuu.”


Pia aliwapongeza wataalamu wa TTCL kwa mafanikio ya kiteknolojia waliopiga hatua nayo, ikiwemo usambazaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kuanzishwa kwa Kituo cha Kuhifadhi Data Kimtandao (Data Center), utoaji wa huduma za intaneti ya kasi, huduma za simu pamoja na bidhaa za kisasa kama vile modemu, MiFi, na huduma ya faiba mlangoni inayowezesha matumizi ya teknolojia ya kisasa majumbani.

Ziara hiyo ya Baba Levo ilivutia umati mkubwa wa wananchi na mashabiki, waliokusanyika kwa wingi kushuhudia msanii huyo akishirikiana na watumishi wa TTCL kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali za shirika hilo la kihistoria.

Kwa upande wake, Meneja wa Banda la TTCL ambaye pia ni Meneja wa Bidhaa, Bi. Janeth Maeda, alisema ujio wa Baba Levo ni ishara ya ushirikiano mzuri kati ya taasisi za umma na watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii.

"Tunamshukuru Baba Levo kwa kutenga muda wake kututembelea. Hii ni ishara kuwa jamii inatambua umuhimu wa TTCL kama taasisi ya umma inayotekeleza dhamira ya Serikali ya kuwafikishia Watanzania wote huduma za mawasiliano,” alisema Bi. Maeda.



Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.