NA JOYCE KASIKI,RUANGWA
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewataka watanzania kote nchini kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kwenye sekta ya madini na kuisajili TIC ili kuzalisha ajira na kuongeza thamani Kwa lengo la kukuza uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji lililofanyika katika viwanja vya soko jipya Kilimahewa wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi ambapo yanafanyika maonyesho ya madini Afisa Mwekezaji Mkuu wa TIC Girson Ntimba amesema ipo haja Kwa watanzania kujitokeza na kuwekeza katika sekta hiyo.
"Kufanya hivyo kutaweza kuimarisha uchumi wa nchi na katika hilo tayari Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imelifanyia kazi kupitia kituo hicho cha uwekezaji na wanahamasisha watu wawekeze miradi ya nyenye thamani."amesema na kuongeza kuwa
"Hapa niseme tu miradi yenye thamani ni kama kuzalisha vital ,Pete hereni na vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kutumika na tukapeleka nje Kwa ajili ya kupata fedha za nje,
"Mheshimiwa mgeni rasmi Waziri Dotto Biteko ,niseme kwamba sisi TIC katika kuhamasisha wawekezaji wa ndani ,katika maonyesho haya tumeweza kupata wawekezaji wawili ambao ni Jitegemee ambao tayari wamesajili mradi na hatua zingine zinaendelea ili kuweza kupata kibali."
Vile vile ametaja Kampuni nyingine ni Elianje ambayo nayo ipo kwenye mchakato wa kusajili ili kuweza kupata cheti cha uwekezaji
Amefafanua kuwa Kampuni inapopata cheti cha uwekezaji inapata msamaha wa Kodi ambao lengo lake ni kuweza kutoa ajira. "Kwa hiyo Serikali inasamehe Kodi ambapo kwa Sasa hivi ili mwekezaji aweze kuweka mradi na kuzalisha ,kuajiri watu na kuongeza kipato Chao na mwekezaji apate faida na Serikali ipate faida ,na kuweza kupata mapato ili badae aweze kulipa Kodi ."
Ameongeza kuwa"Hivyo kusamehe Kodi nikuleta na kuwezesha miradi kuajiri watu wengi ili watanzania wanufaike na miradi hiyo Kwa misingi hiyo kituo cha uwekezaji kitatoa cheti ambacho kitafanya upate msamaha wa Kodi wakati wa kuingiza vifaa bandarini Kwa ajili ya mradi wowote ,iwe utalii au mradi wowote ambao unaongeza thamani na kuhakikisha unapata faida.
Ametumia fursa hiyo kuwataka wawekezaji kufika kwenye ofisi za kituo cha uwekezaji TIC ili waweze kusajili miradi yao Ili wanufaike na uwepo wa TIC .
No comments:
Post a Comment