Serikali ya[ongezwa kufuta kiingilio maonyesho Nane Nane Mbeya

Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenrali Hassan Mabena akitembelea eneo la kilimo (Shamba darasa)  la JKT



                                       NA JOYCE KASIKI,DODOMA

 MKUU wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena ameipongeza serikali kwa kuondoa kiingilio katika maonyesho ya wakulima maarufu kama Nane Nane ambayo Kitaifa yanafanyika jijini Mbeya kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Brigedia Jenerali Mabena ambaye amemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mkuu wa JKT amesema hatua hiyo itaongeza ari kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kufika katika maonyesho hayo na kujifunza masuala mbalimbali ya kilimo,ufugaji na uvuvi na hivyo kuleta tija kwenye maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango kuzindua sherehe za maonyesho hayo,Brigedia Jenerali Mabena amesema,maonyesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kuona pembejeo na zana za kilimo mifugo na uvuvi kwa jili ya kujifunza mbinu bora za uzalishaji wenye tija kwa mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi.

Aidha ameipongeza Serikali chini ya uongozi wa Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele katika sekta hizo kwa kuongeza bajeti kila mwaka ili kuleta tija.

“Sisi sote ni mashahidi ,2022/23 serikali ilitenga bajeti kubwa katika maeneo hayo na hata katika mwaka huu wa fedha imeongeza fedha ambazo zinakwenda kuleta uhakika wa usalama wa chakula nchini na hivyo kuleta utoshelevu wa chakula na ziada kuuzwa nje na kuleta  fedha za kigeni ambazo zitatumika katika maendeleo ya nchi.

Pia ameipongeza serikali kwa kuwaona vijana na kuwatengenezea mazingira ya kujiinua kiuchumi kupitia mradi   unaolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kuwapatia mafunzo, maeneo ya mashamba, mitaji na kuwaunganisha na fursa za masoko ( Building a Better Tomorrow-BBT) ambao sasa utawahusisha na vijana wa kujitolea wa JKT ambapo watapata mafunzo katika vituo atamizi.

Amesema tayari Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa  na wizra ya kilimo wameshasaini makubaliano ambapo mpango uliopo sasa ni kurudia yale makubaliano ili kuwahusisha vijana wa JKT katika mpango wa serikali wa kuwa na mashamba nundu.

Aidha amesema hivi karibuni Wizara ya Mifugo na Uvuvi na wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inakwenda kusaini makubaliano ili vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT  nao wahusishwe katika mpango huo maalum.

“Ili kuhakikisha mpango unaezeshwa serikali imetoa malekezo kwa taasisi za kibenki kupunguza riba za ukopaji na kutoa masharti nafuu ili wafugaji ,wakulima na wavuvi waweze kuenedeleza maeneo hayo ili kuongeza mazao ya chaukula,ufugaji na uvuvi na pia itawezesha vijaa kupata ajira,itakwenda kuongeza pato la Tafa na uhakika wa usalama wa chakula nchini.

Brigedia Jenerali Mabena amewasihi wanchi wa mkoa wa Mbeya na mikoa ya Jirani kutumia fursa iliyotolewa ya kuingia kwenye maonyesho hayo bila kiingilio kwa kufika hasa katika banda la JKT ambako watapata elimu zuri ya kilimo,ufugaji na uvuvi kwa lengo la kuwawezesha wananchi kuzalisha kwa tija katika maeneo hayo.

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.