MENEJA WA TARURA WIAYA YA RUANGWA M𝗞OANI LINDI |
NA JOYCE KASIKI ,RUANGWA
ZAIDI ya shilingi bilioni 11 zimetumika katika mwaka wa fedha 2021/2022 katika ujenzi wa barabara zinazoelekea katika maeneo mgodi Wilayani Rwangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya madini
yanayoendelea katika wilaya ya Rwangwa ,Meneja Tarura Wilaya ya Rwangwa
Mashaka Narubi amesema kuwa pia mwaka huo huo wa fedha 2021/2022 wamejenga
barabara za lami maeneo ya mji wa Rwangwa mjini ambazo zinaelekea maeneo
yote ya migodi ambapo zimegharimu shilingi bilioni 5.2.
Amesema lengo la ujenzi wa barabara hizo ni kurahisisha shughuli za uchimbaji wadini unaoendelea Wilayani humo ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
"Kwenye mpango wetu wa mwaka 2021 mpaka mwaka 2023 tumejengaa jumla ya madaraja madogo 47 ambapo shilingi bilion 1.5 zilitumika katika ujenzi huo na nadaraja yotectuliyoyajenga maeneo ya vijijini ambapo kama fusa kwa wachimbaji wetu wa madini"amesema mashaka.
"Mwaka huu wa fedha 2023/2024 tunakusudia kujenga barabara kilomita
110 kuelekea maeneo ya madini ambapo tunatarajia kutumia bilion 3.4 kwa ajili
ya barabara katika maeneo ya madini"ameongeza.
Pia amesema Tarura Wilaya ya Rwangwa imejilita zaidi kuboresha barabara zinazoelekea kwenye maeneo yenye fursa ya madini ambapo wanaamini kwakufanya hivyo wawekezaji wa madini wajitokeza kwa wingi wilayani humo.
Mashaka ameongeza kuwa mbali na kujenga barabara hizo pia wana
mpango wakuongeza barabara nne ambazo ziraelekea kw4nye maeneo kwenye maeneo ya
madini kwa kiwango cha lami kutoka Rwangwa kuelekea eneo la Nangurugai ambapo
kuna mgodi wa grafact ambapo amesema amesema wameshaanza usanifu na mwezi wa
kumi mwaka huu taanza ujenzi wake ambao itakuwa kilometa thelathini na moja.
No comments:
Post a Comment