|
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima |
|
JOYCE KASIKI,DODOMA
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na
Makundi Dkt.Dorothy Gwajima amesema,matukio mengi ya ukatili yanayojitokeza
hivi sasa hapa nchini huenda ni kutokana
na jamii kukosa elimu sahihi ya malezi na makuzi walipokuwa watoto.
Akifungua
mafunzo ya Sayansi ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (SECD) jijini Dodoma yaliyokutanisha washiriki 79
kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini Dkt.Gwajima amesema kupitia mafunzo hayo
sasa yaende kubadilisha jamii katika vizazi vijavyo.
“Hivi sasa upo ukatili mwingi kwenye jamii kutokana
na sababu mbalimbali pia ni sehemu na yatokanayo na jinsi gani ambavyo
tuliwalea watoto wetu katika hatua za awali ikibidi tangu walipokuwa tumboni
mpaka wanazaliwa.”amesema Dkt.Gwajima na kuongeza kuwa
“Tunaambiwa
kitaalam kuwa katika hatua ambzo ubongo wa mtoto unakua kwa asilimia 70 ni
kwenye miaka ya awali.”
Amesema,kutokana na mafunzo hayo ya kuwajengea
uwezo makundi mbalimbali juu ya sayansi ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto
nchi inakuja kuwa na kizazi ambacho hakina changamoto zinazoonekana hivi sasa
zikiwemo za matukio ya ukatili.
Dkt.Gwajima amesema,hatua ambazo hazikuchukuliwa
katika malezi na makuzi ya watoto katika vipindi vya huko vinasababisha nchi
kuchukua muda mwingi na gharama katika kupambana na matukio ya ukatili ambayo
kwa namna ama nyingine inarudisha nyuma amendeleo ya nchi.
“Changamoto hizi tunazoziona sasa hivi na
tunachukua muda mwingi sana kupambana nazo, ambazo kwa namna moja ama nyingine
zinarudisha maendeleo nyuma,ni dhahiri hatua za malezi na makuiz zinazoanza
kuchukuliwa hivi sasa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Programu Jumuishi ya
Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto,zitaifanya nchi kuwa na
kizazi ambacho kikiambiwa hiki siyo kitaelewa kwa urahisi pasipo kutumia nguvu
nyingi sana.”
|
Waandishi wa habari vinara wa masuala ya Malezi ,Makuiz na Maendeleo ya Awali ya Mtoto wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Doropthy Gwajima
|
Waziri huyo ameushukuru Mtandao wa Malezi na Makuzi
ya Watoto (TECDEN),Shirika lisilo la Kiserikali la Malezi,Makuzi na Maendeleo
ya Awali ya Mtoto (CIC) Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC) kupitia utekelezaji wao wa mradi wa ‘Mtoto Kwanza’
na kufanikisha kuwezesha wadau wengi kukutana na kupata mafunzo ya malezi na
makuzi ya watoto wadogo kwa ajili ya kwenda kutoa elimu hiyo kwa jamii.
Vile viule ameishukuru Taasisi ya Agha Khan
Development Network kwa kushiriki tangu uzinduzi wa Programu na mpaka sasa
wameendelea katika utekelezaji wake.
“Serikali inatambua kwamba mafunzo haya ni fursa
kubwa ya kipekee ya kuelekea kwenye kundi kubwa la wataalam watakaokuwa na
ujuzi wa kutosha kwenye PJT MMMAM ,
“Ni imani yangu kubwa baada ya mafunzo haya
tutapata watendaji wengi zaidi katika ngazi mbalimbali wenye utaalam wa sayansi
ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto watakaoenda kuelimisha jamii
ili ijue kwamba akikosea malezi katika umri wa awali anaweza kumpata mtoto
ambaye siyo matarajio yake.”amesisitiza
Aidha Dkt.Gwajima amesema kupitia mafunzo hayo ushirikiano
wa serikali na wadau wengine katika utekeleaji wa programu ya MMMAM utaimarika.
Vile vile amewapongeza waandishi vinara kwa kutoa
machapisho zaidi ya 400 tangu programu hiyo ilipozinduliwa mwezi Disemba mwaka
jana yenye lengo la kuelimisha jamii kuhusu suala zima la malezi na makuzi ya
watoto wadogo huku akisema kupitia mafunzo hayo waandishi wataenda kuchapisha
machapisho mengi zaidi na yenye ubora zaidi utakaoamsha ari ya wananchi katika
malezi ya watoto wao.
“Kwa hiyo tutakuwa tunafuatilia na pengine
mnaposema ‘score card’ hii iwepo hadi kwa wanahabari ilituwapate wanahabari
wazuri wanaofanya vizuri na tuweze kushindanishwa na nchi nyingine katika
uzalishaji wa habari nzuri,lakini hata waziri anapoenda safari zake anaweza
kuwachukua hawa akaenda nao kwa sababu wanaweza kuandika habari nzuri zaidi
kutokana na kazi wanayoifanya hapa.”amesisitiza Waziri Gwajima
Ametoa rai kwa Wataalam wa maendeleo ya
Jamii,Ustawiwa Jamii na NGOs kuhakikisha
baada ya mafunzo hayo,wanafuatilia juu ya sayansi ya malezi na makuzi ya
maendeleo ya awali ya mtoto ipasavyo kwenye maeneo yeo ya kazi.
Pia amewataka kuwa mabalozi wa kuhakikisha jamii
inayowazunguka inapata uelewa wa malezi na makuzi ya watoto wadogo ikiwa ni
pmoja na kuhakikisha watoto wanapata
lishe ya kutosha,ujifunzaji wa awali,uchangamshi,malezi yenye mwitikio
na ulinzi na usalama wa mtoto ili watoto waweze kukua vizuri na kufikia
utimilifu wao.
“Twendeni tukaeleze jamii kwamba katika umri huu wa
kuanzia 0 mpaka miaka 8 ni muhimu kuwekeza kwa mtoto kwani ndipo ubongo wake
unapokuwa kwa asilimia 70-80,zungumza na mtoto kipindi hicho ambapo ubongo wake
unakua kwa kasi ,tukiyaweka mambo haya vizuri wanandishi wa habari watatusaidia
kuyafikisha kwa wananchi.”
Aidha amesema,matukio ya ukatili kwa watoto
yamezidi huku akisema zaidi ya watoto 11,000 wamekatiliwa,huku
akisema,yakiachwa matukio ya kubakwa na kulawitiwa pia watoto wamekuwa
wakifinywa na kupigwa vibao kupita kiasi na kuitaka jamii kuacha mara moja
vitendo hivyo dhidi ya watoto.
Awali Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi na Makuzi ya
watoto (TECDEN) Mwajuma Rwebangila aliiomba Serikali iendelee kuwaongoza katika
katika utekelezaji wa PJT MMMAM hadi katika ngazi za mikoa na Halmashauri.
Naye Mkurugenzi wa Children in Crossfire (CIC)
Craig Ferla,amesema kutokana na uzinduzi wa Programu ya MMMAM ,Tanzania imekuwa
ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimefikia hatua hiyo kwenye masuala ya MMMAM.
Amesema, CiC kwa kushirikiana na wadau wa masuala
ya MMMAM na TECDEN wapo tayari kuhakikisha utekelezaji wa Programu hiyo unafanyika
kwa ufanisi mkubwa na kufikia ndoto zilizokuwepo wakati wa uaandaaji wa
Programu hiyo.
Kwa upande wake Joyce Marangu kutoka Agha Khan
University amesema,Mafunzo hayo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya
Awali ya Mtoto (SECD) yanajumuisha katika ukuaji wa ubongo,kukabiliana na umahiri
,ikolojia ya utotoni,kuwasialiana na kujifunza na afya ya ukuaji.
Naye Victor Maleko kutoka UTPC ambao ni washirika
katika utekelezaji wa Mtoto Kwanza unaowakilishwa na kutekelezwa na waandishi
wa habari 26 nchi nzima.
“Waaandishi hawa walichaguliwa mahususi ,wana moyo
wa kujituma na wakati Programu ya MMMAM inazinduliwa sisi tulikuwa tumeshaanza
kufanya kazi hii ya kuhabarisha umma kwa ajili ya kuwekeza kwenye masuala ya
malezi na makuzi na mandeleo ya awali ya mtoto Tanzania nzima tangu mwaka 2019 ,
“Na mpaka siku Programu ya MMMAM inazinduliwa story
zaidi 1000 zilikuwa zimeshaandikwa Tanzania nzima ,ni juhudi za waadnishi hawa
vinara wa masuala ya malezi na makuzi ya watoto,na tangu kuzinduliwa kwa PJT
MMMAM mpaka sasa tayari habari zaidi ya 400 zimeshaandikwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa washiriki wa mafunzo
hayo Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Lindi Gaudence Nyamwihura amesema kwa
kupitia mafunzo hayo watakwenda kuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa jamii inazowazunguka.