WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA |
NA JOYCE KASIKI,DODOMA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa maesema,Serikali
imeunda Kamati ya Kitaifa inayoratibu utoaji elimu ya matumizi ya Nishati
mbadala ili nchi iweze kuondokana na matumizi ya kuni zinazosababisha ukataji
misitu hovyo.
Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijni Dodoma
kwenye maonyesho ya wiki ya Nishati,Waziri Mkuu Majaliwa amesema,kamati hiyo
itaonyesha na kutoa fursa za wajasiriamali ambao watahitaji kuingia kwenye
sekta hiyo kwa lengo la kuelimisha zaidi watanzania wabadilike kuwa na matumizi
ya Nishati mbadala .
“Na huo mbadala ni mabadala wa kuondoa matumizi
yanayosababisha kuharibika ka misitu ambayo leo hii Duniani tunakabiliana na changamoto
ya mabadiliko ya tabianchi .”amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa
“Serikali imejipanga vizuri kupitia vikao vyetu vya
awali na sasa tutakuwa na kikao kikubwa
cha Kitaifa kinachojumuisha na Serkali ya Mapinduzi Zanzibar ili eneo lote la
nchi yetu lifikiwe na elimu hiyo na waanze kutumia nishati mbadala.”
Aidha amesema,”Na kwa kuwa hatua zimeshaanza
kuchukuliwa tunataka tuimarishe eneo hilo na tuanze mara moja kwa watanzania
kutumia nishati mbadala..,kwa hiyo kamati ya Kitaifa ikiwa inaendelea kuratibu
vizuri tutatoa maelekezo kadiri tunavoypendelea.”
Ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuanza
utekelezaji wa kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya Nishati mbadala ambao pia
wataenda kuhamasisha wananchi matumizi
ya nishati mbadala katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo kwa Serikali itaanza na
taasisi za elimu ,ambazo zinalaza wasomi wake sehemu moja,lakini pia majeshi
,vyuo,kambi za wakimbizi.
“Huo ndiyo mwelekeo wa Tiafa letu na tunahitaji
watanzania ambao wamefikiwa an elimu hii waisambaze ili kujenga uelewa wa
pamoja katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi”
Ametumia nafasi hiyo kupongeza makundi mbalimbali
ya wananchi wanaojihusisha na kutengeneza mkaa kwa kutumia takataka mbalimbali huku
akisema serikali inahitaji teknolojia hiyo
iwafikie wengi ili nishati hiyo mbadala iwafikie watanzania wote na ipatikane
kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment