PICHAI ni mitambo ya kualiha zge iliyozinduliwa jijini Dodoma na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza jijini Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa magari na mitambo ya kzualisha zege. |
NA MWANDISHI WETU DODOMA
MKUU wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Meja Jenerali Rajabu Mabele amelitaka Shirika
la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kuhakikisha linafanya
kazi kwa weledi ili kuendelea kuwapa imani wadau wanaowapa kazi kwamba wanaweza
kufanya kazi zao kwa viwango vinavyokubalika na kwa ubora zaidi.
Akizungumza
mei 23 mwaka huu jijini Dodoma wakati akizindua magari na Mitambo ya kuzalisha
zege katika eneo la Mwangaza jijini hump,Meja Jenerali Mabele amesema kutokana na imani hiyo lazima kazi zifanyike
kwa viwango vinavyotakiwa ili kutunza uaminifu huo.
Ametumia
nafasi hiyo kusihukuru Serikali ya awamu
ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliamini
shirika hilo kwa kulipa kazi huku akiahidi kuendelea kununua vifaa vya kisasa
ili kufanya kazi zenye ubora zaidi.
“Tunaishukuru
sana Serikali kwa kuendelea kutuamini na kutupa kazi na ndiyo maana mnaona na sisi
tunapambana ili kuhakikisha tunakuwa na
mitambo ili tuweze kuzitekeleza kazi hizo kwa ufasaha,kwa wakati na vizuri
zaidi.”amesema Meja Jenerali Rajab Mabele
na kuogeza kuwa
“Kwa imani
hii tunayopewa na Serikali,watendajiwote wa SUMAJKT lazima tuonyeshe kwamba
wale wanaotuamini hawajakosea,kwa hiyo tufanye kwa kazi kwa bidii ili kuhakikisha
imani ile ile tunayopewa na sisi tuendelee kuonyesha kwamba tupo tayari kwa
ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya serikali ,tufanye kazi kwa
wakati,kazi zenye viwango kama ambavyo tunafanya siku zote tuendelee kuwa na
bidii katika majukumu yetu ya kila
siku.”
Aidha ametaka
mitambo hiyo itunzwe kwa kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara kila
inapohitajika na kwa wakati muafaka ili iendelee kuwa endelevu la kuleta faida
ndani ya shirika na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema, tukio hilo ni
moja ya utekelezaji wa mikakati yao waliyojiwekea ya kuongeza mitambo na
vitendea ili kujiongezea uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Awali akitoa
taarifa ya mtambo huo Mkurugenzi Mwendeshaji kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Injinia Mogan Nyoni amesema vifaa
vilivyozinduliwa vimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.349 huku akisema zoezi la usimikaji hadi kufikia Mei 22 mwaka
huu lilikuwa limefikia asilimia 95.
“Kukamilika
kwa usimikaji wa mitambo hiyo utaongeza kipato cha kampuni ya ujenzi na shirika
kwa ujumla kwani hitajio la zege jijini Doodma ni kubwa lakini pia kutaongeza
imani za kiutendaji kutoka kwa washitiri kutokana na kazi ambazo SUMAJKT na kampuni ya Ujenzi inafanya .”alisema
Injia Mogan
Kwa upade
wake Mwenyekiti wa Bodi SUMAJKT amesema ,mitambo hiyo itaongeza thamani katika
shirika kutokana na ubora wa bidhaa zinazozalishwa,urahisi wa upatikanaji wake
,gharama za uzalishaji kupungua lakini
pia muda wa uzalishaji utapungua.
No comments:
Post a Comment