Umeme wa Julius Nyerere kuingizwa kwenye Grid ya Taifa

 

WAZIRI WA NISHATI JANUARY MAKAMBA


NA JOYCE KASIKI,DODOMA

SERIKALI  imesema katika mwaka ujao wa fedha inatarajia kuingiza umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kwenye Gridi ya Taifa  huku ikisema hilo ni tukio la kihistoria hapa nchini.

Aidha imesema,katika kukabiliana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme katika mwaka ujao wa fedha,ina mpango wa kufunga vituo vidogo vya kupozea umeme (substation) kila wilaya hapa nchini mradi ambao utagharimu kiasi cha shilingi  trilioni nne

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati January Makamba leo Mei 31,2023 wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 ambapo ameomba kiasi cha shilingi trilioni 3.048.

Amesema katika kipindi cha wiki moja kuanzia sasa bwawa la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  litafikisha kiwango cha ujazo kinachowezesha kuanza uzalishaji wa umeme.

Kwa mujibu wa Makamba hadi kufikia 23 Mei, 2023 kina cha maji ya Bwawa kilikuwa kimefikia mita 160.51 kutoka usawa wa bahari na ili kuweza kuzalisha umeme, kiwango cha chini cha maji kinatakiwa kufikia mita 163 kutoka usawa wa bahari.

Amesema ujazaji wa maji unaendelea kulingana na Mpango Kazi wa Ujazaji wa Bwawa ambapo hadi kufikia  23 Mei, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu ambacho ni mita za ujazo bilioni 30.

"Hadi kufikia  23 Mei, 2023 kina cha maji ya Bwawa kilikuwa kimefikia mita 160.51 kutoka usawa wa bahari na ili kuweza kuzalisha umeme, kiwango cha chini cha maji kinatakiwa kufikia mita 163 kutoka usawa wa bahari,

"Ujazaji wa maji unaendelea kulingana na Mpango Kazi wa Ujazaji wa Bwawa ambapo hadi kufikia 23 Mei, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 11.8 sawa na asilimia 39.3 ya kiwango cha juu ambacho ni mita za ujazo bilioni 30."amesema Makamba na kuongeza kuwa 

Kwa kuwa siku za nyuma kumekuwa na shaka ya masuala ya mazingira na uwezekano wa bwawa letu kujaa maji,naomba niwatangazie rasmi kwamba katika kipindi cha wiki moja kuanzia sasa tutafikia kiwango cha chini cha kuweza kuzalisha umeme ,

“Kiwango cha chini ni mita  163 kutoka usawa wa bahari na tumebakiza mita mbili kufikia kiwango hicho na tutafika huko.”amesema Makamba

Vile vile amesema,katika kipindi hicho pia  serikali kupitia Shirika la Umeme nchini TANESCO  itaanza utekelezaji wa miradi ya (CSR) miradi ya kijamii inayotokana na mikataba ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere.


Share:

Cherehani ataka kumalizwa mgogoro wa mipaka

MBUNGE WA USHETU EMMANUEL CHEREHANI

 

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MBUNGEwa Ushetu Emmanuel Cherehani (CCM) ameiomba Serikali kuingilia kati kumaliza mgogoro wa mipaka uliopo baina ya Pori la Ubagwe lililopo katika Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga na Halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ili kumaliza sintofahamu ya mipaka ya maeneo hayo miongoni mwa wananchi.

Akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma Mei 31 ,2023,Mbunge huyo amesema  Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ina mapori matatu ya Usumbwa ,Ubagwe  na Mpunzesabasabin huku akisema katika Pori la Ubagwe kuna mgogoro mkubwa na Halmashauri ya wilaya ya  Kauliua.

“Mgogoro huu umekuwa ukichukua sura mpya kila wakati ,na juzi wananchi wangu wamekamatwa wakawekwa ndani bila sababu za msingi na mbaya zaidi juzi kumekuwa na mgogoro kati ya askari wa Wakala wa Misitu (TFS)  na askari wa Maliasili na Utalii wa Ushetu,nini Kauli ya Serikali na lini mgogoro huo  utaenda kutatuliwa?”amehoji Cherehani

Cherehani pia ameihoji Serikali lini itatenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya malisho ya mifugo kwani kila siku mifugo inaendelea kuongezeka huku ardhi ikabki kuwa ni ile ile.

“Idadi ya ng’ombe kwa wananchi wa Ushetu inazidi kuongezeka mpaka sasa wana ng’ombe 176,000 na wanapakana na mapori ,lakini  wananchi hawana eneo la kuchungia,lini serikali itamaliza tathimini  ili wananchi wapate eneo la kulishia mifugo yao bdala ya kuendelea kugombana baina ya wananchi na Maafisa wa Maliasili.”amehoji Mbunge huyo

Akijibu swali hilo Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema,Wizara yake itawasiliana na Wizara ya Mifugo ili kuona namna ya kutenga maeneo ya mifugo.

“Kwa kuwa Wizara imepewa dhamana ya kulinda na kuyasimamia maeneo hayo inapofika haja ya mahitaji ya maeneo ya mifugo basi tuendelee kuwasiliana na wizara husika ili tukae pamoja tuone namna  bora ya kutenga maeneo hayo.”

Kuhusu mgogoro wa mipaka amesema Serikali inaendelea kuangalia namna ya kuainisha mipaka ili kumaliza migogoro iliyopo inayotokana na mipaka.


Share:

Semguluka ahoji ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji Mwihuzi Nyakahula

MBUNGE WA VITI MAALUM OLIVER SEMGULUKA

 

        NA JOYCE KASIKI,DODOMA              

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Serikali inatarajia kujenga skimu ya umwagiliaji katika eneo la Mwihuzi Nyakahula wilaya ya Biharamlo.

Mavunde ametoa kauli hiyo Mei 31,2023  Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye alitaka kujua lini serikali itajenga skimu hiyo ya umwagiliaji ili kuwawezesha wananchi kufanya kilimo cha umwagiliaji.

“Je ni lini serikali itajenga skimu ya umwagiliaji Mwihuzi Nyakahula wilaya ya Biharamlo”amehoji Oliva

Akijibu Mavunde amesema “Kwenye kitabu cha bajeti ya Wizara ya Kilimo Skimu ya Mwihuzi Nyakahula imetajwa kama sehemu itakayojengwa katika mwaka wa fedha ujao ,kwa hiyo  nimtoe hofu Mbunge kwamba kazi ya ujenzi wa skimu hiyo itafanyika katika mwaka wa fedha ujao.”amesema Mavunde


Share:

Mbunge Njalu ahoji ujenzi wa madaraja matano wilaya ya Itilima

MBUNGE WA ITILIMA SILANGA NJALU (CCM)

 

          NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MBUNGE wa Jimbo la Itilima Silanga Njalu (CCM) ameihoji Serikali kwamba ni lini  itajenga madaraja  matano katika Mito Galamoha , Isolo, Nyagokolwa, Mbogo na Mhuze katika wilaya ya  Itilima.

Aidha katika swali la nyongeza mbuge huyo ametaka kujua kwa nini serikali isiweke fedha za maendeleo ili wananchi waweze kujengewa daraja hilo.

Akiuliza swali Bungeni jijini Mei 30 ,2023,Mbunge huyo pia alitaka Serikali ione umuhimu wa kufungua barabara ya  Makutano-Makulija-Supaloji ambayo imebaki kilomita 51 tu .

Amesema kufungua barabara hiyo kutarahisisha shughuli za kiutalii katika wilaya ya Itilima.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi amesema,katika  Mwaka wa Fedha 2022/23, Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA)  iliajiri Mhandisi Mshauri-Chuo cha Ufundi Arusha kufanya Uchunguzi wa kijiolojia katika mto Galamoha ambapo kazi hiyo imekamilika kwa gharama ya Shilingi Milioni 35.

Aidha amesema kwa sasa TARURA inaendelea na Usanifu wa Daraja hilo kwa lengo la kupata gharama halisi za utekelezaji wa ujenzi wake.

Kuhusu  Mto Isolo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, Serikali imetenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 41 kwa ajili ya kujenga daraja la Mawe Sehemu ya

kwanza ya Mto Isolo ambapo ujenzi wa Daraja la pili katika Mto Isolo usanifu wake utafanyika katika Mwaka wa Fedha 2023/24 kwa kutumia wataalam wa ndani wa TARURA.

Kuhusu Mto Mbogo Ndejembi amesema,Serikali imetenga jumla ya Shilingi Milioni 40 katika Mwaka wa Fedha 2023/24 kwa ajili ya usanifu wa Ujenzi wa Daraja kwa tekinolojia ya upinde wa Mawe lenye ukubwa wa mita 15 ili kupata gharama halisi.

Kwa upande wa  Mto Mhuze Naibu Waziri huyo amesema,umetengewa Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kijiolojia ili kuwezesha kusanifu kwa daraja hilo.

“Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa madaraja katika Mto Galamoha , Isolo, Mbogo na Mhuze utaendelea baada ya kukamilika kwa usanifu ili kupata gharama halisi za ujenzi.”amesema Ndejembi


Share:

Serikali kutimiza ahadi ya Rais Samia kata ya Litui

 

MBUNGE WA VITI MAALUM MHANDISI STELLA MANYANYA

       NA JOYCE KASIKI,DODOMA

NAIBU Waziri,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Deogratius Ndejembi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kufika kwenye kata ya Litui  ili kufanya tathimini na kuona uhitaji uliopo ili Serikali iweze kutimiza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga kituo cha afya katika Kata hiyo.

Ndejembi ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma Mei 31 ,2023 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nyasa  Mhandisi Stella Manyanya (CCM) ambaye alitaka kujua lini Serikali itajenga kituo cha afya katika kata hiyo ili kutekeleza ahadi ya Rais Samia.

Ndejembi ametaja mambo ya kuyazingatia wakati wa tathimini hiyo ni pamoja na  idadi ya watu waliopo katika eneo hilo na kuwasilisha taarifa katika ofisi za Rais Tamisemi ili waweze kuingiza katika mipango ya ofisi hiyo ya kujenga vituo vya afya .

Aidha amesema mwaka wa fedha  2024/25  Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) inakusudia kuanza ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa kwenye vituo vya afya ambavyo vilishapokea fedha za ukarabati na ujenzi .

Akijibu swali la msingi la Mhandisi Manyanaya  (CCM)  Ndejembi amesema kuwa  jumla ya vituo vya afya 817 vinahitaji kujengewa wodi za kulaza wagonjwa kikiwemo kituo cha afya cha kihangara.

Aidha katika swali la msingi Mhandisi Manyanya  amesema kwa kuwa kituo cha afya Kihangara katika Halmashauri ya wilaya ya Nyasa licha ya kukosa wodi hasa ya akina mama lakini pia hakina  mashine ya utrasound hali inayosababisha upasuaji hasa wa akina mama wanaojifungua kwa upasuaji kupata huduma hiyo kwa kubahatisha.

Kufuatia hali hiyo Mbunge huyo ameitaka  serikali kueleza ni lini  itafikiria kupeleka mashine ya utrasaound katika kituo cha afya Kihangara ili kusaidia wananchi hususan akina mama wanaohitajika kujifungua kwa upasuaji l;akini pia ametaka kujua lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya  kujenga kituo cha afya kata ya Litui.

Hata hivyo Ndejembi amesema, Serikali itaangalia  katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha kuona kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika halmashauri ya wilaya ya Nyasa ili wahudumu waweze kununua utrasound mara moja ili kuhudumia akina mama wajawazito katika eneo la kihangala.


Share:

Majaliwa aeleza mwelekeo wa Serikali katika matrumizi ya Nishati mnadala kuokoa misitu

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

                                       


              NA JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa maesema,Serikali imeunda Kamati ya Kitaifa inayoratibu utoaji elimu ya matumizi ya Nishati mbadala ili nchi iweze kuondokana na matumizi ya kuni zinazosababisha ukataji misitu hovyo.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijni Dodoma kwenye maonyesho ya wiki ya Nishati,Waziri Mkuu Majaliwa amesema,kamati hiyo itaonyesha na kutoa fursa za wajasiriamali ambao watahitaji kuingia kwenye sekta hiyo kwa lengo la kuelimisha zaidi watanzania wabadilike kuwa na matumizi ya Nishati mbadala .

“Na huo mbadala ni mabadala wa kuondoa matumizi yanayosababisha kuharibika ka misitu ambayo leo hii Duniani tunakabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi .”amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa

“Serikali imejipanga vizuri kupitia vikao vyetu vya awali na  sasa tutakuwa na kikao kikubwa cha Kitaifa kinachojumuisha na Serkali ya Mapinduzi Zanzibar ili eneo lote la nchi yetu lifikiwe na elimu hiyo na waanze kutumia nishati  mbadala.”

Aidha amesema,”Na kwa kuwa hatua zimeshaanza kuchukuliwa tunataka tuimarishe eneo hilo na tuanze mara moja kwa watanzania kutumia nishati mbadala..,kwa hiyo kamati ya Kitaifa ikiwa inaendelea kuratibu vizuri tutatoa maelekezo kadiri tunavoypendelea.”

Ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuanza utekelezaji wa kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya Nishati mbadala ambao pia wataenda kuhamasisha  wananchi matumizi ya nishati mbadala katika maeneo yao.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo kwa Serikali itaanza na taasisi za elimu ,ambazo zinalaza wasomi wake sehemu moja,lakini pia majeshi ,vyuo,kambi za wakimbizi.

“Huo ndiyo mwelekeo wa Tiafa letu na tunahitaji watanzania ambao wamefikiwa an elimu hii waisambaze ili kujenga uelewa wa pamoja katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi”

Ametumia nafasi hiyo kupongeza makundi mbalimbali ya wananchi wanaojihusisha na kutengeneza mkaa kwa kutumia takataka mbalimbali huku akisema serikali inahitaji  teknolojia hiyo iwafikie wengi ili nishati hiyo mbadala iwafikie watanzania wote na ipatikane kwa urahisi.

Share:

Gekul aagiza uchunguzi wa rushwa gereza la Babati Mjini

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul  akisikiliza kesi ya mahabusu Mwajuma Mada aliyefika gerezani Babati mjini  ikiwa ni sehemu ya msaada unaotolewa na timu ya wataalam wa Mama Samia Legal Aid Campaign

Timu ya wataalamu na uongozi wa gereza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kazi hiyo ya kutoa msaada wa kisheria kwa watu walio vizuizini.


       NA LUSAJO MWAKABUKU-WKS MAYARA

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameuagiza Uongozi wa Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Manyara pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mahabusu na Wafungwa wa gereza la Babati Mjini dhidi ya askari na watumishi wa vyombo hivyo vya haki ambapo katika nyakati tofauti wameonekana kutumia nafasi zao kudai rushwa kwa malengo ya kukwepesha haki.

Tuhuma hizo zimetolewa tarehe 24/05/2023 wakati timu ya wataalam wanaoendesha Mama Samia Legal Aid Campaign ikiongozwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ilipofika gerezani hapo kwa lengo la kutoa elimu pamoja na msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hiyo kubwa iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwaka huu ambayo itadumu kwa miaka mitatu mpaka 2026.

Akiambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mashtaka, Tume ya haki za binadamu, Mrakibu wa Polisi wa Mkoa, Dawati la jinsia la polisi, Wanasheria na watumishi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Naibu Waziri Gekul alifika katika gereza la Babati na kufanikiwa kuongea na uongozi lakini pia na wafungwa na mahabusu waliokuwepo katika gereza hilo lengo likiwa ni kubaini changamoto za kisheria zikiwemo upatikanaji wa dhamana kwa wafungwa wanaostahili pamoja na namna kesi zao zinavyoendeshwa.

Timu ya wataalam wa Mama Samia Legal Aid Campaign ilipokewa na uongozi wa Gereza hilo ambapo pamoja na mambo mengine, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Nkonge Edwin alimweleza Naibu Waziri kuwa moja kati ya vitu ambavyo gereza hilo limefanikiwa kuvitekeleza ni pamoja na kesi kusikilizwa kwa wakati kitu ambacho ni kilio kwa watu wengi walio vizuizini katika maeneo mengine huku akiainisha kasoro ndogondogo zikiwemo uchakavu wa vyombo vya usafiri katika kutoa huduma za wafungwa pamoja na kukataliwa kwa rufani zilizo nje ya muda.

Timu hiyo ya Mama Samia Legal Aid Campaign baada ya kuongea na uongozi wa Gereza iliingia ndani ya gereza na kuongeza na mahabusu pamoja na wafungwa ambapo elimu ya sheria ilitolewa jinsi mtu anavyokamatwa kituoni mpaka anapelekwa gerezani vitu vinavyotakiwa kufuatwa.

 Lakini pia mtaalam kutoka haki za binadamu alielezea haki za msingi za wafungwa wakiwemo gerezani ikiwemo haki ya dhamana kwa makosa yenye dhamana na pia Ofisa kutoka Ofisi ya Mashtaka akaongelea wajibu wa Ofisa wa mashtaka wa wilaya na muda uliopangwa kisheria wa kushughulikia kesi za watu walio vizuizini ambapo kwa kwa mkoa huu hali imeonekana kuwa shwari kwani hakuna mfungwa au maabusu aliyelalamika kupitilizwa muda wa siku 90 wa kusomewa shitaka lake mara wanapowekwa vizuizini kwa mujibu wa sheria.

Ilipofika wakati wa maswali, wafungwa na mahabusu walianza kwa kubainisha changamoto zao wanazokumbana nazo kupitia risala iliyosomwa na Mahabusu Michael Marko ambayo pamoja na mengine ilielezea changamoto ya ucheleweshaji wa upelelezi wa kesi unakopelekea mrudikano wa mahabusu gerezani.

 Ucheleweshwaji wa akala za hukumu kwa watu ambao wameshahukumiwa, Kuporwa fedha wakati wakikamatwa na polisi na pia wakasema kumekuwa na kawaida ya mahabusu kukamatwa na kuachiwa huku pia wakiituhumu Ofisi ya Mashtaka kutokuleta mashahidi kwa wakati.

Hali ikazidi kubadilika mara baada ya wafungwa na mahabusu hao kupewa nafasi ambapo bila kusita wala uoga waliwataja maaskali na maofisa upelelezi pamoja na makarani wa mahakama kwa majina ambao waliwapora fedha wakati wakikamatwa na wengine kuwataka walipe ili kesi zao zisiendelee. 

Na pia mahabusu na wafungwa hao walieleza kuwa walitakiwa kutoa hela zilizoanzia milioni mbili na kuendelea ili waachiwe wakati mahabusu mwingine akidai askari alimwambia mke wake atoke Singida aje alale Manyara na siku ya pili mumewe ataachiwa (Akiashiria rushwa ya ngono)

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Naibu Waziri aliwaagiza viongozi wa polisi pamoja na wa Ofisi ya Mashtaka alioambatana nao kuhakikisha kuwa wale wote waliotajwa katika tuhuma hizo uchunguzi wa kina unafanyika na wale wote watakaobainika kuwa wametumia mamlaka yaka yao vibaya basi hatua kali za sheria zichukuliwe dhidi yao na pia akawaagiza viongozi ha kuhakikisha wana jitihada za upatikanaji wa haki kwa mahabusu na wafungwa hao unapatika kwa wakati na bila usumbufu.


Share:

JKT laita vijana makambini,lachukua wote walihitimu kidato cha sita mwaka huu

MKUU wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena 

 

              NA JOYCE KASIKI,DODOMA 

JESHI la Kujenga Taifa (JKT)  limewataka vijana wote waliohitimu elimu ya kidato cha sita kwa mwaka 2023 kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujibu wa sheria 2023.

Aidha Jeshi hilo limesema,miundombinu ya Jeshi hilo limejiandaa vyema kwa kuwa na miundombinu ya kutosha kwa ajili ya kuwapokea vijana hao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya JKT Chamwino mkoani Dodoma kuhusu wito huo wa vijana Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema, vijana hao wanapaswa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa kuanzia Juni Mosi  hadi Juni 11 mwaka huu.

“Vijana hao wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma –Mara,JKT Msange –Tabora,JKT Ruvu Pwani,JKT Mpwapwa ,Makutupora JKT-Ddpdpma,JKT Mafinga –Iringa,JKT Mlale-Ruvuma ,JKT Mgambo na JKT Maramba –Tanga .”

Ametaja kambi nyingine kuwa ni “JKT Makuyuni-Arusha,JKT –Bulombora,JKT Kanembwa na JKT Mtabila za Kigoma,JKT Itaka Songwe,JKT Luwa na JKT Milundikwa –Rukwa,JKT Nachingwea-Lindi,JKT Kibiti –Pwani na Oljoro JKT Arusha.”

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mabena wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Aidha amesema,orodha kamili ya majina ,makambi waliyopangiwa na mahitaji yote yanayohitajika vinapatikana kwenye tovuti ya JKT www.jkt.go.tz.


Share:

Serikali yaweka wazi mpango wake wa kudhibiti wizi wa dawa

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT.GODWIN MOLLEL

 

             NA WAF- BUNGENI DODOMA

 NAIBU  Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameweka wazi kuwa, Serikali imepanga kuchukua hatua kali kwa wote wataobainika kwenye upotevu wa dawa ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ovu ambayo inawanyima wananchi haki yao ya msingi ya kupata huduma hiyo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini. 

Dkt. Mollel amesema hayo leo Mei 23, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa Luhaga  Mpina katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha 31, Bungeni Jijini Dodoma. 

Amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya iliona dalili za upotevu wa Bilioni 83 hivyo kushirikiana na TAKUKURU ili kuhakikisha wote wataobainika kuwepo katika upotevu huo wa dawa wanachukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia hiyo.

Dkt.Mollel amesema, Serikali imefanya mikakati mbalimbali katika kutatua tatizo la wizi na ubadhilifu wa dawa na vifaa tiba ikiwemo kufanya suala la upotevu wa dawa na vifaa tiba kama agenda katika vikao vya Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya.

Aidha amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa bidhaa za Afya ikiwemo kufunga mifumo ya kielectroniki pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa bidhaa hizo.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Wizara kwa kushirikiana na OR TAMISEMI imeendelea kuimarisha kamati za usimamizi za vituo kwa kuzijengea uwezo kuhusu majukumu yao katika usimamizi wa bidhaa za Afya.

 Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amesema, Wizara imeendelea kutoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wabunge kushiriki katika upokeaji wa bidhaa hizo na taarifa zote wapewe ili kujenga uwazi zaidi juu ya bidhaa hizo za afya.

 Aidha, Dkt. Mollel amesema suala la kupambana dhidi wizi na ubadhilifu wa bidhaa za Afya siyo la Serikali pekee bali ni suala la kushirikiana pande zote, hasa wawakilishi wa wananchi.

Share:

SUMAJKT yazindua mitambo ya kisasa ya kuzalisha zege

 

 

PICHAI ni mitambo ya kualiha zge iliyozinduliwa jijini Dodoma na Mkuu wa  Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele 


MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja  Jenerali Rajabu Mabele akizungumza jijini Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa magari na mitambo ya kzualisha zege.


            NA MWANDISHI WETU DODOMA

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Meja Jenerali Rajabu Mabele amelitaka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kuhakikisha linafanya kazi kwa weledi ili kuendelea kuwapa imani wadau wanaowapa kazi kwamba wanaweza kufanya kazi zao kwa viwango vinavyokubalika na kwa ubora zaidi.

Akizungumza mei 23 mwaka huu jijini Dodoma wakati akizindua magari na Mitambo ya kuzalisha zege katika eneo la Mwangaza jijini hump,Meja Jenerali  Mabele amesema  kutokana na imani hiyo lazima kazi zifanyike kwa viwango vinavyotakiwa ili kutunza uaminifu huo.

Ametumia nafasi hiyo kusihukuru Serikali  ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliamini shirika hilo kwa kulipa kazi huku akiahidi kuendelea kununua vifaa vya kisasa ili kufanya kazi zenye ubora zaidi.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kuendelea kutuamini na kutupa kazi  na ndiyo maana mnaona na sisi tunapambana  ili kuhakikisha tunakuwa na mitambo ili tuweze kuzitekeleza kazi hizo kwa ufasaha,kwa wakati na vizuri zaidi.”amesema Meja Jenerali Rajab Mabele  na kuogeza kuwa

“Kwa imani hii tunayopewa na Serikali,watendajiwote wa SUMAJKT lazima tuonyeshe kwamba wale wanaotuamini hawajakosea,kwa hiyo tufanye kwa kazi kwa bidii ili kuhakikisha imani ile ile tunayopewa na sisi tuendelee kuonyesha kwamba tupo tayari kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya serikali ,tufanye kazi kwa wakati,kazi zenye viwango kama ambavyo tunafanya siku zote tuendelee kuwa na bidii  katika majukumu yetu ya kila siku.”

Aidha ametaka mitambo hiyo itunzwe kwa kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara kila inapohitajika na kwa wakati muafaka ili iendelee kuwa endelevu la kuleta faida ndani ya shirika na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Petro Ngata amesema, tukio hilo ni moja ya utekelezaji wa mikakati yao waliyojiwekea ya kuongeza mitambo na vitendea ili kujiongezea uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Awali akitoa taarifa ya mtambo huo Mkurugenzi Mwendeshaji kampuni ya Ujenzi SUMAJKT  Injinia Mogan Nyoni amesema vifaa vilivyozinduliwa vimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.349 huku akisema  zoezi la usimikaji hadi kufikia Mei 22 mwaka huu  lilikuwa limefikia asilimia  95.

“Kukamilika kwa usimikaji wa mitambo hiyo utaongeza kipato cha kampuni ya ujenzi na shirika kwa ujumla kwani hitajio la zege jijini Doodma ni kubwa lakini pia kutaongeza imani za kiutendaji kutoka kwa washitiri  kutokana na kazi ambazo SUMAJKT na kampuni ya Ujenzi inafanya .”alisema Injia Mogan

Kwa upade wake Mwenyekiti wa Bodi SUMAJKT amesema ,mitambo hiyo itaongeza thamani katika shirika kutokana na ubora wa bidhaa zinazozalishwa,urahisi wa upatikanaji wake ,gharama za uzalishaji kupungua  lakini pia muda wa uzalishaji utapungua.

 

Share:

Magonjwa ya mlipuko kujengewa kituo maalum

 

NAIBU Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akijibu swali Bungenijijini Dodoma  leo Mei 22,2023/2024


                                     NA WAF -  BUNGENI DODOMA 


NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga hekali 90 kwaajili ya ujenzi wa kituo maalumu cha magonjwa ya mlipuko (isolation center) ikiwemo ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera kutokana na mwingiliano na wananchi kutoka nchi jirani na Mkoa huo.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Mei 22, 2023 wakati akijibu swali la Mhe. Bernabetha Kasabago Mushashu katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha 30, Bungeni Jijini Dodoma. 

"Tumeshapata heka 90 ndani ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kujenga Isolation center itayosaidia katika matibabu ya magonjwa ya mlipuko yatayoweza kujitokeza nchini." Amesema Dkt. Mollel. 

Amesema,  Sambamba na kujenga kituo hicho kitacho kitachosaidia kuwatenga wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko, Serikali itaendelea kuboresha huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kutenga zaidi ya Bilioni 4 ili wananchi wa mkoa huo na nchi jirani waendelee kunufaika na huduma hizo. 

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imekamilisha hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa ujenzi wa jengo la huduma za dharura (EMD) ambalo limegharimu shilingi milioni 560,000,000, jengo la uangalizi maalum (ICU) shilingi milioni 650,000,000, jengo la huduma za Mionzi (Radiology) shilingi milioni  237,000,000, nyumba ya mtumishi shilingi milioni 90,000,000.

Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amesema, pamoja na kuboresha miundombinu katika  hospitali  hiyo Wizara imefanya ununuzi na ufungaji wa mashine ya CT Scan ambayo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1,810,000,000 na tayari huduma zimeanza kutolewa katika hospitali hiyo.

Share:

Mikakati ya Serikali kulifanya ATCL kuwa shindani katika soko yaanikwa

 



WAZIRI wa Ujeniz na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma 

             

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

SERIKALI imebainisha mikakati yake ya kuhakikisha Shirika la Ndege la ATCL kuwa shindani katika soko duniani huku Kamti ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiitaka kuchukua hatua kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya sekta ya ujenzi kwa viwango vya chini kuchukuliwa hatu za kisheri ana kinidhamu.

Hayo yamesemwa leo Mei 22,Bungeni jijini Dodoma na Wazazi wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha wa 2023/2024.

Amesema,miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na ATCL kujihudumia yenyewe kwa kuhudumia abiria, mizigo, na ndege kiwanjani, kufanya matengenezo makubwa na madogo kwa ndege zote.

“Vile vile kuongeza uwezo wa kutoa mafunzo nchini kwa marubani, wahandisi wa ndege na wahudumu wa ndege kwa kushirikiana na vyuo vya ndani.

Kwa mujibu wa Waziri huyo ,ili kutekeleza mikakati hiyo, Serikali imeendelea kuiwezesha ATCL kuendelea na ukarabati na maboresho ya karakana kubwa ya matengenezo ya ndege iliyopo Mkoani Kilimanjaro ambayo imefikia asilimia 85.

“Ukarabati huu umeiwezesha ATCL kufanya matengenezo ya kiwango cha “C Check” kwa ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Dash 8 Q400 na kufanya matengenezo yote madogo madogo kwa ndege zake zote. 269.

“Mikakati mengine inayotekelezwa na ATCL ni kuajiri na kuwaendeleza watumishi katika kada maalum ambazo ni pamoja na Urubani na Uhandisi mbapo hadi kufikia Aprili, 2023 ATCL iliajiri marubani tisa na hivyo kufanya jumla ya marubani kuwa 108. “alisema Prof.Mbarawa

Aidha alisema, ATCL inatarajia kuajiri wahudumu wa ndege 43 na hivyo kufanya jumla ya wahudumu wa ndege kufikia 164. Watumishi wa kada nyingine zilizobaki wameongezeka hadi kufikia 389 ikilinganishwa na watumishi 382 waliokuwepo Juni, 2022.

Alisema,ongezekeo hilo la watumishi limefanya ATCL 111 kuwa na watumishi 792 ikilinganishwa na watumishi 613 katika mwaka 2021/22.

Akitoa maoni ya ya jumla ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Moshi Kakoso ameitaka Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwepo na uwajibikaji wa watendaji na  makandarasi katika miradi yote  ambayo imetekelezwa au itatekelezwa chini ya viwango kwa kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa wahusika .

Aidha Kamati hiyo imeishauri Serikali kuhakikisha miradi ya wizara hiyo inazingatia viwango na ubora kwani ni miradi inayogharimu fedha nyingi.

Share:

Watanzania pimeni figo mara kwa mara kuepuka gharama za matibabu

 



NAIBU Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akijibu swali Bungeni jijini Dodoma leo Mei 19,2023.

NA WAF- Bungeni Dodoma 

                  

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amebainisha kuwa, asilimia 7 ya Watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo huku akiwataka  wananchi kupima ugonjwa huo mara kwa mara ili kuepuka madhara yake makubwa ikiwemo gharama kubwa ya matibabu yake.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Mei 19, 2023 wakati akijibu swali la Mhe. Asia Abdukarimu Halamga katika Mkutano wa kumi na moja kikao cha 29, Bungeni Jijini Dodoma. 

Ameendelea kusema kuwa, ugonjwa huu, kwa kiasi kikubwa unahusishwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa kisukari na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Amesema, Katika kujali afya za Watanzania wakiwemo wenye ugonjwa wa figo, Serikali ya Rais Samia imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 290.9 kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali za mikoa, katika vifaa hivyo vipo vifaa vya matibabu ya kusafisha damu (dialysis) kwa wagonjwa wa figo.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Serikali ipo katika mpango wa kuona namna ya kupunguza gharama ya matibabu ya figo kupitia huduma ya kusafisha damu ili wananchi wenye uhitaji waweze kunufaika na huduma hizo, huku akiweka wazi kuendelea kuwatazama wasio na uwezo kabisa kupitia njia ya misamaha.

Sambamba na hilo Dkt. Mollel ameendelea kusisitiza kwa kuwataka Wabunge kuwa mabalozi wazuri wa kuiunga mkono Bima ya Afya kwa wote kwani ndio suluhisho la kudumu la matibabu ya magonjwa yote na huduma bora kwa kila Mtanzania kwa ngazi zote kuanzia zahanati mpaka hospitali ya Taifa.

 


Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.