DCEA:Hali ya dawa za kulevya nchini yazidi kuimarika,wanaotangaza ,kuhamasisha dawa za kulevya kukiona



Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki, DAR ES SALAAM

KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas  Lyimo, amesema hali ya dawa za kulevya nchini Tanzania inaendelea kuimarika, huku matumizi na upatikanaji wa dawa hizo ukipungua kwa kiasi kikubwa kufuatia operesheni endelevu za Mamlaka hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Kamishna Lyimo alisema dawa aina ya heroin na cocaine zimepungua kwa kiwango kikubwa na sasa hazipatikani kwa urahisi hata katika vijiwe ambavyo awali vilikuwa vimeathirika zaidi.

“Hali hii ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali, ikiwemo kuwapeleka waraibu waliokuwa wameathirika katika vituo vya tiba kwa ajili ya kupata matibabu, ambayo yanatolewa bure kote nchini,” alisema Kamishna Jenerali Lyimo.

Aidha , Kamishna Jenerali Lyimo alisema Mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaofika kwenye Banda lao na kupewa Elimu kuhusu aina mbalimbali za dawa za kulevya pamoja na athari zake, sambamba na kuwaeleza wananchi kuhusu sheria zinazohusiana na matumizi, usambazaji na biashara ya dawa hizo haramu.

Aidha, alieleza kuwa DCEA ipo katika operesheni maalum ya kutoa elimu katika ngazi zote za elimu  kutoka shule za msingi, sekondari hadi vyuo kwa lengo la kuwakinga vijana na vishawishi vya kujiingiza kwenye matumizi au biashara ya dawa za kulevya.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa ndani ya kipindi kifupi, tatizo la dawa za kulevya linatokomezwa kabisa nchini, na kila mwananchi anakuwa na uelewa wa kutosha juu ya madhara na athari za dawa hizo,” alisema.

Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya bora ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.

Akitangaza msimamo mkali wa Serikali, alisema wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya hawatasalimika huku akisema hakuna namna watakuwa salama.

 “Mkono wa chuma utawafikia, na pumzi ya moto itawaelekea.”alisisitiza

Vilevile, aliwaonya watu wote wanaotangaza, kusifia au kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya kupitia mavazi, nyimbo au njia nyingine yoyote, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha  alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto wao na kuwafundisha madhara ya dawa za kulevya, ili kujenga kizazi bora na kuimarisha uchumi wa Taifa kwa msingi wa rasilimali watu wenye afya na maadili.

Maonesho ya 49 ya Sabasaba yanaendelea kuvutia maelfu ya wananchi, huku DCEA ikiendelea kutumia jukwaa hilo kutoa elimu, hamasa na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
Share:

Mfumo Mpya wa Kudhibiti Umeme Nyumbani Watengenezwa na Wanafunzi wa NIT




Published from Blogger Prime Android App


 

Na Joyce Kasiki,Dar es Salaam

 

WANAFUNZI  wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wameibuka na ubunifu wa kipekee kwa kutengeneza mfumo wa kisasa wa kudhibiti matumizi ya umeme majumbani, unaotumia teknolojia ya mawasiliano bila waya. 

 

Mfumo huo, uliopewa jina la Smart Home ulioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo, Sayuni Haule, mwalimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), alisema kuwa mfumo huo umetengenezwa na wanafunzi wake kama sehemu ya mazoezi ya vitendo yanayolenga kutafsiri elimu ya darasani kwenda kwenye maisha halisi.

 

 Alisema kuwa mfumo huo ni mfano wa awali (prototype) unaoonesha jinsi teknolojia rahisi inaweza kutatua changamoto za kila siku za matumizi ya nishati majumbani.

 

“Kwa kutumia mfumo huu, mtu anaweza kuwasha au kuzima taa, feni na vifaa vingine vya umeme akiwa mbali na nyumbani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano isiyotumia waya,” alisema Mwalimu Haule,

 

“Mfano, mtu anaweza kuwa kazini au safarini na akagundua kuwa alisahau kuzima taa  kwa kutumia mfumo huu, anaweza kuzima taa hizo kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) bila ya kurudi nyumbani.”

 

Mwalimu Haule aliongeza kuwa mfumo huu unaleta urahisi  kwa watumiaji kwa kuwa unamwezesha mtu kuwa na udhibiti wa vifaa vya umeme popote alipo lakini pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye ulemavu wa viungo kwani huwapa uwezo wa kuendesha mifumo ya nyumbani bila kulazimika kwenda moja kwa moja kwenye swichi.

 

Mbali na kuongeza urahisi,  amesema mfumo huu pia unasaidia kudhibiti matumizi ya umeme na kupunguza gharama. “Kwa mfano, unaweza ‘kufunga’ (lock) mfumo fulani wa umeme ambao hautaki utumike kwa muda husika,umeme utakuwepo lakini hautatumika hadi ufungue tena mfumo huo,” aliongeza.

 

Mradi huu unaonesha uwezo mkubwa wa wanafunzi wa NIT katika kuoanisha elimu na mahitaji halisi ya jamii. ni ishara njema kwa mustakabali wa teknolojia ya ndani ya nchi na inatoa matumaini ya maendeleo ya kiteknolojia yanayoendana na mazingira ya Kitanzania






Share:

FCC yatoa elimu ya ushindani wa kibiashara, Yazindua 'Clinic' ya Biashara kwa ushauri wa faragha



Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Ushindani wa Kibiashara (FCC) imetumia fursa ya maonesho ya biashara kufikisha elimu kwa wadau wa sekta ya biashara huku ikizindua 'clinic' maalum ya kutoa ushauri wa faragha kwa wafanyabiashara kuhusu masuala ya ushindani na ulinzi wa walaji.

Akizungumza katika maonesho hayo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Hadija Ngasongwa, alisema kuwa jukwaa hilo limewawezesha kufikia zaidi ya washiriki 3,500 kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha ushindani wenye tija na kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

“FCC imeanzisha clinic ya biashara ili kutoa nafasi kwa wafanyabiashara hasa wadogo na wa kati  kupata maarifa sahihi kuhusu sheria za ushindani na haki za walaji, kwa faragha na usiri unaohitajika,” alisema Bi. Ngasongwa.

Aliongeza kuwa pamoja na kuelimisha umma, FCC inaendelea kufuatilia mwenendo wa soko na kudhibiti bidhaa bandia ambazo si tu zinahatarisha afya za walaji, bali pia zinaharibu ushindani halali katika biashara.

Ngasongwa alieleza kuwa Serikali kupitia FCC imejenga mazingira rafiki ya kufanyia biashara, hali ambayo inaendelea kuwavutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

 “Sheria zetu ni rafiki kwa wawekezaji, na tunajivunia kwamba Serikali imeimarisha zaidi mazingira ya biashara, jambo linalochochea ukuaji wa uchumi na uwekezaji,” alisisitiza

Alifafanua kuwa FCC inaendelea kufanya tafiti za soko zenye lengo la kuhakikisha uwiano wa ushindani unazingatiwa, pamoja na kusaidia biashara ndogo kukua hadi kufikia viwango vya juu vya ushindani.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha kuwa siyo tu wawekezaji wa nje wanafaidika na mazingira mazuri ya biashara, bali pia wajasiriamali wa ndani wanapata nafasi ya kukuza mitaji yao kupitia ushindani wa haki,” alieleza

Maonesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu kati ya wadau wa biashara na taasisi mbalimbali, huku FCC ikichukua hatua za makusudi kuwa karibu zaidi na wafanyabiashara kwa njia ya ushauri wa moja kwa moja na elimu ya kisheria.

Share:

REA yawataka watanzania kuachana na dhana potofu kuhusu gharama za nishati safi ya kupikia



Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

 WAKALA  wa Nishati Vijijini (REA) umewahimiza Watanzania kote nchini kuondokana na mtazamo potofu kwamba matumizi ya nishati safi ya kupikia ni gharama kubwa ukilinganisha na kuni au mkaa, akisisitiza kuwa teknolojia ya kisasa imepunguza sana gharama hizo.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam, katika banda la REA.

“Kumekuwepo na dhana kwamba kutumia nishati safi ya kupikia kama vile umeme ni gharama kubwa ikilinganishwa na kutumia kuni au mkaa. Hii si kweli. Teknolojia imebadilika sana sasa; kuna majiko ya kisasa yanayotumia umeme kwa kiwango kidogo sana,” alisema Mhandisi Olotu.

Aliwataka wananchi kutembelea banda la REA ili kujionea kwa macho jinsi teknolojia hizo zinavyofanya kazi na kuona jinsi upishi kwa kutumia nishati safi unavyowezekana bila kupoteza ladha ya chakula, huku muda wa kupika ukiwa mfupi zaidi.

Akizungumzia juhudi za REA katika kuhamasisha na kuwawezesha waendelezaji wa teknolojia za nishati safi ya kupikia, Mhandisi Olotu alieleza kuwa lengo ni kuwawezesha Watanzania kubadili mtindo wa maisha na kulinda afya zao pamoja na mazingira.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Afya, watu takribani 33,000 hufariki kila mwaka kutokana na athari za matumizi ya nishati chafu ya kupikia. Mhandisi Olotu alisisitiza kuwa REA ni miongoni mwa wadau wakuu wanaojitahidi kupunguza idadi hiyo kwa kutoa elimu na kuwapatia wananchi mbinu mbadala salama.

“Dhamira yetu ni kuachana kabisa na matumizi ya kuni na mkaa, lakini tunatambua kuwa mabadiliko haya hayawezi kufanyika kwa mara moja. Ndiyo maana tumekuwa tukisambaza majiko ya kisasa yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa au kuni kama njia ya mpito,” alieleza.

Katika hatua za awali, REA imeanza kusambaza majiko ya gesi yenye mitungi ya kilo 6. Hadi sasa, jumla ya mitungi 3,255 pamoja na vichomeo vyake vimegawiwa katika kila wilaya Tanzania Bara kwa ruzuku ya asilimia 50, huku zoezi hilo likiendelea.

“Tunalenga kumwezesha kila Mtanzania kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati hatarishi kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia. Kwa wale wanaohitaji muda kubadilika, tumeanzisha suluhisho la mpito kwa kutumia teknolojia ya majiko yanayotumia mkaa kidogo,” aliongeza.

Aidha, alieleza kuwa REA inatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuzitaka taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia.

“Tumeanza utekelezaji katika taasisi mbalimbali, zikiwemo Jeshi la Magereza. Mpaka sasa, maeneo 211 yameshafikiwa yakiwemo magereza 129, kambi 47, ofisi za mikoa 26, pamoja na nyumba za watumishi, vyuo, shule na hospitali,” alisema.

Nishati safi zinazotumika katika taasisi hizo ni pamoja na bayogesi, gesi ya mitungi (LPG), gesi asilia, mkaa kutoka makaa ya mawe, pamoja na mashine za kutengeneza mkaa mbadala. Vilevile, REA imewajengea uwezo Maafisa wa Magereza 280 kuhusu matumizi bora ya nishati safi.

Kwa ujumla, REA inaendelea kutoa elimu na kuwezesha upatikanaji wa teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanahama kutoka matumizi ya nishati chafu kuelekea kwenye mfumo wa upishi salama, rafiki kwa afya na mazingira.


.


Share:

*SADC: SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI*



Published from Blogger Prime Android App



📌 *Yasisitiza utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya Nishati*

📌 *Kapinga ataka SADC kuweka dhamira thabiti na mikakati madhubuti ya utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia*

Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wametaka Sekta ya Nishati kuwa kichocheo cha kuiunganisha Afrika katika kujenga uchumi wake.

Wamesema hayo leo Julai 4, 2025  wakati wakihitimisha mkutano wa SADC jijini Harare nchini Zimbabwe ambao ulilenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji.

Akizungumza wakati akihitimisha mkutano huo, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Umeme wa Zimbabwe, Mhe. Dkt. July Moyo, ameitaka jumuiya hiyo ya SADC kuipa kipaumbele sekta ya nishati na maji ili kuifanya kuwa na tija kwa wananchi katika kukuza uchumi wao kwa kuwa nishati  ni chanzo kikubwa cha maendeleo. 

Aidha, ameipongeza Tanzania kwa kuandaa na kuwa mwenyeji wa kufanikisha Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Nishati Afrika wa Misheni 300 (M300) ambao ulifanyika kwa mafanikio. Pia, Dkt. Moyo amezishukuru Nchi wanachama zilizohudhuria katika mkutano huo muhimu uliofanyika jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Malawi, Mhe. Ibrahim Matola ameitaka SADC kuhakikisha inaiendeleza miradi yote ya kipaumbele katika jumuiya ili kuifanya sekta ya nishati kuwa kimbilio katika kujenga uchumi wa nchi zao. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameitaka SADC kuhakikisha inakuwa na mikakati madhubuti ya utekekezaji wa maazimio mbalimbali wanayofikia  katika makongamano ya umoja huo ili yawe na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na kuifanya sekta ya nishati kuwa chachu na mkombozi ndani ya SADC. 

Kuhusu utekelezaji wa nishati safi ya kupikia katika jumuiya hiyo, Mhe. Kapinga ameitaka SADC kuweka dhamira thabiti na mikakati madhubuti ya utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kuwafikia watu wengi zaidi katika SADC. 

Mkutano huo uliohitimishwa leo, umehudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan Kaganda, Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati akiwemo Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa  Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na  Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Share:

Waziri Ridhiwani Atoa Wito kwa Vijana Kuchangamkia Fursa Zilizopo

Published from Blogger Prime Android App


 
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam.

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mikopo na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji
Wananchi kiuchumi.


Mhe. Kikwete ametoa wito huo wakati alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuuu lililopo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa SABASABA, leo tarehe 04 Julai, 2025 Jijini Dar es Salaam.
 

“Serikali imeendelea kutenga fedha kuhakikisha makundi mbalimbali yananufaika, kwa mfano kupitia maelekezo ya kisera kwenye Sheria ya PPRA imeelekezwa asilimia 30  ya manunuzi yote ya umma ipelekwe katika kusaidia makundi ya Vijana, akinamama na Wenye Ulemavu," ameeleza Mhe. Ridhiwani.

 
Aidha, ameongeza kuwa upo mfuko maalumu wa kusaidia watu wenye ulemavu,  lakini pia upo mfuko wa vijana na mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, hivyo mifuko yote hiyo kama vijana na  wananchi  wakiikimbilia hakika vilio vya uwezeshaji havitaweza kutokea.
 
 
Pia, Mhe. Kikwete amewata Waandishi wa Habari, Watumishi wa Umma na wadau mbalimbali kuzidi kupaza sauti juu ya uwepo wa mifuko hiyo na faida zake kwa wananchi .


Vilevile, ameelekeza Idara na Taasisi za serikali ziendelee kutoa elimu kwa wananchi hususani Vijana ili waweze kujua fursa za mikopo na uwezeshaji wananchi zilizopo.


“Maelekezo yetu ni kwamba Idara zetu zote, taasisi zetu zote waendelee kuhakikisha kwamba elimu inakuwa ndiyo kipaumbele kwa sababu serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mambo yaliyofanyika ni uwezeshaji wa kifedha, uwezeshaji wa watu, uwezeshaji wa kielimu, tumefanya mambo mengi sana na tumehakikisha watu wetu wanapatiwa elimu ili waweze kujinusuru katika maeneo haya” amebainisha Mhe. Ridhiwani.


Mbali na hayo Mhe. Ridhiwani amewataka Watanzania na hasa kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika Uchaguzi Mkuu kulinda amani iliyopo ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.


=MWISHO=

Share:

PSPTB yatangaza Usajili wa Mitihani ya 31,wadau waombwa kujisajili mapema


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Picha zote zinaonesha wajumne wa Bodi ya PSPTB wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara kwenye banda la PSPTB 




Na Mwandishi wetu

BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi kuanza kwa usajili wa mitihani yake ya kitaaluma ya 31, itakayofanyika kuanzia Agosti 25 hadi Agosti 29, 2025, katika kituo maalum kilichopo jijini Dodoma.

Akizungumza Leo Julai 4,2025 na waandishi wa habari  katika Maonyesho ya Kimataifa ya 49 ya  Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB,  Godfred Mbanyi, amewahimiza   waombaji wote wenye sifa  kujisajili kupitia mfumo wa mtandaoni unaopatikana kwa anuani https://registration.psptb.go.tz.

"Tunapenda kuwafahamisha wadau wetu kuwa usajili wa mitihani ya 31 umefunguliwa rasmi,tunawasihi wale wote wanaokusudia kufanya mitihani hii wajisajili mapema kabla ya tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ambayo ni Agosti 15, 2025," amesema Mbanyi.

Kwa mujibu wa Mbanyi , kwa sasa mitihani hiyo itafanyika katika kituo kimoja tu Dodoma  ili kuimarisha uratibu na kuhakikisha usimamizi bora wa mitihani hiyo muhimu kwa taaluma ya ununuzi na ugavi nchini.

Aidha Mkurugenzi huyo,   amewaasa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu kwa kuwasomesha na kuwafadhili watoto wao walioko kwenye nyanja ya ununuzi na ugavi, kwa kuhakikisha wanalipiwa ada za usajili wa mitihani hiyo.

"Natoa rai kwa wazazi na walezi kuchangia katika maendeleo ya taaluma hii kwa kuwalipia ada watoto wao,hatua hiyo ni uwekezaji muhimu katika kukuza rasilimali watu yenye weledi na uadilifu," aliongeza.

Aidha, Mkurugenzi huyo amewataka wadau wote wa PSPTB nchini kote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uzalendo kwa manufaa ya Taifa, akisema kuwa taaluma ya ununuzi na ugavi ni mhimili muhimu katika usimamizi wa rasilimali za umma na sekta binafsi.

Kwa mujibu wa PSPTB, mitihani hiyo ya kitaaluma ni sehemu ya mfumo wa kutoa ithibati kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi, ambao wana mchango mkubwa katika kudhibiti matumizi ya fedha na kuhakikisha thamani halisi ya manunuzi kwa taasisi mbalimbali nchini.



Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.