MBUNGE WA VITI MAALUM OLIVER SEMGULUKA |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
NAIBU Waziri
wa Kilimo Anthony Mavunde amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Serikali
inatarajia kujenga skimu ya umwagiliaji katika eneo la Mwihuzi Nyakahula wilaya
ya Biharamlo.
Mavunde ametoa
kauli hiyo Mei 31,2023 Bungeni jijini
Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha
Mapinduzi (CCM) ambaye alitaka kujua lini serikali itajenga skimu hiyo ya
umwagiliaji ili kuwawezesha wananchi kufanya kilimo cha umwagiliaji.
“Je ni lini
serikali itajenga skimu ya umwagiliaji Mwihuzi Nyakahula wilaya ya Biharamlo”amehoji
Oliva
Akijibu
Mavunde amesema “Kwenye kitabu cha bajeti ya Wizara ya Kilimo Skimu ya Mwihuzi Nyakahula
imetajwa kama sehemu itakayojengwa katika mwaka wa fedha ujao ,kwa hiyo nimtoe hofu Mbunge kwamba kazi ya ujenzi wa
skimu hiyo itafanyika katika mwaka wa fedha ujao.”amesema Mavunde
No comments:
Post a Comment