
Na Mwandishi wetu DODOMA
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imezindua rasmi kalenda ya uchaguzi Mkuu huku ikitangaza ongezeko kubwa la idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ikiwa ni matokeo ya mafanikio ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya Uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele, amesema jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ni milioni 37.655 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.55% kutoka wapiga kura milioni 29.754 waliokuwepo mwaka 2020.
“Kati ya hao milioni 36.650 ni kutoka Tanzania Bara, huku Zanzibar ikiwa na wapiga kura milioni 1.0 Idadi hii inaonesha mwitikio chanya wa wananchi kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia,” amesema Jaji Mwambegele.
Kwa upande wa Zanzibar, ilielezwa kuwa wapiga kura 725,876 wako katika Daftari la ZEC, huku wengine 278,751 wakiwa wameandikishwa na INEC baada ya kukosa sifa za kujiandikisha kupitia ZEC.
Ratiba ya Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa mujibu wa mamlaka ya kikatiba na kisheria chini ya ibara ya 41(4) ya Katiba ya 1977, pamoja na Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya 2024, INEC imetangaza ratiba rasmi ya uchaguzi ambapo Agost 9 - 27, 2025 ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais,Agosti 14 - 27, 2025 ni utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa Ubunge na Udiwani.
Agosti 27 , 2025 ni siku ya Uteuzi wa wagombea wa nafasi zote,Agosti 28 hadi Oktoba 28 , 2025 ni kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Bara,Agosti hadi Ojtoba 27 , 2025 ni Kampeni za Uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema na Oktoba 29, 2025 (Jumatano) itakuwa ni Siku rasmi ya Kupiga Kura.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima amekabidhi rasmi orodha ya watu 8,703 waliojiandikisha zaidi ya mara moja kwa Jeshi la Polisi.
Taarifa hiyo ni sehemu ya kalenda ya uchaguzi, na hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa mujibu wa Kifungu 114 cha Sheria ya Uchaguzi, ambacho kinaainisha adhabu kwa makosa hayo.
Ametoa wito kwa wananchi na wadau wote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo, na maelekezo yatakayotolewa na Tume katika kipindi chote kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.







No comments:
Post a Comment