|
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (Mwenye shati jeupe) akionyeshwa jinsi mashine ya kuchakata mpunga inavyofanya kazi alipotembelea soko la wafanyabiashara wa mchele jijini Mbeya |
NA JOYCE KASIKI,MBEYA
NAIBU Waziri wa
Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ametembelea kikundi cha wauzaji wa mchele
(Mbeya Rice Group) katika Kongano la wauzaji mchele soko la Mwanjelwa jijini Mbeya huku akiwaeleza wafanyabiashara
wa bidhaa hiyo kuwa serikali itaendelea
kuona na kupunguza tozo zisizo na tija kwao na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ya Kigahe
imekuja kufuatia malalamiko ya wafanyabiashara wa mchele katrika soko hilo la
mchele kutozwa tozo nyingi na hivyo kusababisha bidhaa ya mchele kuuzwa kwa bei
ghali.
“Naomba niwahakikishie
kuwa serikali itandelea kuwaunga mkono katika shughuli zenu na ndiyo maana leo
nimekuja nione kazi zenu lakini pia kusikia changamoto zinazokwamisha shughuli
zenu ili tuweze kuzifanyia kazi.”amesema Kigahe
Aidha amewataka
viongozi wa soko hilo waendelee kuboresha mchele wao ili kuhakikisha unakuwa ni
bidhaa bora ambayo inaweza kushindanishwa katika soko la Kimataifa.
“Naomba mjitahidi sana
katika uandaaji wa mpunga wakati mnapoelekea kuuchakata ili kupata mchele,hakikisheni
mnaanika vizuri mahali ambapo hapawezi kusababisha mchele kuwa na mchanga
lakini pia mtafute mashine ambayo inayoweza kupumbua mchele na chenga,lengo
kubwa hapa ni kifaya bidhaa yetu ishindane kimataifa.”amesema Kigahe
Aidha amesema,Serikali
inaendelea kuongea na taasisi za kifedha na hasa kwenye vikundi ili
wafanyabaishara hao waweze kukopesheka na benki mbalimbali ikiwemo benki ya
TIB.
“TIB wana fedha za
kutosha na wanalenga vikundi vilivyopo
kwenye sekta hii ya kilimo na riba yao haizidi asilimia nane ,na
mngekuwa na SACCOs yenu mngekopa kwa asilimia nne mpaka tano ,sasa hii
ingewawezesha kupata mitaji na hivyo kupata teknolojia mnazozihitaji kutoka
katika kiwanda cha SIDO.
Ametumia nafasi hiyo
kuitaka SIDO iwapeleke TIB
kuwatambulisha kwamba ni kikundi chenye tija katika uchumi wa nchi ili waaminike na kuwawezesha kupata mitaji na huduma nyingine zitakazosaidia kuboresha biashara zao.
Vile Vile ameielekeza SIDO iwasaidie kutengeneza
teknolojia wananzohitaji kwa gharama nafuu au iwaunganishe na sehemu ambako ni
sahihi ili waweze kupata hizo teknolojia
“Kwa hiyo mimi niseme
sisi tutaendelea kuwasaidia,kuwatengenezea mazingira mazuri zaidi ili mzalishe kwa tija .”
Kuhusiana na suala la
ushuru mkubwa lililolalamikiwa na wafanyabiashara hao,Naibu Waziri huyo
ameiagiza Ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa ilichukue hilo na waone namna ya
kuangalia kupunguza ushuru ili waweze kuchukua wafanyabiashara wengi zaidi na
kupata fedha nyingi licha ya kukusanya kidogo kidogo lakini itaongeza uhiyari wa kulipa kodi na hivyo
serikali kupata mapato mengi zaidi.
“Kwa hiyo nadhani hili
tuliangalie kama serikali na hasa wenzetu wa halmashauri mtusaidie, kwa hiyo
mtaangalia maeneo ya kodi na vibali mbalimbali wanapoenda kununua mazao kwa
wakulima.”amesisitiza
Awali Katibu Mkuu wa
Mbeya Rice Group Julius Ngalawa amesema,lichaya changamoto wanazokumbana nazo
lakini wameendelea na biashara hiyo ambayo imeajiri zaidi ya watu 3000.
“Mbeya Rice Group,tunachakata
tani 78,000 za mpunga.. ,na inashughulika na mnyororo wa thamani wa zao la
mpunga wanaanza kwa mkulima mpaka kwa mlaji ,tuna vikundi vya wakulima katika
maeneo mbalimbali tunafanya mikataba nao na pia tuna wakulima mmoja mmoja ambao
ni binafsi wanakuja kukoboa,
“Pia Mbeya Rice Group
tuna watu zaidi ya 3000 tunaofanya nao kazi ambao tumewaweka katika
vikundi,kuna vikundi vya washushaji ,wabeba mchele,usaidizi mashineni,pia kuna
wananwake wapatao wanane wanaomiliki
mitambo ya kukobolea mpunga.”
Aidha amesema ,kikundi
hicho kinajishughulisha na uuzaji wa mchele nje ya nchi ambapo amesema biashara
bado haiajwa rasmi lakini mpango wao ni kuhakikisha biashara hiyo inakuwa rasmi
ili waweze kulipa kodi za serikali maslahi mapana ya nchi.
Amesema masoko ya
mchele wanaouzalisha yapo katika nchi za Uganda,Zambia ,Botswana ,kwa hiyo
Mbeya Rice Group tukajiongeza tukaona ni nafuu sasa tuwe na sehemu ambayo ni
Packaging process ambayo tutakuwa tutatoa mchele katika mashine zetu tunauweka
sehemu tunafanya ‘packaging’ tunaukatia vibali na kuusafirisha kwa njia halali
ili serikali na wananchi kwa ujumla kila mmoja apate pato lake.
Kwa mujibu wa Ngalawa
kikundi hicho kimeingia makubaliano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH
ambapo walifanikiwa kupata wazo bunifu la mashine ya kukaushia mpunga na wamepata
milioni 40 kutoka COSTECH kwa ajii ya kutengenezewa mashine ya kukaushia mpunga
ambayo itakuwa ni suluhisho la ukaushaji wa mpunga na kutoa bidhaa bora ya
mchele.
Kwa upande wake
mfanyabiashara wa Mchele Joyce Mahenge amemuomba Naibu Waziri huyo awasaidie
katika kupunguza utiriri wa kodi unaosababisha kuleta kero kwao na mchele
kuuzwa kwa bei ghali.