WAZIRI wa Ujeniz na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
SERIKALI imebainisha mikakati yake ya kuhakikisha
Shirika la Ndege la ATCL kuwa shindani katika soko duniani huku Kamti ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiitaka kuchukua hatua kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya sekta ya ujenzi kwa viwango vya chini kuchukuliwa hatu za kisheri ana kinidhamu.
Hayo yamesemwa leo Mei 22,Bungeni jijini Dodoma na
Wazazi wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa wakati akiwasilisha
bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha wa 2023/2024.
Amesema,miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na
ATCL kujihudumia yenyewe kwa kuhudumia abiria, mizigo, na ndege kiwanjani, kufanya
matengenezo makubwa na madogo kwa ndege zote.
“Vile vile kuongeza uwezo wa kutoa mafunzo nchini
kwa marubani, wahandisi wa ndege na wahudumu wa ndege kwa kushirikiana na vyuo
vya ndani.
Kwa mujibu wa Waziri huyo ,ili kutekeleza mikakati
hiyo, Serikali imeendelea kuiwezesha ATCL kuendelea na ukarabati na maboresho
ya karakana kubwa ya matengenezo ya ndege iliyopo Mkoani Kilimanjaro ambayo
imefikia asilimia 85.
“Ukarabati huu umeiwezesha ATCL kufanya matengenezo
ya kiwango cha “C Check” kwa ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Dash 8
Q400 na kufanya matengenezo yote madogo madogo kwa ndege zake zote. 269.
“Mikakati mengine inayotekelezwa na ATCL ni kuajiri
na kuwaendeleza watumishi katika kada maalum ambazo ni pamoja na Urubani na
Uhandisi mbapo hadi kufikia Aprili, 2023 ATCL iliajiri marubani tisa na hivyo
kufanya jumla ya marubani kuwa 108. “alisema Prof.Mbarawa
Aidha alisema, ATCL inatarajia kuajiri wahudumu wa
ndege 43 na hivyo kufanya jumla ya wahudumu wa ndege kufikia 164. Watumishi wa
kada nyingine zilizobaki wameongezeka hadi kufikia 389 ikilinganishwa na
watumishi 382 waliokuwepo Juni, 2022.
Alisema,ongezekeo hilo la watumishi limefanya ATCL
111 kuwa na watumishi 792 ikilinganishwa na watumishi 613 katika mwaka 2021/22.
Akitoa maoni ya ya jumla ya Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Miundombinu,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Moshi Kakoso ameitaka Serikali
kuhakikisha kwamba kunakuwepo na uwajibikaji wa watendaji na makandarasi katika miradi yote ambayo imetekelezwa au itatekelezwa chini ya
viwango kwa kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa wahusika .
Aidha Kamati hiyo imeishauri Serikali kuhakikisha
miradi ya wizara hiyo inazingatia viwango na ubora kwani ni miradi inayogharimu
fedha nyingi.
No comments:
Post a Comment