WAKULIMA WAIOMBA TFRA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA


 

           

Wateja waliofika kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Nchini (TFRA) kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kati Joshua Ngondya.

             NA RENATHA MSUNGU ,DODOMA

WAKULIMA wa mazao mbalimbali hapa nchini, wameishauri Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA),kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea  ili kuwasaidia kufanya kilimo chenye tija.

Hayo yamebanishwa na Mkulima Joseph Nyimbo wakati akipata maelekezo ya namna ya kujisajili ili aweze kupata mbolea ya ruzuku kutoka serikalini.

"Wakulima wengi hatujui matumizi ya mbolea, tunaishkuru TFRA kwa kuendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa matumizi ya mbolea,"Amesema Nyimbo.

Kwa upande wake Meneja wa TFRA Kanda ya Kati Joshua Ng'ondya amewataka wakulima kutoka kwenye Kilimo cha mazoea na badala yake wafanye kilimo chenye tija ili kujiinua kiuchumi.

Amesema wanapaswa kutumia mbolea sahihi ambazo zinaubora uliothibitishwa na TFRA ili kuendesha kilimo chenye tija ambacho kitawainua kiuchumi.

"Ni vizuri mkazingatia elimu mnayopewa na watalam wa kilimo,ikiwemo kutumia mbolea ya ruzuku kwa ajili ya kustawisha mazao shambani,"Amesema Ng'ondya

Naye Afisa Udhibiti Ubora wa TFRA Steven Gossi amewataka wakulima kujitokeza kujisajili ili waweze kupata mbolea ya ruzuku kutoka serikalini.

Amesema hivi sasa mfumo wa utoaji mbolea umeboreshwa.

 

 

Share:

No comments:

Post a Comment

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.