TANZANIA YAPIGIWA MFANO, KUKABILI MAAFA, MATUMIZI SAFI YA NISHATI YA KUPIKIA YATAJWA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App




NA. MWANDISHI WETU- WINDHOEK

Serikali ya Tanzania imeendelea kuonesha umahiri wake katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini kwa kuzingatia mifumo sahihi ya kukabiliana na maafa na matumizi ya teknolojia ya kisasa pamoja na miongozo, kanuni na sheria mbalimbali zinazoongoza katika uratibu wa maafa hayo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Viongozi  kuhusu masuala ya kupunguza athari za maafa pamoja na Kikao cha Tisa cha Jukwaa la Kanda la Afrika la Kupunguza Athari za Maafa na vilivyofanyika jijini Windhoek nchini Namibia   kwa muda wa  siku nne kuanzia Oktoba 21 hadi 24 2024.

Mhe.Nderiananga ameeleza kuwa, uwekezaji mkubwa umefanywa na Serikali ya Tanzania hususan katika kuhakikisha teknolojia inavusha Taifa katika kukabili maafa ambapo Serikali ilianzisha Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga  katika Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura nchini Tanzania ambacho kimeifanya nchi  kuwa mahiri katika masuala ya menejimenti ya maafa hususan katika kuzuia, kupunguza kujiandaa na kukabili maafa pindi yanapotokea.

Katika hatua nyingine Mhe.Nderiananga amezungumzia kuhusu mkakati wa miaka kumi wa Nishati safi ya Kupikia ambao utekelezaji wake umeanza mwaka 2024 hadi 2034,  ameeleza kuwa unalenga kuhifadhi mazingira, kulinda afya kwa kuzuia matumizi ya kuni na mkaa ili kuepuka athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“Suala ya mabadiliko ya tabia nchi linaathiriwa na ukataji wa miti inayopelekea uharibifu mkubwa wa mazingira na kuchagiza ukosefu wa mvua za kutosha, uwepo wa ukame unaoathiri uzalishaji wa chakula, tunampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzindua mkakati huo,”alisema

Amesema moja ya mikakati ambayo Tanzania imejiwekea ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.

"....Kama nchi tumejipanga kuhakikisha Taasisi za Serikali na Mashirika binafsi yanawekeza ipasavyo katika matumizi ya nishati safi kwa maslahi mapana ya mazingira safi na salama, Afya zetu na Afrika kwa ujumla " amesisitiza Mhe.Nderiananga

Kufuatia hatua huyo Mhe.Nderianga ametoa  wito kwa Mataifa mbalimbali duniani kufuata nyayo za Tanzania kwa kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya muda mfupi na mrefu ya Nishati safi ya Kupikia ili kuifanya Dunia kuwe mahali safi na salama pa kuishi.

Awali akifungua mkutano huo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Kazi na Uchukuzi Nchini Namibia Mhe. John Mutorwa amesema mikutano hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo awamu hii imefanyika nchini Namibia na kuwakutanisha wadau zaidi ya elfu moja wa  maafa kwa nchi za Afrika  wakiwemo wataalamu kutoka  katika ngazi za kitaifa, Serikali za mitaa, Mashirika ya Umoja wa Kitaifa na Kimataifa, Asasi za Kiraia, sekta binafsi, taasisi za elimu na utafiti na wanahabari, na hii imetajwa kuwa ni mafanikio makubwa kwa bara la Afrika.

“Tunashukuru kwa namna nchi zilivyojitokeza kushiriki mikutano hii muhimu katika kuhakikisha masuala ya maafa yanakabiliwa na kuwa na Afrika stahimilivu katika maafa, tunawashukuru sana Mawaziri mlioweza kushiriki mikutano hii, nasi tumepata heshima kama nchi, na tunaahidi kuendelea kuimarisha mashirikiano yetu kama Bara la Afrika,”alisema Mhe. Mutorwa

Aidha, alitoa rai kwa kila nchi kuona umuhimu wa kujipanga kukabili maafa bila kujali utofauti na hali za Mataifa ya Afrika, lengo kuyafikia na kuyaishi malengo na kuwa tayari kusimamia masuala haya.

“Maafa si jambo la kulifurahia, yanapaswa kupewa mwitikio mkubwa na mikakati yenye mashiko na inayotekelezeka lengo ni kulinda jamii zetu na kuweza kuifanya Dunia sehemu salama ya kuishi,hili litafanikiwa tukiendelea kushikamana kwa umoja wetu wa Afrika” alisisitiza



Share:

TANZANIA YARIDHISHWA NA USHIRIKIANO ULIOPO NA NCHI YA NAMIBIA 

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App




  NA. MWANDISHI WETU – WINDHOEK NAMIBIA

Tanzania itaendelea kuimarisha misingi ya uhusiano wa diplomasia baina yake na nchi ya Namibia katika kuimarisha mahusiano yaliyopo katika nyanja mbalimbali huku mchango wa Tanzania katika uhuru wa Namibia ukitajwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga mapema 24 Oktoba, 2024 alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia, ambapo aliambatana na watendaji wa ofisi hiyo kwa lengo la kushiki Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Viongozi (High Level Meeting) kuhusu masuala ya kupunguza athari za maafa pamoja na Kikao cha Tisa cha Jukwaa la Kanda la Afrika la Kupunguza Athari za Maafa na vitakavyofanyika Windhoek nchini Namibia. Mikutano hiyo itafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 24 Oktoba, 2024.

Mhe. Ummy ameeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na uongozi makini, na mahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna anavyojipambanua kidiplomasia na kuhakikisha mahusiano ya Taifa na nchi nyingine unakuwa wenye manufaa na kuiletea nchi heshima katika nyanja mbalimbali.

“Hakika Tanzania imeendelea kuwa kitovu cha amani na utulivu, hii imetokana na uongozi mahiri wa Mhe.Rais Dkt. Samia kwa miongozo na maelekezo yake katika kuhakikisha nchi inaendelea kujipatia maendeleo,”amesema Mhe. Ummy

Aidha, katika mazungumzo na mwenyeji wake ambaye ni Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Namibia Bw. Elias Tamba ameeleza kuwa, nchi ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Namibia katika masuala mbalimbali kwa kuzingatia urafiki uliopo baina ya Mataifa hayo mawili toka kipindi ya Uhuru wa Namibia ambapo Tanzania inakumbukwa kwa mchango wake.

Bw. Tamba ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendelea kuhakikisha inaimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina yake na Namibia huku akizitaja fursa za kimaendeleo kwa taifa hilo ikiwemo masuala ya kibiashara.

Ujumbe wa Tanzania nchini Namibia umeongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiwa ameambatana na Timu yake  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akiwemo Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo,  Dkt.Jim Yonazi, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi hiyo Brig. Jenerali Hosea Ndagala, Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo pamoja na Bw. January Kitunsi.


Share:

𝗡𝗔𝗜𝗕𝗨 𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗔𝗜𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗲-𝗚𝗔 𝗞𝗨𝗜𝗠𝗔𝗥𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗨𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜𝗔𝗡𝗢 𝗡𝗔 𝗦𝗘𝗞𝗧𝗔 𝗕𝗜𝗡𝗔𝗙𝗦𝗜

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App




Na Mwandishi wetu ,eGA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deus Sangu  ameitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, ili kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wabunifu kwenye eneo la TEHAMA.

 Sangu ametoa rai hiyo hivi karibuni, wakati akifunga programu ya awamu ya sita ya mafunzo kwa vitendo (practical training) kwa mwaka wa fedha 2024/2025, inayoendeshwa na e-GA kupitia Kituo chake cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (e-GovRIDC) jijini Dodoma.

"Naipongeza e-GA kwa kazi nzuri mnayofanya ya kukuza vipaji na kuongeza uwezo kwa vijana katika matumizi ya TEHAMA, lakini pia nawashauri kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kutoa fursa kwa wanafunzi wanaoshiriki mafunzo kwa vitendo pamoja na mafunzo kazini katika kituo hiki kupata fursa za ajira ", alisema Mhe. Sangu. 

Amesema kuwa, ushirikiano kati ya e-GA na sekta binafsi utaongeza tija katika kukuza na kuimarisha tasnia ya TEHAMA, na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana na hatimaye kupunguza changamoto ya ajira kwa taifa.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni, baadhi ya taasisi binafsi zikiwemo Benki na Kampuni za Simu za Mkononi, zilitembelea kituo hicho na kuonesha nia ya kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano (MOU) katika masuala ya elimu, utafiti, na ubunifu wa TEHAMA, ikiwa ni hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya e-GA na taasisi hizo.

“Nimetembelea miradi ‘projects’ mbalimbali zinazoendelea katika kituo hiki na nimeona kazi kubwa ambayo e-GA mnaifanya ya kuwaandaa vijana wetu, ili waweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia mpya zinazoibukia kama vile Akili Mnemba ‘Artificial Intelligence- AI’, ‘Machine Learning, ‘Blockchain’ na Sarafu ya Kidijitali ‘Digital Currency’ na nimeona jinsi vijana wetu walivyo na uwezo mkubwa katika maeneo hayo”, amesema Sangu. 

Aidha, ameipongeza e-GA kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vijana wanajifunza teknolojia mpya zinazoibuka duniani, ili waweze kufanya bunifu mbalimbali za TEHAMA ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifumo ya kielektroniki kupitia teknolojia hizo itakayosaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi Serikalini na utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Mafunzo haya mnayoyatoa yanawasaidia wanafunzi kuongeza ujuzi na uzoefu katika kuzielewa teknolojia mpya ili kuchochea maendeleo na mageuzi makubwa ya Serikali ya kidigitali, na hivyo kuwa na kizazi chenye ujuzi wa kutosha kuhusu TEHAMA na hatimaye kushiriki katika kuijenga Serikali ya Kidijitali”, alifafanua Mhe. Sangu. 
                                                                                                                                
Alibainisha kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi na kuijengea uwezo Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ili kuhakikisha matumizi ya TEHAMA Serikalini yanazidi kuimarika sambamba na kuandaa vijana mahiri katika TEHAMA ili washiriki katika ujenzi wa Serikali ya Kidijitali.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mhandisi Benedict Ndomba, aliahidi kuendeleza na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, pamoja na kuwajengea uwezo vijana katika TEHAMA ili kutoa fursa kwa vijana kuonesha uwezo wao katika TEHAMA na kuweza kushindana katika soko la ajira duniani. 

“e-GA itaendeleza ushirikiano na sekta binafsi pamoja na Vyuo Vikuu mbalimbali ili kuwajengea uwezo vijana katika eneo la TEHAMA, lakini pia kuwawezesha kushindana katika soko la ajira duniani na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumesaidia kupunguza changamoto ya ajira nchini”, alisisitiza Ndomba.

Akizuzungumza kwa niaba ya wanafunzi walioshiriki program hiyo, Bw. Philemon Mbunda ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ameishukuru  e-GA kwa kupata fursa ya kushiriki katika programu hiyo ambayo imewasaidia kuongeza ujuzi na uzoefu katika kuzifahamu teknolojia mpya zinazoibukia.
“Tumekuwa hapa kwa muda wa wiki kumi na tumejifunza mambo mengi kuhusu teknolojia zinazoibukia na namna tunavyoweza kuzitumia katika kubuni mifumo mbalimbali itakayoleta tija kwa taifa letu, tunaahidi kuwa mabalozi wazuri na kuhakikisha elimu tuliyoipata hapa tunaiendeleza kwa vitendo”, alisema Bw. Philemon.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), huendesha programu ya mafunzo kwa vitendo kila mwaka ambapo, huchukua vijana kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo katika TEHAMA na kuweza kushindana katika soko la ajira, ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wanafunzi 65 kutoka Vyuo Vikuu 12 walishiriki programu hiyo kwa muda wa wiki 10.
Share:

Wakulima sasa kutambuliwa kibiashara


Published from Blogger Prime Android App




      Na Joyce Kasiki,DODOMA


WAKALA  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umejipanga kuanza kuwasajili Wakulima kwa kuwapa nembo ambayo itawatambulisha kibiashara.

Afisa Usajili wa BRELA Gabriel Giranangay ameyasema hayo  katika  maonesho ya Wakulima (88) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Wakala huo.

Amesema BRELA inawasaidia wakulima kusajili biashara zao rasmi ili kuwa na usajili wa kampuni, ushirika, au biashara ndogo ndogo zinazohusiana na kilimo na hivyo kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.

Aidha amesema usajili wa alama za Biashara  ni muhimu kwa wakulima kulinda jina la bidhaa zao .

Gabriel amesema BRELA hutoa huduma hizo ili kuhakikisha biashara za kilimo zinakubalika kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za ushauri kuhusu jinsi ya kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya kilimo, ikiwa ni pamoja na kanuni za usajili, sheria za biashara, na masharti ya leseni.


"Kwa hiyo mchango wa BRELA ni kuhakikisha inachangia katika kuhakikisha kuwa wakulima wanapata huduma zinazohitajika ili kuendesha shughuli zao za kilimo kwa njia rasmi na kisheria, " amesema

Amesema lengo la BRELA ni kurahisisha mchakato wa usajili, kutoa huduma za leseni, na kuhakikisha kuwa biashara zinakubaliana na sheria na taratibu za nchi.


Aidha amesema huduma kuu zinazotolewa na BRELA ni pamoja na Usajili wa Kampuni,Kusajili kampuni, mashirika, na ushirika ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo na ushauri kuhusu sheria za biashara na taratibu za kisheria.

Xxxxx
Share:

Watakaofanya ununuzi nje ya Mfumo wa NeST kufungwa jela

Published from Blogger Prime Android App



Na Mwandishi Wetu


WATUMISHI wa Serikali watakaofanya ununuzi wa Umma nje ya Mfumo wa NeST watakuwa wamefanya kosa la jinai, na kukabiliwa na adhabu ya kifungo jela pamoja na kulipa faini, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023.

Akizungumza kwenye kipindi maalum cha Tenda Radio, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Wakili Paul Kadushi, amewataka viongozi wa taasisi za serikali na watumishi kwa ujumla kuzingatia matakwa ya sheria hiyo iliyoanza kutumika Juni 17, 2024 na kanuni zake ambazo zimeanza kutumika Julai 1, 2024.

Kadushi amefafanua kuwa sheria iliyofutwa haikuweka ulazima wa kutumia mfumo wa kielektroniki kufanya ununuzi, hatua iliyosababisha taasisi nyingi kufanya ununuzi nje ya mfumo. 

“Lakini kwa sheria hii mpya [Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023] sasa imeweka sharti la lazima kwa taasisi nunuzi zote kutumia mfumo wa kielektroniki katika kufanya ununuzi,” Wakili Kadushi aliiambia Tenda Radio.
Share:

Kanda ya Kati wakiwa na kampeni ya Sako kwa Bako

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dodoma
Afisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Mtandao wa Tigo Tanzania Isaac Nchunda amesema kampuni hiyo ni moja ya mitandao inayokua kwa kasi na hivyo kurahisisha maisha ya watanzania .

Akizungumza katukanofusi za Tigo jijini Dodoma na waandishi wa habari leo Agosti Mosi,2024 Nchunda amesema katika kuhakikisha kampuni ya Tigo inaendelea kurahisisha maisha ,imepeleka kampeni ya SakoKwaBako ambayo sasa ina miezi miwili tangu ianzishwe.

"Leo tigo ipo kanda ya kati na tumewaletea kampeni ya SakoKwaBako  ambayo sasa ina miezi miwili, ikiwa Kanda ya kati Dodoma Makao Makuu ya nchi na ni siku nzuri ambayo usafiri wa reli ya mwendokasi (SGR) imezinduliwa ,tigo ndiyo mtandao bora zaidi Tanzania kwa sababu tuna teknolojia ya karne ya hivi sasa ya 4G na 5G ,

"Na hapa Dodoma tunayo 5G hivyo tunatoa huduma nzuri kwa wateja wanaotumia mtandao wa Tigo ambapo wanafurahia huduma yenye kasi zaidi ya 5G."amesema Isaac
Amesema SakoKwaBako inatoa bonasi kwa kila mteja  anayenunua bando la tigo anapata MB na dakika za bure.
Amewaasa wananchi wajiunge zaidi na mtandao huo ili wanaufaike na ofa hizo ambapo pia ameizungumzia kampeni yao kupitia simu aina ya ZTE A34 ambapo amesema hiyo ni simu ya kisasa na inapatika kwa unafuu zaidi.
"Simu hii inauzwa shilingi  180,000 lakini pia inatolewa kwa mkopo ambapo mteja atatanguliza kiwango cha awali cha sh.35,000 na atalipa sh.650 kwa siku hadi mteja atakapomaliza deni lake na wakati huo huo anaendelea kutumia simu yake kabla hata ya kumaliza deni lake."amesisitiza

Akizungumzia kuhusu huduma za tigo kwa ujumla amesema, kampuni hiyo inahudumia wateja zaidi ya milioni 21 huku akisema hiyo ni kwa sababu ya ubora wa huduma zake.

"Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na kwamba Tigo ndiyo mtandao unaokua kwa kasi zaidi nchini. "Amesema

Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo Kanda ya Kati Said Iddy amesema kufuatia umuhimu wa uwepo wa Reli ya SGR ,wananchi wanapaswa kutumia mtandao wa Tigo kwa ajili ya kukata tiketi ya treni hiyo.

Amesema kampuni hiyo imefanya maboresho makubwa ya mtandao wake kwa ajili ya kuboresha mtandao na biashara kwa ujumla kwa kutumia mtandao wa tigo.

Pia amesema Tigo inashiriki maonesho ya wakulima na wafugaji (88 ) viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma huku akiwasihi wananchi wote kutembelea banda la tigo kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

Share:

Mkongo wa Taifa unavyorahisisha mawasiliano nchi nzima



Published from Blogger Prime Android App
Mkurugenzi wa T-Pesa Lulu Mkudde akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kwenye maoneaho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam .



Na Joyce Kasiki Dar Es Salaam 


SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL) limesema ,hadi sasa limesambaza mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini huku zaidi ya wilaya 98 nazo zikiwa zimefikiwa na mkongo huo ambao unarahisisha mawasiliano na kuleta matokeo chanya kwenye shughuli za kiuchumi

Hayo yamesemwa leo Julai 12 na Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL Pesa Lulu Mkudde wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya  Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika hilo.

Amesema juhudi hizo zote zinalenga katika upatikanaji wa huduma za elimu ,afya na maendeleo kwa ujumla yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini .

Amewahakikishia wananchi kwamba TTCL itahakikisha huduma za mawasiliano zinakuwa nzuri ili kuwapa fursa wananchi kupata huduma mbalimbali  lakini nao kujiingizia kipato kupitia mtandao bora wa TTCL kwa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Mkudde Mkongo wa Taifa ni moja ya miradi ya kimkakati inayofanywa na TTCL huku akiitaja miradi mingine kuwa ni  kutoa mafunzo mbalimbali , kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu.

Kuhusu ushiriki wao kwenye maonesho hayo amesema,katika kuunga mkono kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu isemayo Tanzania ni mahalo sahihi pa uwekezaji Mkkude amesema, wanatumia fursa hiyo kufungua milango kwa wawekezaji na wafanyabiashara kufanya kazi zao kidigitali na kuleta matokeo chanya.

Vile vile amesema katika maonesho hayo TTCL  limekuja na huduma ya mtandao (WiFI  T-Cafe ) ambayo imelenga  kuwaondolea adha wafanyabiashara, waandishi  wa habari na wataalam wa masuala ya ushauri na yeyote anayetaka kufanya kazi nje ya ofisi yake ,na kupata huduma hiyo bure.

Pia amezungumzia huduma ya 'fiber nyumbani kwako' inayopatikana kwa gharama nafuu ambapo amesema elomu ya huduma imetolewa kipindi chote cha maonesho.

"Na tayari tumepokea maombi mapya mengi ,wanaohitaji huduma ambayo imekuja kuleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifufushi vya kawaida, ambapo sasa shirika limeleta huduma hii ambayo inamwezesha mteja kutumia internent ambayo haina ukomo.

Amewasihi wananchi ambao bado hawajaomba nafasi hiyo kutumia tovuti  www.ttcl.co.tz kisha taarifa zao zitachukuliwa na kuanza mchakato wa kuwafungia huduma hiyo .

Katika hatua nyingine amesema shirika katika huduma yake ya T-Pesa wamekuja na huduma ya akaunti ambayo inamwezesha mteja kufungua akaunti ya TTCL Pesa bila kuwa na hitaji la sim card.
Share:

Utafiti:Zaidi ya nusu ya eneo la Tanzania lina viashiria vya mafuta

Published from Blogger Prime Android App
Mkuruhenzi wa PURA Mhandisi Charles 




Na Joyce Kasiki ,Dar Es Salaam


 MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni amesema,Tanzania ina viashiria vya kuwepo mafuta katika wneo la ukubwa wa skweakilomita 534,000.

Akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la PURA katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) Mhandisi Sangweni amesema hayo ni matokeo ya utafiti wa awali huku akisema eneo hilo ni asilimia zaidi ya asilimia 50 ya eneo lote la Tanzania lenye ukubwa wa skwea kilomita karibu 900,047.

"Hapa nchini tumefanya tafiti za awali katika maeneo mbalimbali ,ikumbukwe kwamba nchi yetu ukubwa wake  inakava skwea kilomita karibu 900,047, kati ya hizo tafiti tulizofanya maeneo yenye viashiria vya kuwepp mafuta ni eneo la skwea kilomita 534,000 ,

"Sasa hiyo ni karibu asilimia zaidi ya 50 ya eneo lote la Tanzania,lakini katika haya maeneo ambayo yana viashiria vya mafuta au gesi asilia hadi sasa tumefanya yafiti eneo la ukibwa skwea kilomia 160,200.., sasa bado tuna eneo kubwa ambalo tunaamini lina miamba tabata na linaweza kuwa na mafuta hatujafanyia tafiti"amesema Mhandisi Sangweni

Aidha amesema ,mpaka mwishoni mwa mwaka huu au mwaka ujao , wanatarajia kutangaza maeneo mbalimbali ambayo yatavutia wawekezaji kwa ajilli ya kushirikiana na PURA na kampuni yao Tanzu la Shirika la Maendeleo ya Patroli nchini (TPDC)   kwenye kutafuta mafuta.

Vilevile amesema kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamefanya Dunia yote inataka kibafilisha mwelekeo kutoka kwenye matumkzi ya nishati chafu na kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ,Tanzania nayo ipo kwenye muelekeo huo.

"Tunafahamu kwamba dunia inabadilika,kwenye upande wa nishati dunia yote inaongelea nishati safi na inataka kutoka kwenye nishati hiyo ya petroli kwenda kutumia nishati ya hewa  ambayo inazuia uchafuzi wa mazingira ,malengo ni kufika 2060 dunia iwe imefikia kwenye matumizi ya nishati jadidifu kwa kiasi kikubwa."

Amesema,kwa upande wa Tanzania  malengo ya kufikia nishati safi ya kupikia kwa hadi asilimia 80 ifikapo 2034 huku akisema kuhama kwenye nishati  ambayo inachafua hali ya hewa na kutumia nishati ambayo uchafuzi wake siyo wa kiasi kikubwa au haichafui kabisa.

"Sasa sisi kama watafutaji wa petroli ,ni wadau wakubwa kwenye hilo na katika hili sisi tunafanya tafiti mbalimbali za kuwezesha hili liwezekane,lakini wakati huo tunatafuta kiasi cha gesi ambacho ndiyo tuliyogundua hivi sasa hapa nchini."amesema Mhandisi huyo

Kwa mujibu wa Mhandisi Sangweni ,gesi hiyo itasaidia kutumika  majumbani  ,kwenye magari na maeneo mengine ya uendeshaji mitambo kwa sababu gesi asilia iliyopo ambayo kwa sasa imegunduliwa Songosongo na Mnazibay imepitishwa duniani kama chanzo cha nishati ambacho kitatumika kwa kipindi cha mpito kuelekea matumizi ya nishati jadidifu .

"Kwa hiyo sisi kama taasisi ya Serikali tunatekeleza hilo kwa kujenga mazingira bora na yanayovutia kwa wawekezaji ambao ndio wenye makampuni wanaokuja kufanya tafiti kwenye eneo hili la mkondo wa juu wa petroli."amesisitiza


Sasa sisi tunadhibiti shughuli A utafutaji hapa nchini 


Share:

Ushirikishwaji usomaji ankara za maji unavyoondoa migogoro

Published from Blogger Prime Android App
MENEJA Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Idhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo


Na Joyce Kasiki 

MENEJA Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Idhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo amesisitiza Ankara zote za maji kusomwa wakati mwenye Dira yupo ili kuondoa malalamiko ya kubambikiziwa Ankara za maji.

Kaguo ameyasema hayo katika maonesho ya 48 ya  Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) huku akisema tayari EWURA ilishatoa mwongozo wa suala hilo.

"Katika maji  malalamiko makubwa yapo katika ankara ,lakini EWURA  ilishatoa miongozo kwamba ankara zote ziwe zinasomwa wakati mwenye dira yupo,yaan hakuna cha kusema eti geti limefungwa, litafunguliwa mbele yako halafu unasoma, na  muhusika atapokea ujumbe mfupi kwenye simu unaoonyesha usomaji ambapo mtumiaji atahakiki kama hajabambikizwa,kama hajasema lolote baada ya siku chache atapokea ujumbe wa  ankara ya kulipia," amesema Kaguo

Amezungumzia upande wa kutibu maji ambapo amesema , wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara kujiridhisha namna ambavyo mamlaka inatibu maji na kama wateja wanaridhika na huduma.

"Tulitengeneza mfumo  wa kushindanisha mamlaka ambapo kuna mamlaka inayoongoza kitaifa na kuna mamlaka inayoongoza kwa kuwa mwishoni hali iliyosaidia kuboreshwa kwa huduma za maji kwa ujumla

“Kila mwaka EWURA huwa inatayarisha ripoti za mamlaka ya maji ambayo inaonyesha mamlaka ipi ni bora kuliko nyingine, inafanya uwajibikaji na uwazi uwe mkubwa,kwenye maji tunapopanga bei tunashirikisha wadau wote na bei inayokuja inakuwa inaeleweka  hii ni kwa ajili ya kukuza uwajibikaji."amesema

Ameongeza kuwa"EWURA huwa inageuka kama mahakama ya kuendeshea kesi pale Mamlaka ya maji inaposhindwana na wananchi na kusababisha malalamiko,hii ni kwasababu kwenye uwajibikaji watu wakipata huduma isiyoridhisha wanalalamika,kwa hiyo Kama mamlaka ya maji ilitenda kosa italipa fidia kwa muhusika."

Kuhusu gesi asilia amesema imesaidia katika uzalishaji wa umeme nchini, inatumika kupikia katika baadhi ya taasisi, viwanda zaidi ya 50 Dar es Salaam na Pwani vinatumia lakini pia ni Nishati mbadala katika kuokoa mazingira nchini 

Katika hatua nyingine Kaguo amewasisitiza wananchi wote wenye magari  kuhakikisha wanachukua risiti baada ya kununua mafuta  ili kurahisisha ulipaji fidia pindi inapotokea wameharibikiwa na gari kutokana na mafuta waliyojaza.

Amesema iwapo mafuta yalikuwa na matatizo na kusababisha gari kuharibika mwenye kituo atapaswa amfidie gharama za ukarabati na adhabau atapewa.


Share:

CBE sasa kutoa 'Masters' kwa njia ya mtandao

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Matukio katika picha yakionesha Mkuu wa Chuo cha CBE alipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)  jijini Dar Es Salaam




Na Joyce Kasiki Dar Es Salaam


MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Profesa Tandi Luoga amesema chuo hicho kimekuja kivingine kwani kimeanza kutoa masters kwa njia mtandao.


Akizungumza alipotembelea banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam ,Profesa Luoga amesema hatua hiyo inakwenda kumrahisishia mtumishi kusoma bila kuathiri shughuli zake.


Amesema Programu ya mtandaoni imeanza Machi mwaka huu huu huku akisema hii ni kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia katika kurahisisha mambo.


Amesema ,Chuo hicho chenye matawi manne katika mikoa  ya Dar Es Salaam ,Dodoma,Mwanza na Mbeya kimefikia maamuzi huo wa masomo mtandaoni ili kutoa wigo mpana hasa kwa watumishi na makundi mengine kujiendeleza kielimu.


 "Kwa hiyo kwa sasa tuna wanafunzi wanaoshiriki masomo kwa njia ya mtandao ambapo mahali popote walipo wanapata masomo yao ." Amesema


Amesema mwanafunzi wa Masters anayesoma kwa njia ya mtandao , hahitaji kwenda mpaka CBE Mwanza,Dodoma Mbeya au Dar Es Salaam kusoma isipokuwa wakati wa mitihani ambapo mwanafunzi anaenda kwenye Tawi lolote la chuo hicho lililo karibu naye.


"Hatua hii imesaidia kusambaza elimu ya biashara ndani na nje ya Tanzania, lakini imepunguza gharama kusafiri na malazi kwa mwanafunzi husika." Amesisitiza


Pia amesema chuo hicho kina kozi nyingine nyingi kwa ngazi mbalimbali zikiwemo za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo katika mafunzo ya muda mrefu wanaotoa elimu kuanzia ngazi ya cheti  ,diploma,bachelor na masters .


Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wenye sifa na vigezo kuomba nafasi za masomo katika chuo hicho .


Xxxxxx


Share:

PURA na mkakati wake wa kutafuta wawekezaji

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App




Ns Joyce Kasiki Dsr Es Salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Khalfan Khalfan amesema  PURA itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye sekta ya utafutaji wa mafuta ili kuongeza tija katika eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara kwenye banda la PURA jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti huyo amesema hilo ni jukumu la PURA na kwamba waeekezaji hai lazima watafutwe kiushindani.

"Ili kutekeleza suala la kupata wawekezaji kwa ushindani ,taasisi imekuwa zinafanya matayarisho ya kuwatafuta wawekezaji hao kwa ushindani siyo kwa kuokotwa ,

"Na ili uwapate kwa ushindani tunafanya Duru kwa maana ya kutosha mkutano wa 'kupromote' maeneo halafu wawekezaji wanakuja mkutanoni wanadikiliza sera kisha wanachama maeneo."amesema Profeda Khalfan

Aidha ametaja majukumu makubwa ya PURA kuwa ni pamoja na  kumshkuru Esziei wa Nishati maduala ya mkondo wa juu wa Petroli ambao ni utafutaji ,uzalishajina usambazaji wa gesi nchini.

Pia amesema jukumu lingine ni kusimamia ufanisi wa sekta ya utafutaji na uzalishaji pamoja na watafutaji kwa ujumla wake lakini pia kuhakikisha watanzania nao wanashiriki kwenye shughuli za uzalishaji na utafutaji kwenye sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo,jukumu lingine ni kusimamia pale zitakapoanzishwa shughuli za uuzaji wa gesi nje ya nchi huku akitoka mfano mradi ambao Serikali imekuwa ikifanya mazungumzo na wawekezaji huku akisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri.

Amesema mazungunzo hayo yakifanikiwa ,wawekezajinwataweka mtambo wa kuchakata gesi mkoa wa Lindi eneo la Likongo ambapo gesi ile itaenda kuuzwa nje ya nchi.

Aidha ametaja  mafanikio yaliyopatikana kwenye gesi asilia kuwa ni pamoja na kuchangia kwa wastani wa asilimia 50 ya Umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani pamoja na matumizi ya gesi kwenye magari huku watanzania zaidi ya 1,428 wakipata  ajira za kudumu na za muda katika miradi ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini na kupunguza changamoto ya ajira nchini.



Share:

Ubunifu uchoraji picha Rais Samia washangaza wananchi maaonesho sabasaba

Na Joyce Kasiki,Dar
PICHA moja  ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan iliyochorwa na mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma inayomuelezea Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa  katika majukumu yake matatu makubwa ya Kitaifa imekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wengi wanaotembelea maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Dkt.Deograsia Ndunguru amesema,watunwengi wanaotembelea banda lao wamekuwa wakishangazwa na ubunifu na ujuzi ambao ametumia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza fani ya sanaa chuoni hapo Enock Tarimo kuchora moja inayomuelezea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa katika mavazi matatu tofauti katika majukumu yake ya kitaifa.

"Picha hii ni moja lakini inamuonesha Dkt.Samia katika majukumu matatu tofauti,Ukisimama katikati anaonekana akiwa katika vazi la kiremba chekundu ambayo hutumika maeneo yote kwamba ni picha Rais,ukisimama kushoto anaonekana kama Mwenyekiti wa CCM akiwa katika vazi la kijani na nyeusi na ukisimama upande wa kulia anaonekana katika vazi la kijeshi kama  Amiri Jeshi Mkuu ,kwa hizi ni ubunifu ambazo zinafanya na wanafunzi wetu."

Amesema taaluma ya Sanaa ni moja ya fani ambazo zina fursa ya ajira kwa vijana na hivyo kuwawezesha kujiajiri wenyewe .

Dkt.Ndunguru alisema  wanafunzi wa fani hiyo katika Chuo hicho   wamekuwa wakifundishwa kutumia fursa mbalimbali kupitia rasilimali zinazowazunguka katika mazingira yao  katika kujipatia kipato kwani sanaa ni ajira.

"Kwa mfano chupa za wine na chupa nyingine,chupa hizi hutupwa kila baada ya matumizi ,lakini kwa fani ya sanaa hii ni fursa ambapo zinatengenezwa mapambo."alisema Dkt.Ndunguru

Ameongeza kuwa"Katika maonesho haya tumekuja kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo pamoja na wanafunzi ,kwa hiyo katika banda letu kuna bunifu mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wetu ikiwemo hiyo picha ya Rais Dkt.Samia ,mapambo pamoja na picha nyingine nyingi zilizochorwa na wanafunzi wetu.

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wangependa fani hiyo na hawana nafasi ya kufika ngazi za elimu ya juu,kusoma hata kozi fupi ili waweze kupata ujuzi wa kutosha.

Mhitimu wa UDOM 2023 Sultan Samwel ambaye amejiajiri katika kampuni yake ya mambo ya sanaa Talnis Creative Agency, ametembelea banda hilo na kufurahishwa kuona picha zake alizochora akiwa shuleni.

"Nimefurahi kukuta picha nilizochora katika moja ya mitihani yangu nikiwa chuoni pamoja picha za wanafunzi wenzangu,kimsingi niseme tu sanaa ni ajira kama zilivyofani nyingine kama daktari au sheria na nyingine nyingi,kama hivi mimi nimejiajiri katika kampuni yangu.

Xxxxx

Share:

Serikali kuongeza vituo 8 vya kujaza gesi kwenye magari

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App




Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam
 

SERIKALI imesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu itakuwa imejenga  vituo vya kujaza gesi kwenye magari (CNG)  maeneo ya Muhimbili, Kibaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Mwenge, Goba, Mbezi Beach na Mbagala .

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) huku akisema  baadhi ya vituo hivyo vitajengwa na TPDC na vingine sekta binafsi. 

"Hili la kuwa na kituo kimoja cha Ubungo Maziwa na Airport tutaachana nalo ndani ya mwaka huu na mwakani, tutakuwa na magari mengi yanazunguka ndani ya jiji ambapo wateja watafikiwa na kujaza gesi, 

"Kwa hiyo suala la kujaza gesi kwenye magari tunajaribu kulirahisisha na kadiri inavyowezekana ili kuondoa adha ambayo ipo sasa." Amesema Mhandisi Mramba

Akizungumza kuhusu bomba la mafuta amesema mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 30 ambapo hadi sasa  kilomita zaidi ya 600 za mabomba zimeshaingia nchini .

Amesema matarajio ya Serikali, hadi kufikia mwishoni   mwa 2025 mradinuwe umekamilikq.

Mhandisi Mramba amesema,mkataba rasmi wa kuanza utekelezaji wa mradi huo ulifanyika Februari 2022 na uwekezaji umedhaanza na  unatekelezwa kwa kasi .

"Mradi huu umezungumzwa muda mwingi, umeanza kuzungumzwa tangu awamu ya tano, awamu hii ya sita, ni mradi mkubwa unachukua muda mrefu, ujenzi unahusisha usanifu, kulipa watu fidia, kujenga mtambo mkubwa wa kufanya mafuta yasipoe.amesisitiza

Aidha ameitaka kampuni Tanzu ya TPDC ya GASCO   kujitangaza zaidi kupitia maonesho ya sabasaba kwani kuna Watanzania wanahitaji huduma ambazo GASCO wanazitoa. 

"Tunataka iwe na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi yetu, eneo ambalo tunataka waongeze ushiriki wao katika uchumi ni eneo la gesi, tunataka gesi iliyopatikana nchini isambae kwa haraka zaidi. Isambae kweney vituo vya kujaza kwenye magari, isambae na majumbani. "

Aidha ametaka sekta binafsinishirikishwe zaidi  katika usambazaji wa gesi majumbani na gesi za kwenye magari badala ya kutegemea TPDC peke yake hatua ambayo itachukua   muda mrefu kuwafikia Watanzania wengi.

"Lakini tukishirikisha sekta binafsi wakasambaza mabomba kwa ajili ya gesi majumbani, kujenga vituo vingi vya CNG, wakaenda mpaka mikoani gesi hii itasambaa haraka. "Amesisitiza

Share:

KAMATI YA GEF YATINGA DODOMA YAHIMZA  KIZAZI CHENYE USAWA DIRA YA TAIFA 2050

Published from Blogger Prime Android App


Na WMJJWM-Dodoma

Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye Usawa, imeshauri agenda ya Kizazi chenye Usawa kujumiishwa katika Dira ya Taifa ya 2050 ili utekelezaji wake uwe katika mifumo ya utendaji wa Serikali.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwa mkoa wa Dodoma Julai 09, 2024, yenye lengo la kufuatilia utekelezaji Programu ya Kizazi chenye Usawa na jitihada zilizopo katika Taasisi mbalimbali kukuza haki na usawa wa kiuchumi kwa wanawake nchini.

Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wake Mhe. Angellah Kairuki, Bi. Being'i Issa amesema suala la Usawa wa kijinsia ni mtambuka na linahitaji nguvu ya kila Taasisi kushirikiana na kuhakikisha linawekwa katika vipaumbele vyake ili kuwezesha kufikia ahadi zilizowekwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kufikia Kizazi chenye Usawa kiuchumi nchini.

"Niseme tu suala la Usawa wa kijinsia sio la Wizara moja au Taasisi moja ni letu sote na tukilibeba na kuliweka katika agenda za Kitaifa litaondoa ukakasi wa agenda hii kuonekana na ya upande wa jinsi moja tu bali ni kwa jinsi zote Wanawake kwa wanaume" amesisitiza Being'i.

Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Carolyn Kandusi ameshauri kuwepo na mikakati dhabiti katika Taasisi mbalimbali ili kuwe na mifumo itakayowezesha kuwepo na usawa wa kijinsia katika maeneo muhimu hasa katika sekta zenye kuwezesha wananchi kiuchumi.

Katibu wa Kikundi cha wajasiriamali cha Winni Star kilichonufaika wa uwezeshaji Wanawake kupitia asilimia kumi za Halmashauri, Julia Issaya Malabar amesema pamoja na kukumbana na changamoto mbalimbali hasa za kimtaji, wameungana na kujiwezesha kuanzisha biashara hiyo na baadae kuwezeshwa mkopo kutoka Halmashauri. Amewaasa Wanawake kuanza kujitoa ili juhudi zao ziweze kuungwa mkono na Serikali na wadau wengine wa maendeleo.
 
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika kiwanda cha uchakataji wa bidhaa za plastiki cha CAL Plastic Company Mmiliki wa Kiwanda hicho Aziza Abdi Hassir ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuwezesha kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mkopo kutoka Mfuko wa WDF uliofanikisha kukuza biashara yake hiyo.

"Nilianza na mtaji wa Millioni 9 kama fedha za uendeshaji na mpaka sasa nimefikia zaidi ya Millioni 100 na kuajiri watu kutoka sita mpaka zaidi ya 180 kwa kuzingatia Usawa wa kijinsia katika kutoa fursa za kiuchumi kupitia Kiwanda changu" alisisitiza Aziza

Kamati hiyo katika kufuatilia utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye Usawa siku ya kwanza kwa mkoa wa Dodoma imetembelea Kikundi cha wajasiriamali Wanawake cha Winning Star kilichopo Ilazo, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki kinachomilikiwa na Mwanamke Nala jijini Dodoma.

Share:

TMDA yatoa elimu usugu vimelea vya dawa

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kaaiki,Dar es Salaam 

USUGU wa vimelea  vya Dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi ya dawa yasiyo sahihi kwa baadhi ya watumiaji.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar Es Salaam ambapo amewataka 

Pia imewataka wananchi  kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kuacha kutumia dawa kiholela bila  maelekezo ya wataalamu.

"Katika kuhakikisha dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi wananchi wanapaswa kufuata maelekezo sahihi  yanayotolewa na wataalam na ndio maana pamoja na mambo mengine,sisi TMDA timeshiriki maonesho haya pia kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kufahamu majukumu ya Taasisi hii."amesema Fimbo

Ametumia nafasi hiyo kutoa  wito  kwa wananchi kuendelea kutembelea kwenye banda lao kupata elimu ya udhibiti na matumizi sahihi ya dawa  na vitendanishi.


Share:

Mhandisi Mramba aipa tano EWURA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam


KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati Felichesmi Mramba ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji kwa huduma inayofanya ya udhibiti huku akisema imesaidia kupunguza hata changamoto ya kukatikakatika kwa umeme.

Mramba ameyasema hayo leo Julai 9,2024 kwenye maonesho ya 48 ya  Kimataifa ya Biashara alipotembelea banda la Mamlaka hiyo.

"Leo nimetembelea banda la EWURA, kama mnavyofahamu ,EWURA ni taasisi yenye wajibu wa kudhibiti huduma za Maji na Nishati,kwenye eneo la nishati,tunadhibiti umeme ,huduma za  umeme ,huduma za gesi asilia ,huduma za mafuta,

"Tunachoweza kusema EWURA imefanya kazi nzuri sana mpaka sasa hivi,kama mnavyoona huduma zinazodhibitiwa na EWURA zinapatikana na wameweza kudhibiti upatikanaji wa huduma yenyewe ,bei ya huduma inayotolewa na ubora wa huduma hiyo,sasa kwenye eneo la bei nafikri mnafahamu kwamba nchi yetu ni miongoni mwa nchi zenye bei ya chini sana ya huduma za umeme  ,

"Ubora wa huduma ya umeme umeimarika sana, kule kukatikakatika saana na mgao wa umeme kumepungua kwa kiasi kikubwa, ingawa hatusemi kwamba ubora sasa umefikia mahali kwamba hakuna shida..., hapana, lakini angalau ubora wa huduma hiyo upo katika kiwango cha kuridhisha na tunaendelea kuboresha ."amesema Mhandisi Mramba 

Vile vile amesema, kwenye maeneo ya gesi asilia EWURA amesaidia sana na anaendelea kufuatilia kwanza kutoa leseni kwa wale wanaojenga vituo hasa vya gesi iliyokandamizwa (CNG) pamoja na vituo vya mafuta, lakini pia anasimamia kuhakikisha kwamba huduma zinazotolewa na vile vituo vinakidhi mahitaji ya jamii.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mramba,wajibu wa Wizara ya Nishati ni  kuhakikisha kwamba EWURA anafanya kazi yake kulingana na sheria na sera zilizopo, lakini pia tunamwezesha kutekeleza majukumu yake katika mazingira yanayokubalika ndani ya sekta .

"Kwa hiyo tunaendelea kuwatia moyo watanzania kuwa zipo huduma pia za kiushauri ambazo EWURA anazitoa,zipo huduma za kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi."amesisitiza

Kwa upande wake Mkurugenzi wa EWURA James Andilile amesema ,EWURA imeingia mkataba na TANESCO kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wao ili kuboresha utebdaji na upatikanaji wa umeme ambapo kwa sasa Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Nishati ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarika.


Share:

Mhandisi Mramba aipa tano EWURA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam 

KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwenye maeneo ya gesi asilia ambapo amesaidia  na anaendelea kufuatilia  kutoa leseni kwa wale wanaojenga vituo hasa vya gesi iliyokandamizwa (CNG), pamoja na vituo vya mafuta.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na  Mhandisi  Mramba, alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya 48 ya Kimataiafa ya Biashara Dar es Salaam (DITF),amesema Mamlaka hiyo inasimamia  na kuhakikisha huduma zinazotolewa na vile vituo vinakidhi mahitaji ya jamii.

Mhandisi Mramba huyo amesema jukumu la Wizara ya Nishati ni kuhakikisha kwamba EWURA inafanya kazi yake kulingana na sheria na sera zilizopo na kwamba  wanaiwezesha kutekeleza majukumu yake katika mazingira yanayokubalika ndani ya sekta.

"Tunaendelea kuwatia moyo watanzania kuwa zipo huduma za kiushauri ambazo EWURA inazitoa, zipo huduma za kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi, amesema Mhandisi Mramba.

 Mkurugenzi Mkuu wa EWURA James Andilile amesema Mamlaka hiyo imeingia mkataba na  Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wao ili kuboresha utendaji  huo na upatikanaji wa umeme .

Amesema kuwa  kwa sasa Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Nishati ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarika.

Share:

Kikwete ashauri kushushwa bei za gesi umeme kiwezesha matumizi Nishati mbadala

Published from Blogger Prime Android App
RAIS Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete  alipotembelea banda la TANESCO katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam

Na Joyce Kasiki,Dar es Salaam 

RAIS Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete amesema vita dhidi ya nishati safi ya kupikia nchini itafanikiwa endapo gharama ya umeme na gesi zitapungua.

Dkt Kikwete ameyasema hayo jana alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.

"Maadui wawili  wa mazingira yetu  ni kuni na mkaa,kwa hiyo kama napambana yataelekezwa katika kupunguza gharama za umeme na gesi itasaidia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia."alisema Dkt.Kikwete na kuongeza kuwa 

Kwa mujibu wa Dkt.Kikwete,watu wengi nashindwa kuhusu gharama za gesi na umeme kwa ajili ya kupikia huku akisema kama gharama hizo zitakuwa kwa gharama.nafuu kama ilivyo kwa kuni na mkaa,basi vita dhidi ya Nishati safi yabkupikia unafanikiwa na hivyo kuokoa mazingira.

 Akiwa katika banda la Wakala wa Nishati  Vijijini(REA), Dkt.Kikwete baada ya kukagua majiko yanayotumia umeme aliishauri REA kuja na mpango utakaowasaidia watu wasiokuwa na uwezo kutumia nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu.

“Vitu mnavyovileta hapa kama Nishati nafanya kupikia ni kwa ajili ya watu wenye uwezo tu,Bali mnapaswa kuleta na vile vya gharama nafuu ambavyo kila mtu anaweza kuhusu gharama." Amesisitiza
Share:

Mkurugenzi Mkuu VETA aeleza umuhimu wa VETA

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Joyce Kasiki,Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore amepongeza juhudinza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kujenga vyuo vingi vya VETA ambapo hadi kufikia 2025 kutakuwa na idadi ya vyuo takriban 145 vitakavyokuwa katika wilaya zote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam kwenye Banda la VETA,Mkurugenzi huyo amesema lengo la Dkt.Samia na Serikali kwa ujumla no kuhakikisha kila eneo lenye wahitimu wa VETA kunakuwa na nyenzo rahisi zinazoweza kutatua changamoto za jamii husika.

"Nia ya vyuo hivinsiyo kujenga tu ,bali ni kwa shughuli maalum ya kupata wataalam wenye ujuzi wa kutatua changamoto.kwenye eneo husika kulingana na rasilimali zilizopo na mahitaji yake."

Ameongeza kuwa "Mwaka 2022 tulikuwa na vyuo vya VETA  vipatavyo 29 ambavyo vilitoanhufuma  sasa vipo 80 na ujenzi unaendelea wa vyuo 65 katika wilaya  ifikapo 2025 vyuo vyote vitakuwa vimekamilika na kufanya idadi ya vyuo vya VETA kuwa takriban 145  ambapo kila wilaya itakuwa ina chuo hiki."

Kasore amesema hatua hiyo pia inakwenda kuleta Tina katika uwekezaji ambapo wataalam katika fani mbalimbali wanakwenda kupatikana kupitia vyuo hivyo na kufanya kazi kwenye maeneo ya uwekezaji na viwanda.

Vile vile amesema VETA imekuwa ikitoa elimu ya ufundi kwa wenye ulemavu ambao nao wamekuwa karibuni nyenzo za kifundishia watu wenye ulemavu kutokana na changamoto za ufundishaji nanujifunzaji wanaouona wanapokuwa wanafundishwa na walimu wao.

"Ndio maana tunasema kwetu VETA aletwe mtoto mwenye ulemavu wowote sisi tutamuangalia sina ya ulemavu na tutajua aseme fani gani na namna ya kumfundisha."amesisitiza

Pia amesema katika maonesho hayo wamekuwa kuonesha nini VETA inafanya ambapo zipo bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na walimu kwa kushiriliana na wanafunzi wao ambazo kimsingi zinaenda kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

"Kwa mfano kuna machine ya kumenya viazi vya chips ambapo unakuta ni mjasiriamali mdogo anataka kumenya dunia la viazi,huyu hawezi kupata adha ya kuweka mtu wa kumenya viazi kama atakuwa na mashine hii,kwa hiyo zipo bidhaa nyingi ambazo zinaenda kurahisisha kazi huko katika jamii zetu." Amesema

Pia amesema VETA inatoa mafunzo kwa wafanyakazinwa ndani na wanaohudumia wazee na watoto huku akisema wakina hiyo ni changamoto wakaongeza na mtaala huo ili hata wale wanaohitaji kwenda kufanya kazi za ndani nje ya nchi wamekuwa na mtaalam huo na hivyo kufanya kazi kwa kujiamini na uhakika.
Share:

TAWA YANADI FURSA ZA UWEKEZAJI MAONESHO YA 48 YA KIMATAIFA ALMAARUFU SABASABA 2024

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App



Na Beatus Maganja, Dar es Salaam.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatumia maonesho ya 48 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam kuhamasisha Umma wa watanzania wawekezaji na wageni  kutoka mataifa mbalimbali kuwekeza katika maeneo  inayoyasimamia huku ikijinasibu kuwa na fursa lukuki za uwekezaji

Akiongea na wageni waliotembelea banda la TAWA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Afisa utalii Daud Tesha amesema TAWA ina uwanda mpana wa fursa za uwekezaji unaotoa mwanya kwa wawekezaji wa aina mbalimbali kuwekeza katika Taasisi hiyo

Akizitaja fursa hizo Tesha amesema yapo maeneo mengi yanayohitaji wawekezaji na uwekezaji katika Taasisi hiyo kama vile maeneo ya utalii wa picha kwenye maeneo ya hifadhi za Wanyamapori, maeneo ya kihistoria yenye Utalii wa kiutamaduni, eneo la uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA), Uwindaji wa Kitalii na Ufugaji wa Wanyamapori

"TAWA imetenga maeneo kadhaa Kwa ajili ya kufanyika shughuli za utalii wa picha kutokana na ikolojia na aina ya vivutio vilivyopo katika maeneo hayo ikiwemo Pori la Akiba Mpanga/Kipengere eneo ambalo lina maporomoko ya maji zaidi ya 10 ambayo hutoa burudani safi kwa watalii" amesema Daud Tesha 

"Maeneo  mengine ni Pori  la Akiba Wamimbiki, Tabora ZOO, Ruhila ZOO , Makuyuni Wildlife Park ambapo wananchi wanakaribishwa kuwekeza kwenye miundombinu ya Utalii ikiwemo kujenga Kambi za Kulala wageni (Campsites), Hosteli, Loji na maeneo ya mapumziko mafupi kwa watalii (Picnic Sites) ameongeza 

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja ametumia  fursa hiyo kuwakaribisha wananchi Wote kutembelea banda la TAWA Ili kupata maelezo ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi hiyo.

"Kama kauli mbiu ya Maonesho haya inavyosema kuwa Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji, nitumie fursa hii kuwaambia watanzania wote kuwa TAWA ni Taasisi sahihi kwa biashara na uwekezaji kwani inatoa fursa za uwekezaji wa aina mbalimbali kama vile ujenzi wa loji, kumbi za mikutano katika maeneo yetu, kambi za watalii, michezo ya watoto lakini kama haitoshi mwekezaji anaweza akatumia fursa ya kuwekeza katika mashamba ya wanyamapori, bustani za wanyamapori n k" amesema Maganja

"Kwahiyo hii ni fursa adhimu Kwa wawekezaji wote kutembelea banda letu ili waweze kupata ufafanuzi wa fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi yetu" ameongeza

Maonesho haya yenye Kauli Mbiu "Tanzania ni Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji" yameanza 28 Juni, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati 14 Julai, 2024
Share:

Fundi seremala asiyeona aishangaza jamii

Published from Blogger Prime Android App
Raphael Mwambalaswa fundi seremala asiyeona aliyepata mafunzo VETA


Na Joyce Kasiki, Dar es Salaam 

VYUO vya VETA vimedhihirisha umahiri wake katika kufundisha hadi watu wenye ulemavu na kuwatoa katika dimbwi la utegemezi.

Watoto wengi wenye ulemavu wamekuwa wakatiwa tamaa katika jamii ambapo wengi wao hawapelekwi shule.

Mwanafunzi Raphael Mwambalaswa  amekuwa kivutio kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ambapo watu wanaofika katika banda hilo wamekuwa wakishangaa namna anavyofanya kazi na uwezo wake katika fani hiyo ya ufundi seremala.

Mwambalaswa ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), amesema aliamua kwenda VETA kwa sababu aliamini  wanaweza  kumsaidia mtu asiyeona kuweza kujitegemea ndiyo maana aliamua kwenda kujifunza. 

Amesema baadhinya watu katika jamiinwamekuwa wakiamini kuwa na ulemavu mtu hawezi kufanya kitu chochote jambo ambalo siyo sahihi.

Kupitia maonesho hayo ameiasa jamii kuhakikisha inawapa elimu watu wenye ulemavu kuanzia wanapokea wadogo na mwishoni siku wawapeleke VETA ndiko ambapo walimu wana ujuzi na umahiri wa kufundishwa watu wenye ulemavu na wakala mafundi Waziri kabisa na hivyo kujitegemea kiuchumi.

Naye Mkufunzi katika Fani ya Useremala Chuo cha Veta Dar es Salaam, Mwalimu Salehe Omary, amesema wana miongozo inayowawezesha kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakiwapa maelekezo ya kuzingatia usalama. 

“Moja ya majukumu yetu ni kuhakikisha kila mtu anapata ujuzi awe mwenye uwezo wa viungo au asiye na viungo, nimepata mafunzo ya namna ya kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu. Changamoto aliyonayo mwanafunzi wangu Mwambalaswa (asiyeona) kwangu ilikuwa ni kitu kipya. 

“Lakini kwa sababu nina utayari haikuwa shida, mwanafunzi wangu pia alitumika kama mwalimu kwa kunipa mbinu za kumfundisha, zimetufanya mimi na yeye kazi yetu kuwa rahisi. 

Amesema mwanafunzi huyo alipofika chuoni hapo walitumia siku mbili kumzungusha katika mazingira yote ya chuo kuanzia anapoingia getini hadi katika karakara ya kujifunzia bila kupata changamoto yoyote
Share:

VETA Songea yabuni mashine kusaga chakula cha kuku,samaki

Published from Blogger Prime Android App




Na Joyce Kasiki,Dar es Dalaam

WAFUGAJI wa kuku na samaki wamerahisishiwa namna ya kupata chakula cha kuku au samaki kwa kutumia mashine yenye gharama nafuu kutoka chuo cha VETA Songea.

Mwalimu Sussac Mbulu amezungumza katika maonesho ya 48 ya Kinataiga ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo amesema ,kwa kiwa na mashine hiyo mfugaji atatengeneza chakula bora cha mifugo yake na kuifanya kuwa na afya bora.

Amesema wamebuni mashine za aina mbili ambapo moka ni inayotumia mkono na nyingine ya umeme.

Mbulu amesema mashine inayotumia umeme ina uwezo wa kusaga kilogramu 200 za chakula kwa siku huku ya mkono uwezo wake ni kisaga kilogramu 100 kwa siku.

Ametoa rai kwa wanaofuga kuku na samaki kununua mashine hiyo ambayo itamrahisishia katika upatikanaji wa chakula cha mifugo yake.

Vile vile amesema,mashine hiyo itawasaidia hata wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu kiweza kujiajiri wenyewe kwenye eneo la ufugaji wa kuki na samaki.


Share:

Yunus ahimiza watumishi ofisi ya Waziri Mkuu kutatua changamoto za wananchi

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Picha zote ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba yanayoenselea jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar Es Salaam leo tarehe 5 Julai, 2024.

Aidha, amehimiza watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutatua changamoto za wananchi wanaotembelea banda hilo kwa ajili ya  kupata huduma na uelewa masuala yanayotekelezwa na ofisi hiyo. 

Katika Maonesho hayo Naibu Katibu Mkuu ametembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kujionea namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo katika maonesho hayo.
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.