NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT.GODWIN MOLLEL |
NA WAF- BUNGENI DODOMA
Dkt. Mollel amesema hayo leo Mei 23, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha 31, Bungeni Jijini Dodoma.
Amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya iliona dalili za upotevu wa Bilioni 83 hivyo kushirikiana na TAKUKURU ili kuhakikisha wote wataobainika kuwepo katika upotevu huo wa dawa wanachukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia hiyo.
Dkt.Mollel amesema, Serikali imefanya mikakati mbalimbali katika kutatua tatizo la wizi na ubadhilifu wa dawa na vifaa tiba ikiwemo kufanya suala la upotevu wa dawa na vifaa tiba kama agenda katika vikao vya Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya.
Aidha amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha
mifumo ya usimamizi wa bidhaa za Afya ikiwemo kufunga mifumo ya kielectroniki
pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa bidhaa hizo.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Wizara kwa kushirikiana na OR TAMISEMI imeendelea kuimarisha kamati za usimamizi za vituo kwa kuzijengea uwezo kuhusu majukumu yao katika usimamizi wa bidhaa za Afya.
No comments:
Post a Comment