WAZIRI WA NISHATI JANUARY MAKAMBA |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
SERIKALI imesema katika mwaka
ujao wa fedha inatarajia kuingiza umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kwenye Gridi
ya Taifa huku ikisema hilo ni tukio la kihistoria hapa nchini.
Aidha imesema,katika kukabiliana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika
mwaka ujao wa fedha,ina mpango wa kufunga vituo vidogo vya kupozea umeme
(substation) kila wilaya hapa nchini mradi ambao utagharimu kiasi cha shilingi trilioni nne
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati January Makamba leo Mei 31,2023 wakati akiwasilisha
makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 ambapo ameomba kiasi cha
shilingi trilioni 3.048.
Amesema katika kipindi cha wiki moja kuanzia sasa bwawa la Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere litafikisha
kiwango cha ujazo kinachowezesha kuanza uzalishaji wa umeme.
Kwa mujibu wa
Makamba hadi kufikia 23 Mei, 2023 kina cha maji ya Bwawa kilikuwa kimefikia mita
160.51 kutoka usawa wa bahari na ili kuweza kuzalisha umeme, kiwango cha chini
cha maji kinatakiwa kufikia mita 163 kutoka usawa wa bahari.
Amesema ujazaji
wa maji unaendelea kulingana na Mpango Kazi wa Ujazaji wa Bwawa ambapo hadi
kufikia 23 Mei, 2023 kiwango cha maji
kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu
ambacho ni mita za ujazo bilioni 30.
"Hadi kufikia 23 Mei, 2023 kina cha maji ya Bwawa kilikuwa kimefikia mita 160.51 kutoka usawa wa bahari na ili kuweza kuzalisha umeme, kiwango cha chini cha maji kinatakiwa kufikia mita 163 kutoka usawa wa bahari,
"Ujazaji wa maji
unaendelea kulingana na Mpango Kazi wa Ujazaji wa Bwawa ambapo hadi kufikia 23 Mei, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa
na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu ambacho ni mita za ujazo bilioni 30."amesema Makamba na kuongeza kuwa
“Kwa kuwa siku za nyuma kumekuwa na shaka ya masuala ya mazingira na
uwezekano wa bwawa letu kujaa maji,naomba niwatangazie rasmi kwamba katika
kipindi cha wiki moja kuanzia sasa tutafikia kiwango cha chini cha kuweza
kuzalisha umeme ,
“Kiwango cha chini ni mita 163 kutoka usawa wa bahari na
tumebakiza mita mbili kufikia kiwango hicho na tutafika huko.”amesema Makamba
Vile
vile amesema,katika kipindi hicho
pia serikali kupitia Shirika la Umeme nchini TANESCO itaanza utekelezaji wa miradi ya (CSR) miradi
ya kijamii inayotokana na mikataba ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa Julius
Nyerere.
No comments:
Post a Comment