MBUNGE WA USHETU EMMANUEL CHEREHANI |
NA JOYCE
KASIKI,DODOMA
MBUNGEwa
Ushetu Emmanuel Cherehani (CCM) ameiomba Serikali kuingilia kati kumaliza
mgogoro wa mipaka uliopo baina ya Pori la Ubagwe lililopo katika Jimbo la
Ushetu mkoani Shinyanga na Halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ili
kumaliza sintofahamu ya mipaka ya maeneo hayo miongoni mwa wananchi.
Akiuliza
swali Bungeni jijini Dodoma Mei 31 ,2023,Mbunge huyo amesema Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ina mapori
matatu ya Usumbwa ,Ubagwe na
Mpunzesabasabin huku akisema katika Pori la Ubagwe kuna mgogoro mkubwa na
Halmashauri ya wilaya ya Kauliua.
“Mgogoro huu
umekuwa ukichukua sura mpya kila wakati ,na juzi wananchi wangu wamekamatwa
wakawekwa ndani bila sababu za msingi na mbaya zaidi juzi kumekuwa na mgogoro
kati ya askari wa Wakala wa Misitu (TFS) na askari wa Maliasili na Utalii wa
Ushetu,nini Kauli ya Serikali na lini mgogoro huo utaenda kutatuliwa?”amehoji Cherehani
Cherehani
pia ameihoji Serikali lini itatenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya malisho ya
mifugo kwani kila siku mifugo inaendelea kuongezeka huku ardhi ikabki kuwa ni
ile ile.
“Idadi ya ng’ombe
kwa wananchi wa Ushetu inazidi kuongezeka mpaka sasa wana ng’ombe 176,000 na
wanapakana na mapori ,lakini wananchi
hawana eneo la kuchungia,lini serikali itamaliza tathimini ili wananchi wapate eneo la kulishia mifugo
yao bdala ya kuendelea kugombana baina ya wananchi na Maafisa wa Maliasili.”amehoji
Mbunge huyo
Akijibu
swali hilo Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema,Wizara yake
itawasiliana na Wizara ya Mifugo ili kuona namna ya kutenga maeneo ya mifugo.
“Kwa kuwa
Wizara imepewa dhamana ya kulinda na kuyasimamia maeneo hayo inapofika haja ya
mahitaji ya maeneo ya mifugo basi tuendelee kuwasiliana na wizara husika ili
tukae pamoja tuone namna bora ya kutenga
maeneo hayo.”
Kuhusu
mgogoro wa mipaka amesema Serikali inaendelea kuangalia namna ya kuainisha
mipaka ili kumaliza migogoro iliyopo inayotokana na mipaka.
No comments:
Post a Comment