
Na Joyce Kasiki ,Dar Es Salaam
MENEJA Masoko na Muhamasishaji Mkuu wa Mfuko wa mikopo wa SELF Linda Mshana amewaasa watanzania wachangamkia fursa za mikopo hasa ya Nishati mbadala inatolewa na mfuko huo.umetua rasmi kuwatangazia Watanzania habari njema kuhusu fursa mpya zilizopo katika banda lao.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la mfuko huo lililopo kwenye banda kubwa la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 49 yanayoendelea jijini Dar Es Salaam,Linda amesema SELF wamekuja na huduma na bidhaa mpya zinazolenga kumkomboa Mtanzania wa kawaida na kumuwezesha kiuchumi kupitia mikopo nafuu, elimu ya fedha, na bima kwa ajili ya biashara na maisha.
"Katika maonesho haya, SELF tumekuja na mikopo mipya ya 2025 inayolenga kuchochea maendeleo endelevu na kuwaunganisha Watanzania wote kwenye masuala ya kifedha ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla"amesema Mshana
Amesema mikopo mipya inayotolewa na SELF ni pamoja na mkopo ya Nishati Mbadala kwa wajasiriamali wanaojihusisha na uuzaji wa bidhaa za sola, gesi, na teknolojia mbadala ya kuni na mkaa ambapo amesema,mfuko huo utapunguza riba kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo, ili kuhakikisha biashara zao zinakua na mazingira yanatunzwa kwa kizazi kijacho.
"Tumekuja Sabasaba kuwahamasisha Watanzania wachangamkie fursa hizi mpya,kama unafanya biashara ya sola, gesi, au bidhaa mbadala ya kuni na mkaa hii ni fursa yako,SELF tuko tayari kushika mkono wako na kukuinua kiuchumi,” amesema Linda
Vile vile.amesema ipo mikopo ya Vikundi kwa watu walioungana na kusajili kikundi chao rasmi, SELF wanatoa mikopo kwa ajili ya shughuli za pamoja za uzalishaji mali huku akisema ni nafasi ya kipekee kwa watu wasio na duka au sehemu rasmi ya biashara, lakini wenye nia ya pamoja ya kujiendeleza.
Pia amezungumzia mikopo ya Kuboresha Makazi ya Wafanyakazi ambapo amesema,kwa wafanyakazi wanaotaka kuishi maisha bora zaidi, SELF wanatoa mkopo wa kuboresha makazi yao .
Pia amesema ipo mikopo ya Biashara na Ujasiriamali kwa wafanyabiashara ambapo SELF wanatoa mikopo rafiki kwa ajili ya kukuza mitaji, kuongeza uzalishaji, na kufanikisha ndoto za kimaendeleo.
Katika hatua nyingine amesema pia katika maonyesho hayo wanatoa elimu ya fedha na Biashara pamoja na elimu ya bima.
"Kwa wale wanaohitaji msaada wa kitaalamu kuhusu kuandaa bajeti, kusimamia biashara, au kupanga malengo ya kifedha, SELF wametenga sehemu maalum ya ushauri na elimu ndani ya banda lao. Huduma hizi zitatolewa bure kwa wote watakaotembelea,
"SELF pia wanajali ustawi wa biashara na maisha ya Watanzania. Kupitia bima mbalimbali tunazozitoa, tunahakikisha kwamba mali, afya na biashara za wananchi zinalindwa dhidi ya majanga yasiyotegemewa."amesema na kuongeza kuwa
Maonesho haya yanatoa nafasi ya kipekee kwa kila Mtanzania kufika, kujifunza na kuchukua hatua. SELF wanawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kujionea mikopo na huduma mbalimbali zilizobuniwa kwa ajili ya maendeleo ya watu wote hata wale waliokuwa wametengwa na mifumo ya kifedha ya awali.
No comments:
Post a Comment