MKUU wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
JESHI la
Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana
wote waliohitimu elimu ya kidato cha sita kwa mwaka 2023 kutoka shule zote za
Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujibu wa sheria 2023.
Aidha Jeshi
hilo limesema,miundombinu ya Jeshi hilo limejiandaa vyema kwa kuwa na
miundombinu ya kutosha kwa ajili ya kuwapokea vijana hao.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya JKT Chamwino mkoani Dodoma kuhusu
wito huo wa vijana Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena
amesema, vijana hao wanapaswa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa kuanzia
Juni Mosi hadi Juni 11 mwaka huu.
“Vijana hao
wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma –Mara,JKT Msange –Tabora,JKT Ruvu
Pwani,JKT Mpwapwa ,Makutupora JKT-Ddpdpma,JKT Mafinga –Iringa,JKT Mlale-Ruvuma
,JKT Mgambo na JKT Maramba –Tanga .”
Ametaja kambi
nyingine kuwa ni “JKT Makuyuni-Arusha,JKT –Bulombora,JKT Kanembwa na JKT
Mtabila za Kigoma,JKT Itaka Songwe,JKT Luwa na JKT Milundikwa –Rukwa,JKT
Nachingwea-Lindi,JKT Kibiti –Pwani na Oljoro JKT Arusha.”
Kwa mujibu
wa Brigedia Jenerali Mabena wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho
wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu
ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
Aidha
amesema,orodha kamili ya majina ,makambi waliyopangiwa na mahitaji yote
yanayohitajika vinapatikana kwenye tovuti ya JKT www.jkt.go.tz.
No comments:
Post a Comment