MBUNGE WA VITI MAALUM MHANDISI STELLA MANYANYA |
NA JOYCE
KASIKI,DODOMA
NAIBU
Waziri,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Deogratius Ndejembi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kufika kwenye kata ya
Litui ili kufanya tathimini na kuona
uhitaji uliopo ili Serikali iweze kutimiza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya
kujenga kituo cha afya katika Kata hiyo.
Ndejembi
ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma Mei 31 ,2023 wakati akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya (CCM) ambaye alitaka kujua
lini Serikali itajenga kituo cha afya katika kata hiyo ili kutekeleza ahadi ya
Rais Samia.
Ndejembi
ametaja mambo ya kuyazingatia wakati wa tathimini hiyo ni pamoja na idadi ya watu waliopo katika eneo hilo na
kuwasilisha taarifa katika ofisi za Rais Tamisemi ili waweze kuingiza katika
mipango ya ofisi hiyo ya kujenga vituo vya afya .
Aidha
amesema mwaka wa fedha 2024/25 Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za
Mitaa (TAMISEMI) inakusudia kuanza ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa kwenye
vituo vya afya ambavyo vilishapokea fedha za ukarabati na ujenzi .
Akijibu
swali la msingi la Mhandisi Manyanaya (CCM)
Ndejembi amesema kuwa jumla ya vituo vya afya 817 vinahitaji
kujengewa wodi za kulaza wagonjwa kikiwemo kituo cha afya cha kihangara.
Aidha katika
swali la msingi Mhandisi Manyanya amesema
kwa kuwa kituo cha afya Kihangara katika Halmashauri ya wilaya ya Nyasa licha
ya kukosa wodi hasa ya akina mama lakini pia hakina mashine ya utrasound hali inayosababisha
upasuaji hasa wa akina mama wanaojifungua kwa upasuaji kupata huduma hiyo kwa
kubahatisha.
Kufuatia
hali hiyo Mbunge huyo ameitaka serikali
kueleza ni lini itafikiria kupeleka
mashine ya utrasaound katika kituo cha afya Kihangara ili kusaidia wananchi
hususan akina mama wanaohitajika kujifungua kwa upasuaji l;akini pia ametaka
kujua lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kujenga kituo cha afya kata ya Litui.
Hata hivyo
Ndejembi amesema, Serikali itaangalia katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha kuona
kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika halmashauri ya
wilaya ya Nyasa ili wahudumu waweze kununua utrasound mara moja ili kuhudumia
akina mama wajawazito katika eneo la kihangala.
No comments:
Post a Comment