Umeme wa Julius Nyerere kuingizwa kwenye Grid ya Taifa

 

WAZIRI WA NISHATI JANUARY MAKAMBA


NA JOYCE KASIKI,DODOMA

SERIKALI  imesema katika mwaka ujao wa fedha inatarajia kuingiza umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kwenye Gridi ya Taifa  huku ikisema hilo ni tukio la kihistoria hapa nchini.

Aidha imesema,katika kukabiliana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika mwaka ujao wa fedha,ina mpango wa kufunga vituo vidogo vya kupozea umeme (substation) kila wilaya hapa nchini mradi ambao utagharimu kiasi cha shilingi  trilioni nne

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati January Makamba leo Mei 31,2023 wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 ambapo ameomba kiasi cha shilingi trilioni 3.048.

Amesema katika kipindi cha wiki moja kuanzia sasa bwawa la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  litafikisha kiwango cha ujazo kinachowezesha kuanza uzalishaji wa umeme.

Kwa mujibu wa Makamba hadi kufikia 23 Mei, 2023 kina cha maji ya Bwawa kilikuwa kimefikia mita 160.51 kutoka usawa wa bahari na ili kuweza kuzalisha umeme, kiwango cha chini cha maji kinatakiwa kufikia mita 163 kutoka usawa wa bahari.

Amesema ujazaji wa maji unaendelea kulingana na Mpango Kazi wa Ujazaji wa Bwawa ambapo hadi kufikia  23 Mei, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu ambacho ni mita za ujazo bilioni 30.

"Hadi kufikia  23 Mei, 2023 kina cha maji ya Bwawa kilikuwa kimefikia mita 160.51 kutoka usawa wa bahari na ili kuweza kuzalisha umeme, kiwango cha chini cha maji kinatakiwa kufikia mita 163 kutoka usawa wa bahari,

"Ujazaji wa maji unaendelea kulingana na Mpango Kazi wa Ujazaji wa Bwawa ambapo hadi kufikia 23 Mei, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu ambacho ni mita za ujazo bilioni 30."amesema Makamba na kuongeza kuwa 

Kwa kuwa siku za nyuma kumekuwa na shaka ya masuala ya mazingira na uwezekano wa bwawa letu kujaa maji,naomba niwatangazie rasmi kwamba katika kipindi cha wiki moja kuanzia sasa tutafikia kiwango cha chini cha kuweza kuzalisha umeme ,

“Kiwango cha chini ni mita  163 kutoka usawa wa bahari na tumebakiza mita mbili kufikia kiwango hicho na tutafika huko.”amesema Makamba

Vile vile amesema,katika kipindi hicho pia  serikali kupitia Shirika la Umeme nchini TANESCO  itaanza utekelezaji wa miradi ya (CSR) miradi ya kijamii inayotokana na mikataba ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere.


Share:

Cherehani ataka kumalizwa mgogoro wa mipaka

MBUNGE WA USHETU EMMANUEL CHEREHANI

 

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MBUNGEwa Ushetu Emmanuel Cherehani (CCM) ameiomba Serikali kuingilia kati kumaliza mgogoro wa mipaka uliopo baina ya Pori la Ubagwe lililopo katika Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga na Halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ili kumaliza sintofahamu ya mipaka ya maeneo hayo miongoni mwa wananchi.

Akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma Mei 31 ,2023,Mbunge huyo amesema  Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ina mapori matatu ya Usumbwa ,Ubagwe  na Mpunzesabasabin huku akisema katika Pori la Ubagwe kuna mgogoro mkubwa na Halmashauri ya wilaya ya  Kauliua.

“Mgogoro huu umekuwa ukichukua sura mpya kila wakati ,na juzi wananchi wangu wamekamatwa wakawekwa ndani bila sababu za msingi na mbaya zaidi juzi kumekuwa na mgogoro kati ya askari wa Wakala wa Misitu (TFS)  na askari wa Maliasili na Utalii wa Ushetu,nini Kauli ya Serikali na lini mgogoro huo  utaenda kutatuliwa?”amehoji Cherehani

Cherehani pia ameihoji Serikali lini itatenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya malisho ya mifugo kwani kila siku mifugo inaendelea kuongezeka huku ardhi ikabki kuwa ni ile ile.

“Idadi ya ng’ombe kwa wananchi wa Ushetu inazidi kuongezeka mpaka sasa wana ng’ombe 176,000 na wanapakana na mapori ,lakini  wananchi hawana eneo la kuchungia,lini serikali itamaliza tathimini  ili wananchi wapate eneo la kulishia mifugo yao bdala ya kuendelea kugombana baina ya wananchi na Maafisa wa Maliasili.”amehoji Mbunge huyo

Akijibu swali hilo Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema,Wizara yake itawasiliana na Wizara ya Mifugo ili kuona namna ya kutenga maeneo ya mifugo.

“Kwa kuwa Wizara imepewa dhamana ya kulinda na kuyasimamia maeneo hayo inapofika haja ya mahitaji ya maeneo ya mifugo basi tuendelee kuwasiliana na wizara husika ili tukae pamoja tuone namna  bora ya kutenga maeneo hayo.”

Kuhusu mgogoro wa mipaka amesema Serikali inaendelea kuangalia namna ya kuainisha mipaka ili kumaliza migogoro iliyopo inayotokana na mipaka.


Share:

Semguluka ahoji ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji Mwihuzi Nyakahula

MBUNGE WA VITI MAALUM OLIVER SEMGULUKA

 

        NA JOYCE KASIKI,DODOMA              

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Serikali inatarajia kujenga skimu ya umwagiliaji katika eneo la Mwihuzi Nyakahula wilaya ya Biharamlo.

Mavunde ametoa kauli hiyo Mei 31,2023  Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye alitaka kujua lini serikali itajenga skimu hiyo ya umwagiliaji ili kuwawezesha wananchi kufanya kilimo cha umwagiliaji.

“Je ni lini serikali itajenga skimu ya umwagiliaji Mwihuzi Nyakahula wilaya ya Biharamlo”amehoji Oliva

Akijibu Mavunde amesema “Kwenye kitabu cha bajeti ya Wizara ya Kilimo Skimu ya Mwihuzi Nyakahula imetajwa kama sehemu itakayojengwa katika mwaka wa fedha ujao ,kwa hiyo  nimtoe hofu Mbunge kwamba kazi ya ujenzi wa skimu hiyo itafanyika katika mwaka wa fedha ujao.”amesema Mavunde


Share:

Mbunge Njalu ahoji ujenzi wa madaraja matano wilaya ya Itilima

MBUNGE WA ITILIMA SILANGA NJALU (CCM)

 

          NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MBUNGE wa Jimbo la Itilima Silanga Njalu (CCM) ameihoji Serikali kwamba ni lini  itajenga madaraja  matano katika Mito Galamoha , Isolo, Nyagokolwa, Mbogo na Mhuze katika wilaya ya  Itilima.

Aidha katika swali la nyongeza mbuge huyo ametaka kujua kwa nini serikali isiweke fedha za maendeleo ili wananchi waweze kujengewa daraja hilo.

Akiuliza swali Bungeni jijini Mei 30 ,2023,Mbunge huyo pia alitaka Serikali ione umuhimu wa kufungua barabara ya  Makutano-Makulija-Supaloji ambayo imebaki kilomita 51 tu .

Amesema kufungua barabara hiyo kutarahisisha shughuli za kiutalii katika wilaya ya Itilima.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi amesema,katika  Mwaka wa Fedha 2022/23, Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA)  iliajiri Mhandisi Mshauri-Chuo cha Ufundi Arusha kufanya Uchunguzi wa kijiolojia katika mto Galamoha ambapo kazi hiyo imekamilika kwa gharama ya Shilingi Milioni 35.

Aidha amesema kwa sasa TARURA inaendelea na Usanifu wa Daraja hilo kwa lengo la kupata gharama halisi za utekelezaji wa ujenzi wake.

Kuhusu  Mto Isolo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, Serikali imetenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 41 kwa ajili ya kujenga daraja la Mawe Sehemu ya

kwanza ya Mto Isolo ambapo ujenzi wa Daraja la pili katika Mto Isolo usanifu wake utafanyika katika Mwaka wa Fedha 2023/24 kwa kutumia wataalam wa ndani wa TARURA.

Kuhusu Mto Mbogo Ndejembi amesema,Serikali imetenga jumla ya Shilingi Milioni 40 katika Mwaka wa Fedha 2023/24 kwa ajili ya usanifu wa Ujenzi wa Daraja kwa tekinolojia ya upinde wa Mawe lenye ukubwa wa mita 15 ili kupata gharama halisi.

Kwa upande wa  Mto Mhuze Naibu Waziri huyo amesema,umetengewa Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kijiolojia ili kuwezesha kusanifu kwa daraja hilo.

“Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa madaraja katika Mto Galamoha , Isolo, Mbogo na Mhuze utaendelea baada ya kukamilika kwa usanifu ili kupata gharama halisi za ujenzi.”amesema Ndejembi


Share:

Serikali kutimiza ahadi ya Rais Samia kata ya Litui

 

MBUNGE WA VITI MAALUM MHANDISI STELLA MANYANYA

       NA JOYCE KASIKI,DODOMA

NAIBU Waziri,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kufika kwenye kata ya Litui  ili kufanya tathimini na kuona uhitaji uliopo ili Serikali iweze kutimiza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga kituo cha afya katika Kata hiyo.

Ndejembi ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma Mei 31 ,2023 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyasa  Mhandisi Stella Manyanya (CCM) ambaye alitaka kujua lini Serikali itajenga kituo cha afya katika kata hiyo ili kutekeleza ahadi ya Rais Samia.

Ndejembi ametaja mambo ya kuyazingatia wakati wa tathimini hiyo ni pamoja na  idadi ya watu waliopo katika eneo hilo na kuwasilisha taarifa katika ofisi za Rais Tamisemi ili waweze kuingiza katika mipango ya ofisi hiyo ya kujenga vituo vya afya .

Aidha amesema mwaka wa fedha  2024/25  Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) inakusudia kuanza ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa kwenye vituo vya afya ambavyo vilishapokea fedha za ukarabati na ujenzi .

Akijibu swali la msingi la Mhandisi Manyanaya  (CCM)  Ndejembi amesema kuwa  jumla ya vituo vya afya 817 vinahitaji kujengewa wodi za kulaza wagonjwa kikiwemo kituo cha afya cha kihangara.

Aidha katika swali la msingi Mhandisi Manyanya  amesema kwa kuwa kituo cha afya Kihangara katika Halmashauri ya wilaya ya Nyasa licha ya kukosa wodi hasa ya akina mama lakini pia hakina  mashine ya utrasound hali inayosababisha upasuaji hasa wa akina mama wanaojifungua kwa upasuaji kupata huduma hiyo kwa kubahatisha.

Kufuatia hali hiyo Mbunge huyo ameitaka  serikali kueleza ni lini  itafikiria kupeleka mashine ya utrasaound katika kituo cha afya Kihangara ili kusaidia wananchi hususan akina mama wanaohitajika kujifungua kwa upasuaji l;akini pia ametaka kujua lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya  kujenga kituo cha afya kata ya Litui.

Hata hivyo Ndejembi amesema, Serikali itaangalia  katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha kuona kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika halmashauri ya wilaya ya Nyasa ili wahudumu waweze kununua utrasound mara moja ili kuhudumia akina mama wajawazito katika eneo la kihangala.


Share:

Majaliwa aeleza mwelekeo wa Serikali katika matrumizi ya Nishati mnadala kuokoa misitu

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

                                       


              NA JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa maesema,Serikali imeunda Kamati ya Kitaifa inayoratibu utoaji elimu ya matumizi ya Nishati mbadala ili nchi iweze kuondokana na matumizi ya kuni zinazosababisha ukataji misitu hovyo.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijni Dodoma kwenye maonyesho ya wiki ya Nishati,Waziri Mkuu Majaliwa amesema,kamati hiyo itaonyesha na kutoa fursa za wajasiriamali ambao watahitaji kuingia kwenye sekta hiyo kwa lengo la kuelimisha zaidi watanzania wabadilike kuwa na matumizi ya Nishati mbadala .

“Na huo mbadala ni mabadala wa kuondoa matumizi yanayosababisha kuharibika ka misitu ambayo leo hii Duniani tunakabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi .”amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa

“Serikali imejipanga vizuri kupitia vikao vyetu vya awali na  sasa tutakuwa na kikao kikubwa cha Kitaifa kinachojumuisha na Serkali ya Mapinduzi Zanzibar ili eneo lote la nchi yetu lifikiwe na elimu hiyo na waanze kutumia nishati  mbadala.”

Aidha amesema,”Na kwa kuwa hatua zimeshaanza kuchukuliwa tunataka tuimarishe eneo hilo na tuanze mara moja kwa watanzania kutumia nishati mbadala..,kwa hiyo kamati ya Kitaifa ikiwa inaendelea kuratibu vizuri tutatoa maelekezo kadiri tunavoypendelea.”

Ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuanza utekelezaji wa kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya Nishati mbadala ambao pia wataenda kuhamasisha  wananchi matumizi ya nishati mbadala katika maeneo yao.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo kwa Serikali itaanza na taasisi za elimu ,ambazo zinalaza wasomi wake sehemu moja,lakini pia majeshi ,vyuo,kambi za wakimbizi.

“Huo ndiyo mwelekeo wa Tiafa letu na tunahitaji watanzania ambao wamefikiwa an elimu hii waisambaze ili kujenga uelewa wa pamoja katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi”

Ametumia nafasi hiyo kupongeza makundi mbalimbali ya wananchi wanaojihusisha na kutengeneza mkaa kwa kutumia takataka mbalimbali huku akisema serikali inahitaji  teknolojia hiyo iwafikie wengi ili nishati hiyo mbadala iwafikie watanzania wote na ipatikane kwa urahisi.

Share:

Gekul aagiza uchunguzi wa rushwa gereza la Babati Mjini

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul  akisikiliza kesi ya mahabusu Mwajuma Mada aliyefika gerezani Babati mjini  ikiwa ni sehemu ya msaada unaotolewa na timu ya wataalam wa Mama Samia Legal Aid Campaign

Timu ya wataalamu na uongozi wa gereza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kazi hiyo ya kutoa msaada wa kisheria kwa watu walio vizuizini.


       NA LUSAJO MWAKABUKU-WKS MAYARA

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameuagiza Uongozi wa Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Manyara pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mahabusu na Wafungwa wa gereza la Babati Mjini dhidi ya askari na watumishi wa vyombo hivyo vya haki ambapo katika nyakati tofauti wameonekana kutumia nafasi zao kudai rushwa kwa malengo ya kukwepesha haki.

Tuhuma hizo zimetolewa tarehe 24/05/2023 wakati timu ya wataalam wanaoendesha Mama Samia Legal Aid Campaign ikiongozwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ilipofika gerezani hapo kwa lengo la kutoa elimu pamoja na msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hiyo kubwa iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwaka huu ambayo itadumu kwa miaka mitatu mpaka 2026.

Akiambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mashtaka, Tume ya haki za binadamu, Mrakibu wa Polisi wa Mkoa, Dawati la jinsia la polisi, Wanasheria na watumishi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Naibu Waziri Gekul alifika katika gereza la Babati na kufanikiwa kuongea na uongozi lakini pia na wafungwa na mahabusu waliokuwepo katika gereza hilo lengo likiwa ni kubaini changamoto za kisheria zikiwemo upatikanaji wa dhamana kwa wafungwa wanaostahili pamoja na namna kesi zao zinavyoendeshwa.

Timu ya wataalam wa Mama Samia Legal Aid Campaign ilipokewa na uongozi wa Gereza hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Nkonge Edwin alimweleza Naibu Waziri kuwa moja kati ya vitu ambavyo gereza hilo limefanikiwa kuvitekeleza ni pamoja na kesi kusikilizwa kwa wakati kitu ambacho ni kilio kwa watu wengi walio vizuizini katika maeneo mengine huku akiainisha kasoro ndogondogo zikiwemo uchakavu wa vyombo vya usafiri katika kutoa huduma za wafungwa pamoja na kukataliwa kwa rufani zilizo nje ya muda.

Timu hiyo ya Mama Samia Legal Aid Campaign baada ya kuongea na uongozi wa Gereza iliingia ndani ya gereza na kuongeza na mahabusu pamoja na wafungwa ambapo elimu ya sheria ilitolewa jinsi mtu anavyokamatwa kituoni mpaka anapelekwa gerezani vitu vinavyotakiwa kufuatwa.

 Lakini pia mtaalam kutoka haki za binadamu alielezea haki za msingi za wafungwa wakiwemo gerezani ikiwemo haki ya dhamana kwa makosa yenye dhamana na pia Ofisa kutoka Ofisi ya Mashtaka akaongelea wajibu wa Ofisa wa mashtaka wa wilaya na muda uliopangwa kisheria wa kushughulikia kesi za watu walio vizuizini ambapo kwa kwa mkoa huu hali imeonekana kuwa shwari kwani hakuna mfungwa au maabusu aliyelalamika kupitilizwa muda wa siku 90 wa kusomewa shitaka lake mara wanapowekwa vizuizini kwa mujibu wa sheria.

Ilipofika wakati wa maswali, wafungwa na mahabusu walianza kwa kubainisha changamoto zao wanazokumbana nazo kupitia risala iliyosomwa na Mahabusu Michael Marko ambayo pamoja na mengine ilielezea changamoto ya ucheleweshaji wa upelelezi wa kesi unakopelekea mrudikano wa mahabusu gerezani.

 Ucheleweshwaji wa akala za hukumu kwa watu ambao wameshahukumiwa, Kuporwa fedha wakati wakikamatwa na polisi na pia wakasema kumekuwa na kawaida ya mahabusu kukamatwa na kuachiwa huku pia wakiituhumu Ofisi ya Mashtaka kutokuleta mashahidi kwa wakati.

Hali ikazidi kubadilika mara baada ya wafungwa na mahabusu hao kupewa nafasi ambapo bila kusita wala uoga waliwataja maaskali na maofisa upelelezi pamoja na makarani wa mahakama kwa majina ambao waliwapora fedha wakati wakikamatwa na wengine kuwataka walipe ili kesi zao zisiendelee. 

Na pia mahabusu na wafungwa hao walieleza kuwa walitakiwa kutoa hela zilizoanzia milioni mbili na kuendelea ili waachiwe wakati mahabusu mwingine akidai askari alimwambia mke wake atoke Singida aje alale Manyara na siku ya pili mumewe ataachiwa (Akiashiria rushwa ya ngono)

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Naibu Waziri aliwaagiza viongozi wa polisi pamoja na wa Ofisi ya Mashtaka alioambatana nao kuhakikisha kuwa wale wote waliotajwa katika tuhuma hizo uchunguzi wa kina unafanyika na wale wote watakaobainika kuwa wametumia mamlaka yaka yao vibaya basi hatua kali za sheria zichukuliwe dhidi yao na pia akawaagiza viongozi ha kuhakikisha wana jitihada za upatikanaji wa haki kwa mahabusu na wafungwa hao unapatika kwa wakati na bila usumbufu.


Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.