Serikali yafungia shule ya chalinze modern islamic kuwa kituo cha mitihani

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknlojia

Serikali yafungia shule ya chalinze modern islamic kuwa kituo cha mitihani

                          

Na WyEST,Dar Es Salaam

 

Serikali imeifungia Shule ya Awali na Msingi Chalinze Morden Islamic kuwa kituo cha Mitihani kutokana na udanganyifu uliofanyika katika Mtihani wa darasa la Saba uliofanyika Oktoba 5 na 6, 2022.

 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi kufuatia taarifa zilizotolewa na Mwanafunzi Iptisam Suleiman Slim wa kituo cha Mtihani wa shule ya Awali na Msingi Chalinze Morden Islamic akieleza kwamba alibadilishiwa namba yake ya mtihani  wakati akifanya mtihani wa somo la mwisho.

 

Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema uchunguzi uliofanywa na Kamati ya mitihani ya Mkoa wa Pwani  na ule wa  wataalamu wa miandiko  " Forensic"  uliofanywa na Jeshi la polisi umebaini  ufanano wa miandiko kwa watahiniwa 7 wa shule hiyo .

 

Waziri Mkenda amesema kwa kuwa kulikuwa na uzembe uliofanyika pamoja na kuifungia shule hiyo watumishi wa Serikali ambao walikuwa wasimamizi wa kituo hicho watachukuliwa hatua za kinidhamu  huku akimuagiza Mmiliki wa shule ya Awali na Msingi ya Chalinze Morden Islamic kuwafukuza kazi walimu wote waliohusika katika udanganyifu huo. 

 

 “Kwa kuwa Shule hii ni ya binafsi tunaifungia kuwa kituo cha mitihani na haitaruhusiwa kufanyia tena mitihani, lakini pia mwenye shule hakikisha unawafukuza kazi mara moja waalimu waliohusika  na kama hilo halitafanyika  nakuagiza  Kamishna wa Elimu  futa usajili wa shule hiyo na kuifunga  mara moja,”amesema Waziri Mkenda

 

Aidha kufuatia changamoto hiyo Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefanya marekebisho ya namba za Mtihani za watahiniwa husika ili kila mtahiniwa aweze kupata matokeo yake halali.

 

“Nakupongeza Mwanafunzi Iptisam wa kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa, tayari NECTA imefanya marekebisho hata kwa wengine ambao wamefanyiwa udanganyifu kama huo. Natoa wito kwa wananchi na wanafunzi wote ukiona mtu anafanya mchezo kwenye mitihani toa taarifa na serikali itachukua hatua mara moja,”amesema Prof. Mkenda 

 

Kwa upande wake Mzazi wa Mwanafunzi Iptisam, Suleiman Said ameishukuru Serikali kwa kufanyia kazi changamoto hiyo  aliyoipata mtoto wake wakati wa kufanya mitihani yake ya kuhitimu darasa la Saba. Pia amevishukuru Vyombo vya Habari kwa kutoa taarifa hiyo na kuweza kuwafikia walengwa na kuifanyia kazi.


Share:

Dkt.Stergomena ashiriki mkutano wa Tume ya kudumu ya Pamoja baina ya Tanzania na Msumbiji

WAZIRI wa Ulinzi Dkt.Stergomena Tax akizungumza kwenye Mkutano wa Tume ya Pamoja baina ya Tanzania na Msumbiji.

  

 NA MWANDISHI WETU

WAZIRI  wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena  Tax  ameshiriki Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano katika msuala ya Ulinzi na Usalama (JPCDS) baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika Ukumbi wa Joachim Chisano, Maputo nchini Msumbiji. 

Waziri Tax ni Mwenyekiti Mwenza wa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Cristovao Chume.

Mkutano huo unafanyika kwa mara ya nne sasa ambapo  Mkutano wa kwanza ulifanyika hapa nchini mkoani Dar es Salaam, Februari  04 - 06 Februari, 2011 ambapo Tume hiyo ilianzishwa rasmi.  

Mkutano huo umefanyika kwa ngazi tatu, ambapo ulianza kwa kutanguliwa na ngazi ya wataalamu , ukifuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa mawairi wenye dhamana ya  masuala ya ulinzi na Usalama wa mataifa haya mawili.

Pamoja na mambo mengine vikao vya ngazi zote vilijadili ushirikiano kuhusu masuala ya kiulinzi,  na hatimaye kutoa fursa kwa  Mawaziri hawa wawili, kusaini mikataba  itakayowezesha  kutekelezwa kwa Hati ya Makubaliano  kuhusu ushirikiano kupitia sekta ya Ulinzi na usalama, uliosainiwa kwa pamoja   21 Septemba, 2022 na Mawaziri wa pande zote mbili.

Utiaji saini huo, ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na mwenzake Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu, aliyoifanya Rais Samia nchini Msumbiji hivi karibuni.


Mbali na  Dkt. Stergomena, ujumbe wa Tanzania ulimjumuisha pia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Sylvester Lubala Mabula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, viongozi wandamizi wakuu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kutoka mataifa yote mawili
Share:

Miongozo ya uanzishaji na uendeshaji mabaraza ya watoto uwafikie watendaji wa mitaa na vitongoji

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima akiagana na wanafunzi jijini Dodoma


Na WMJJWM, Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum  Dkt.Dorothy Gwajima amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha Miongozo ya Uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya Ulinzi kwa Watoto yanawafikia watendaji wote hadi ngazi ya Mtaa na Kijiji.

Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo alipotembelea na kuzungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makulu na Shule ya Sekondari Sechelela katika Kata ya Dodoma Makulu, Jijini Dodoma Oktoba 30, 2022 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa uanzishaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto na Madawati ya Ulinzi wa Watoto Shuleni. 

Amesema miongozo na nyaraka ambazo kila mwananchi hususani watendaji wanatakiwa kuielewa ili kurahisisha utendaji, hivyo hazitakiwi kufungiwa ofisini.

"Hii ni nyaraka ya wazi, kila mtu anatakiwa aisome, kuanzia Mwenyekiti wa mtaa, kijiji hizi hazitakiwi kufungiwa kabatini" amesema Dkt.Gwajima

Ametumia wasaa huo pia kuzungumza na wanafunzi wa shule hizo na kuwataka kuyatumia vema mabaraza ya watoto ili kujilinda dhidi ya ukatili mahali popote.

Dkt.Gwajima ameongeza pia kwamba, Serikali inafanya jitihada nyingi kutokomeza ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kuanzisha mabaraza ya watoto na madawati ya ulinzi yawasaidie kujadili changamoto wanazokutana nazo na kutoa taarifa za viashiria vya ukatili panapostahili.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule hizo wamemshukuru Waziri Gwajima Kwa juhudi zake za kukabiliana na vitendo vya ukatili na kuwa mabaraza na madawati ya ulinzi yamewasaidia kupunguza changamoto nyingi hasa mimba za utotoni.

"Katika shule yetu Dawati limetusaidia hasa watoto wa kike kwani kabla ya Dawati walikosa mahali pa kusemea shida zao" amesema Irene Boniphace

 Naye mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Sechelela Grace Shiri amesema madawati ya watoto shuleni yamewasaidia hata walimu na wanafunzi katika shule hiyo.

"Dawati la wanafunzi limewasaidia kujitambua na kuweza kusema shida zao pale wanapopata ukatili ndani na nje ya shule, kujua majukumu yao na walimu yametusaidia kujua kwa haraka matatizo yao, wamekuwa wazi na wanaongozana wenyewe" amesema Shiri

 

Share:

Watoto wanaoishi mazingira hatarishi watambuliwe

RAIS Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali katika hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe .


 

           NA JOYCE KASIKI,DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kuwatambua watoto wote wanaoishi katika mazingira hatarishi ili Serikali iweze kuwasaidia kwa kuhakikisha wanalelewa,wanakua vizuri na kufukia utimilifu wao ambao utaleta tija katika maisha yao ya baadaye na  Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki Mtumba katika hafla ya utiaji saini mkataba wa lishe kwa Wakuu wa mikoa hapa nchini.

“Pamoja na kuwekeza katika suala la lishe, lakini tunafahamu kuwa wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi linazidi kuwa kubwa “amesema Rais Samia

Amesema,mwaka 2021 jumla ya watoto 992,901 walitambuliwa na kupewa huduma mbalimbali za kukabiliana na lishe duni na utapiamlo huku akihimiza kuendelea kutambuliwa kwa watoto hao ili kuimarisha afua za ukuaji wao na waweze kufikia hatua timilifu za ukuaji.

“Kuna watoto wanaishi katika mazingira magumu na kukua kwao kunakuwa kugumu hivyo hivyo, na hawa ndiyo wanakuja kuwa wahalifu wa baadaye kwa sababu kama anaishi mazingira magumu atatoka mapema nyumbani kwenda kujitafutia ,hana elimu hana namna  yoyote lakini  anakwenda kujitafutia,lazima wengi wao watakuwa wezi,watakuwa na vitendo viovu halafu tunakuja kupiga kelele.”amesema na kuongeza

“Gwajima (Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum) hili la kwako,mkahakikishe watoto wanaoishi mazingira magumu na hatarishi wanatambuliwa na tunawasaidia.”

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema lishe bora ni msingi wa afya na uchumi wa mtu mmoja mmoja ambapo suala hili linapaswa kuzingatiwa kuanzia kwenye malezi na makuzi ya watoto ili kueta tija kwa Taifa.

“Lishe mbovu inaleta utapiamlo ambao unaleta madhara ya kiafya na kiuchumi na hivyo kuathiri maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla ,lakini utapiamlo wa kuzidi au wa kupungua virutubishi mwilini unapelekea magonjwa ya mara kwa mara na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na hivyo kuathiri kipato cha familia na sekta ya afya.

Aidha amesema,udumavu kwa watoto unasababisha madhara ya kiakili na kimwili ya muda mrefu yanayoweza kupelekea magonjwa ya mara kwa mara ,upungufu wa uelewa darasani hatimaye kuathiri uchumi wa nchi hapo baadaye .

“Tunaweza tukadharau suala hili la lishe tukawekeza kwenye barabara na vitu vingine ,lakini lazima tujue hivyo vikibomoka tunaweza kupata fursa ya kukarabati ,lakini kwenye lishe na ubongo wa mtoto ,hatuna fursa ya kukarabati  baada ya miaka mitano,kwa hiyo wakati wa kuwekeza kwa mtoto ni sasa na hapa tutapata Taifa lenye watu wenye tija.”amesema

Hata hivyo amesema,nchi inaenda vizuri katika suala la lishe huku akisema Tafiti za TDHS zinazotumika inaonyesha utapiamlo ,ukondefu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano  umepungua kutoka asilimia 4.5 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2018.

Kuhusu upungufu wa damu kwa wanawake wenye umri wa kuzaa umepungua kutoka asilimia 45 mwaka 2015/16 hadi asilimia 29 mwaka 2015/16 huku udumavu nao ukipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 32 mwaka 2018/19.

“Lakini sasa hapa kwenye udumavu ,maana yake tunapozungumza asilimia 32,watoto wenye umri wa miaka mitano kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ni kama takriban watoto milioni tisa kwa hiyo tunazungumza watoto milioni tatu Tanzania wana udumavu,wamedumaa na hawafundishiki,

 “Pia watoto hawa hawaelewi,hawawezi kuwa wabunifu katika kufanya kazi na kuleta maendeleo ya nchi ,tunaweza tukapishana huko mikoani,mawizarani lakini tayari ubongo wa huyo mwenzetu ulishadumaa hauwezi kubadilikahauwezi kuingiza vipya,hauwezi kuja na ubunifu wa mambo mapya.

Kutokana na hali hiyo amesema Wizara ya Afya itaendelea na jukumu la kuandaa na kuto sera miongozo na mikakati ya afya ikiwemo huduma za lishe na kuzifanyia kazi sera zilizopitwa na wakati kwa maslahi mapana ya watoto hapa nchini na Taifa kwa ujumla.

Kuhusu kupunguza udumavu kwa watoto amesema wataendelea kushirikiana na wadau wa lishe nchini kutekeleza afua za lishe zenye matokeo makubwa zinazolenga siku 1000 za maisha ya mtoto ikiwemo utoaji wa madini ya chuma na acid ya folic kwa akina mama wajawazito takriban kwa akina mama wajawazito milioni 2.3 kwa mwaka.

Naibu Katibu Mkuu Afya Dkt.Grace Maghembe amesema,mkakati uliowekwa ni kuwafikia wananchi ili waweze kuelewa suala hili la lishe kwa kurejesha siku ya maadhimisho ya lishe ya kijiji ili  iweze kuadhimishwa kwenye ngazi ya kijiji .

Vile vile amesema pia mpango ni kuelimisha jamii kupitia wahudumu wa ngazi ya afya ya jamii na kufanya vikao vya tathimini kwa ngazi ya kata na ngazi ya kijiji badala ya tathimini hizo kufanyika katika ngazi ya mikoa na halmashauri lakini pia kutumia mitandao ya kijamii ili elimu iweze kufika kwa jamii.

Share:

Kozi ya wasaidizi wa kisheria kuanza kutolewa nchini

Mkuu wa kitengo Cha sheria katika Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) Berinda Mollel akizungumza jijini Dodoma katika ukubi wa Jakaya wakati wa Mkutao wa Chama cha Mawakili wa Serikali.


 

         NA JOYCE KASIKI,DODOMA               

TAASISI ya  Mafunzo ya sheria kwa vitendo  imesajili kozi ya wasaidizi wa kisheria ambayo pia itaanza kutolewa mwaka huu hapa nchini ili kulijengea uwezo kundi hilo la wasaidizi wa kisheria.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkuu wa kitengo Cha sheria katika Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo (LST) Berinda Mollel huku akisema kozi hiyo itaanza kutolewa mwaka huu.

Vile vile Mollel amesema,wao kama wataalam wanaotoa mafunzo ya weledi katika ngazi ya watu waliohitimu shahada ambapo wanapenda  kuwa mawakili au watumishi wa umma .

“Pia tunatoa mafunzo ya weledi kwa wasaidizi wa kisheria ,kwa hiyo jukumu letu sisi tulilopewa na nchi ni kutoa mafunzo haya kwa sababu ndiyo taasisi pekee inayotoa mafunzo ya weledi katika ngazi hii.”amesema na kuongeza kuwa

“Tangu kuanzishwa kituo hicho miaka 12 iliyopita tumezalisha maelfu ya mawakili ambao wengi wao wanafanya kazi hii ya uwakili katika maeneo mbalimbali.”amesisitiza

 

Mollel ametumia nafasi hiyo kuwaasa  wahitimu wote wa shahada ya sheria kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili binafsi nchini au katika utumishi wa umma kufanya mafunzo ya mwaka mmoja katika taasisi  hiyo huku akiainisha kuwa wahitimu hao ni wale waliomaliza shahada zao baada ya sheria kuanza kufanya kazi mwezi Mei 2017.

 

“Dhamira kuu ya taasisi hii ni kutoa ushauri  wa kisheria kwa watoto,kutoa ushauri wa kisheria kwa wanawake,kuandaa nyaraka za mahakamani, kufuatilia mwenendo wa kesi mahakama kutoa mwongozo wa taratibu za kufuatilia kesi, kutoa msaada wa kisheria katika makundi mengine sambamba na usuluhishi wa migogoro”amesema Mollel

Share:

NIC Shirika la Bima linalotoa huduma bora na kwa haraka

 

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Bia la Taifa (NIC) Karimu Meshack akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa chama cha Mawakili Tanzania


           NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MKUU wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Karimu Meshack amesema,Shirika hilo ni moja ya mashirika bora yanayotoa huduma bora za bima kwa wananchi zinazohusiana na majanga mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Chama cha Mawakili Tanzania,Meshack amesema,lengo la shirika hilo ni kutoa huduma bora kwa watanzania waliojiunga na shirika hilo kwa wakati pindi wanapopata majanga mbalimbali.

“NIC ni Shirika la serikali lakini pia ni shirika la kibiashara la kutoa huduma za Bima za mali na ajali pamoja na bima za maisha ,shirika mwanzo lilikuwa haliwezi kutengeza faida hivyo lilikuwa likijiendesha kwa hasara,lakini kwa miaka minne mfululizo limekuwa likiendeshwa kwa faida ambapo kwa mfano rekodi ya mwaka 2020/21 tumeweza kutengeza faida ya shilingi bilioni 72.”amesema Meshack

Amesema Shirika hilo limeweza kutengeza faida kutokana na mapinduzi ya kimaendeleo katika maeneo matatu ikiwemo eneo la rasimaliwatu kwa kutafuta wataalam wenye weledi wa kuweza kuliendesha shirika pamoja na vijana wenye uwezo wa kufanya biashara

“Pia katika eneo la kimifumo ambapo shirika linaendeshwa kidigitali shughuli zote za kibima zinafanyika kwenye sytems na tumeanzisha mfumo ambao unatuwezesha kutoa huduma kwa wateja kwa haraka na ufanisi wa kiwango cha juu,

“Kwa mfano katika shirika letu ndani ya siku saba mteja anakuwa ameshapata huduma,ndani ya saa 24 mteja anapokuja kukata bima anatakiwa kuwa ameshahudumiwa na anaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Aidha amesema hivi sasa NIC lipo kwenye maeneo yote nchini lakini kwa sababu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia iliyopo mteja anaweza kupata huduma za kibima kwa kutumia NIC Kiganjani akiwa mahali popote ili mradi mteja awe na pesa kwenye simu yake ya kiganjani.

“Eneo lingine ni la kiubunifu , sasa hivi tume-‘restructure’ (tumetengeneza upya)  bidhaa zetu zote za kibima kwa mfano tunasukuma bidhaa moja ya Bimlife ambayo biashara hii imefanyiwa utafiti kwa ajili ya kwenda kujibu changamoto zinazomkumba mtanzania wa kawaida,

“Mfano hii Bimlife inatoa mafao ya msiba kwa mwanachama aliyepatwa na msiba ambapo haina maana kwamba fedha ya rambirambi ,na kwa kupata kwako fidia ya rambirambi haina maana kwamba itaenda kuchukua fedha ulizowekeza kwenye Bimlife,ukifika wakati wa kupata mafao yako unayapata kwa kiwago kile kile kwa mujibu wa mkataba lakini wakati huo masuala ya fidia au rambirambi yanakuwa kama bonus .

Meshack ametumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania wajiunge na NIC ili waweze  kupata huduma za bima kwa sababu ni shirika ambalo linalipa ,na linaloongoza kwa mtaji ndio maana ‘tunasema sisi ndio Bima wengine wanafuata’

Kwa  mujibu wa Meshack Shirika lipo kwa ajili ya kusapoti jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapasapot kwenye miradi ya kimaendeleo,kuwapa sapoti kwenye shughuli za kiserikali na watanzania wote kwa kurudisha kile kinachopatikana kwenye jamii.

“Kwa hiyo tunawashauri waje wakate bima mbalimbali,kwa mfano bima ya nyumba ,watu wanafikiri kuna thamani kubwa sana kukata bima ,nyumba ya milioni 100 ukiikatia bima NIC unalipia shilingi 177,000 kwa mwaka ,kwa hiyo upote nyumba yako ya milioni 100 uliyoisumbukia kwa miaka mingi kuijenga ndani ya dakika moja,ndio maana tunawakaribisha watanzania waje walitumie hili ni shirika lao.”amesisitiza


Share:

Kukosekana kwa huduma za MMMAM kunachangia kuwa na kundi kubwa la watoto waliokosa malezi bora

 

MKURUGENZI Msaidizi ,Ofisi ya Rais TAMISEMI nayeshughulikia Serikali za Mitaa Stephan Motambi akifungua kikao kazi cha tathimini  ya utekelezaji ya Mradi wa Mtoto Kwanza ambao kwa sasa unatekelezwa katika mikoa kumi Tanzania Bara.



BAADHI ya wadau wanaotekeleza mradi wa Mtoto kwanza wakiwa katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa Mtoto kwanza kilichofanyika jijini Dodoma.
i


      NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MKURUGENZI   Msaidizi Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Serikali za Mitaa Stephan Motambi amesema, kushindwa kufanya vizuri kwenye utoaji huduma za malezi,makuzi na maendeleo ya awali kwa watoto, kunachangia kuwa na kundi kubwa la watoto waliokosa malezi bora ambao wanakwenda kuwa mzigo kwa familia na Taifa kwa siku za baadaye.

Akifungua kikao cha wadau wa malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto jijini Dodoma kilichoandaliwa na Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Mtoto (TECDEN) Motambi amesema,hatua hiyo inasababisha kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kuhudumia watoto hao kuliko ambazo zingetumika katika malezi na makuzi yao.

“Sasa hivi tunahitaji kuajiri maafisa ustawi wengi ili wakashughulikie changamoto za watoto wa mitaani na fedha nyingi inatumika,lakini kama wangepata malezi mazuri wasingekuwepo  mitaani na hivyo fedha zinazotumika kuwahudumia hivi sasa zingefanya kazi nyingine kwenye Taifa.”amesema Motambi

Kufuatia hali hiyo amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka sekretarieti za mikoa kumi iliyoanza kutekeleza mradi wa Mtoto Kwanza kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha watoto wanakua na kufikia utumilifu wao na hatimaye kuwa na tija kwa Taifa lao.

“Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka sekretarieti za mikoa kumi iliyoanza kutekeleza mradi wa Mtoto Kwanza lazima muone kuwa hii  ni fursa ya kuonyesha umahiri wenu katika kutekeleza afua zinazohusu malezi ya watoto, na mara nyingi mlikuwa mkalamika kwamba hamna wadau au mradi wa kuwawezesha kuifikia jamii,

“Sasa mradi huu wa mtoto kwanza muutumie vizuri na mshiriki kikamilifu katika kuutekeleza kwa faida ya jamii na Taifa,kushindwa kufanikiwa kwa mradi huu kutasababishwa na sisi wenyewe kushindwa kutimiza majukumu yetu sawasawa ,kwa hiyo nawaomba maafisa wote ,mshiriki na mtoe matokeo ambayo ni kufanikiwa kwa utekelezaji wa  Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM ).Amesema Motambi 

Aidha amewataka watendaji wote wanaofanya uratibu katika ngazi mbalimbali wahakikishe kwamba Programu hiyo inatekelezwa kwa ufanisi ili dhima ya kuanzishwa kwa programu hiyo iweze kufanikiwa.

Awali Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (TECDEN) Mwajuma Rwebangila amesema Mradi wa Mtoto kwanza unatekelezwa katika mikoa 26 Tanzania Bara ingawa kwa sasa wameanza na mikoa 10 ya Lindi ,Mbeya,Tabora,Dodoma,Rukwa,Manyara,Arusha,Morogoro,Dar es Salaam na Kagera .  

Amesema,utekelezaji wa Mradi wa Mtoto kwanza umelenga katika kuchochea utekelezaji wa Programu Jumuishi ya MMMAM.  

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Action For Community Care (ACC)  linalotekeleza mradi wa Mtoto kwanza mkoani Dodoma Pendo Maiseli amesema,mwelekeo unaonyesha mradi huo kuleta ufanisi katika utekelezaji wa PJT-MMMAM.

Amesema,kwa kipindi cha miezi minne tangu wapatiwe elimu ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto wao kama wadau wanaotekeleza mradi huo wamefanikiwa kuwakutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yanayofanya shughuli za watoto na kuwapa uelewa kuhusu elimu ya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

“Vievile tumefanya uzinduzi wa PJT-MMMAM kwa mkoa wa Dodoma ambao umeshirikisha wadau wengi,pia tumefanikiwa kuwafikia na kutoa elimu hii kwa wazazi na walezi 328 ,haya ni mafanikio kwetu ambayo tunaona ni mwelekeo mzuri katika utekelezaji wa Programu ya Taifa ya MMMAM.”amesema Maiseli

Akielezea kuhusu changamoto amesema,bado wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu suala la malezi,makuzi na maendeleo ya mtoto huku akisema bado wadau wana kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu suala hilo.

Share:

Rais Samia awaagiza Mawakili wa Serikali kushugulikia haraka na kwa haki kesi za uwekezaji


 

RAIS Samia Suluhu Hassan

           NA JOYCE KASIKI,DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Mawakili wa Serikali kushughulikia kwa haraka  na haki kesi za uwekezaji kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi huku akipiga marufuku kusainiwa mikataba ya Serikali bila kushirikisha ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) .

Akizungumza leo Septemba 29 ,2022 mwaka huu jijini Dodoma kwenye Mkutano wa Chama cha Mawakili wa Serikali Rais Samia amesema,kwa kuishirikisha ofisi ya AG katika kusaini mikataba hiyo itakwenda kuleta maslahi mapana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Rais Samia ,huko nyuma mikataba ilisainiwa bila ofisi ya AG kujua  na wanapopata tatizo ndio wanaikumbuka ofisi hiyo na huenda wakati huo waliosaini wameshastaafu au wamtangulia mbele ya haki.

 “Ninyi ndiyo majeshi ya kulinda uchumi wetu kisheria ,uwekezaji lazima ulindwe lakini pia biashara lazima zilindwe,na watu kulinda hayo yote ni ninyi,ninyi ni walinzi wa kalamu na sheria siyo walinzi wa mabunduki kwa hiyo mwende mkalinde uchumi wetu ili nchi hii iweze kupokea wawekezaji wengi zaidi, tuwekeze na tukuze uchumi kwa maslahi mapana ya Taifa.”amesema Rais Samia

 Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema wizara inaanzisha mpango mahususi wa utoaji msaada wa kisheria ambao utaluwa endelevu kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao hawezi kumudu gharama.
Aidha amesema mpango huo utazinduliwa  Desemba 10 mwaka huu ambapo siku hiyo , ni siku ya haki duniani .


Share:

Wadau kutoka wilaya za Dodoma wakutana kujadili utelezaji wa PJT-MMMAM

AFISA Mradi,Mradi wa Mtoto kwanza Magret Mukama akifafanua jambo katika kikao kazi cha wadau kuhusu utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ( MMMAM) kilichofanyika jijini Dodoma

 



MATUKIO katika picha ni baadhi wadau walioshiriki katika kikao kazi hicho.



        NA JOYCE KASIKI,DODOMA

SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Malezi na Makuzi ya Watoto ‘Action for Community Care (ACC)’limewakutanisha Maafisa Maendeleo ya Jamii,Maafisa Ustawi na viongozi wa Dini kutoka wilaya  zote nane za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuweka mpango kazi wa pamoja katika utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Mtoto (PJT-MMMAM) ya mwaka 2021/22-2025/26 hadi katika ngazi ya jamii.

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuandaa mpango kazi huo Afisa Mradi katika Mradi wa Mtoto kwanza Magret Mukama amesema,kwa kuwakutanisha wadau inakwenda kuchochea utekelezaji wa Programu hiyo na hatimaye kujenga watu ambao watakuwa na tija katika Taifa.

 “Serikali inatekeleza Programua ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya Miaka mitano kwa kushirikiana na wadau mbalimbali,kwa hiyo leo tumewakutanisha wadau hawa tuweze kuwapitisha katika Mwongozo wa PJT-MMMAM nao waielewe na hatimaye waweze kufikisha elimu hii katika jamii kila mmoja kwa nafasi yake.”amesema Mukama

Wakizungumza katika kikao kazi hicho viongozi wa dini wamesema,Progframu hiyo imekuja kwa wakati muafaka na wao kama viongozi wa dini watatuia nafasi zao kuhakikisha elimu inafika kwa jamii ambayo ni waumini wao.

Kuhani Raha Halisi wa Kanisa halisi la Mungu Baba la wilayani Kondoa amesema,kwa kutumia nafasi zao watahakikisha ujumbe wa Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Mtoto unafika kwa waumini kupitia nyumba zao za ibada.

“Sisi viongozi wa Dini tuna watu wengi na tunaaminika,kwa hiyo hili jambo limekuja kwa wakati muafaka na sisi tutahakikisha tunashirikiana na Serikali katika utekelezaji wa suala hili ili watoto wapate malezi ambayo yatawafanya wakue vyema na baadaye kuleta tija katika Taifa.”amesema Kuhani huyo

Afisa Ustawi wa Jamii Elizabeth Shoo kutoka wilaya ya Kondoa amesema,wakati wa utekelezaji wa Programu hiyo utakidhi haja na kurejesha msingi wa malezi na makuzi ya watoto.

“Siku hizi na huu utandawazi uliopo kila mtu amekuwa ‘busy’ wazazi wamejisahau jukumu lao la malezi wameliacha kwa wasichana wa kazi,u-busy wa kutafuta pesa umefanya wazazi hawajui hata kuhusu ulinzi na usalama wa watoto wao,lakini kwa ujio wa Programu hii sasa wazazi watakwenda kuamka na kulea watoto kwa kufuata misingi iliyowekwa na kuwawezesha kukua kwa utimilifu wao.”amesema Shoo



Share:

Dkt.Mganga :Unywaji maziwa shuleni uanzie kwa wanafunzi wa darasa la awali kwani ndiyo wapo katika hatua za ukuaji

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Fatma Mganga akizungumza na wadau wa Maziwa nchini katika kongamano la wadau wa maziwa lililofanyika jijini Dodoma



BAADHI ya wadau wa Maziwa

WADAU wa Maziwa wakifautilia jambo kwenye kongamano la wadau wa maziwa lililofanyikaleo  jijini Dodoma


NA JOYCE KASIKI,DODOMA

                                                

KATIBU Tawala wa mkoa wa Dodoma Fatma Mganga amewataka viongozi wa mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatafakari namna ya kuanza kunywesha maziwa shuleni angalau kwa watoto wa darasa la awali hadi darasa la nne ili waweze kupata lishe na kukua vizuri.

Mbali na hilo Halmashauri zinaweza kutumia fedha kiasi cha shilingi 1000 kinachotengwa kwa ajili ya lishe shuleni kwa kila  mtoto kwa ajili ya kununua maziwa na kuwapa watoto ili waweze kuboresha afya zao badala ya kuzitumia katika masuala ambayo hayana tija kwa afya za watoto hao.

Dkt.Mganga maeysema hayo leo jijini hapa wakati akifungua kongamano la wadau wa maziwa ikiwa ni siku moja kabla ya kuadhimisha siku ya unywajimaziwa shuleni.

Amesema inawezekana idadi ya wanafunzi wa shule zote za msingi na sekondari wakawa wengi na hivyo kufanya mkoa kushindwa kumudu gharama ya shughuli hiyo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo malengo yatakayowekwa na wadau wa kongaman hilo yatauhusu mkoa wa Dodoma ambao umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya udumavu ambayo huenda pia inasababishwa na watoto kukosa kunywa maziwa.

 “Malengo hayo yatatufanya tukimbie ,na kwa  mkoa wa Dodoma mimi hayo malengo yatakuwa yananihusu sana,maana huwa tuna masuala ya lishe, hapa tuna fedha ambazo halmashauri wanaambiwa watenge fedha za lishe angalau kila mtoto shilingi 1000 ,

“Sasa nikawa nasema, kumbe hata hizi fedha kiasi fulani tunaweza kukitumia kwa kununua maziwa wakanywa watoto shuleni kwa sababu hiyo pia ni lishe ,lakini pia na sheria imeshatengenezwa kwamba shilingi 1000 hiyo  isitumike kwenye masuala tu ya kwenda kuangalia kitu fulani kuhusiana na masuala ya lishe  ,au unakuta imetumika kwenye ‘supervision’ ,kumbe ingetumika kununua maziwa watoto wangeboresha afya zao .”amesema na kuongeza kuwa

“Hata kama shule hatuwezi kunywesha watoto wote basi inyweshe kuanzia angalau chekechea’darasa la awali’ hadi darasa la tatu ,au la  nne ,kwa mfano hapa Dodoma tuna watoto kama laki tisa  hivi ..,watoto wa sekondarti kama laki tatu na laki sita  ni shule za msingi,lakini tukiangalia inawezekana laki sita ukawa mzigo mkubwa sasa labda tuchukue darasa la awali  hadi darasa la tatu au la nne ambao wapo kwenye umri wa kuendelea kukua, amesema na kuongeza kuwa

“Hivi unaweza kufikiria mtoto wa chekechea kinatakiwa kiwahi mwisho wasiku mtoto anakuja shule ana njaa,hakuna uji wala chakula chochote ,mtoto anaanza kuchukia shule tangu akiwa darasa la awali ,sasa ili watoto hawa wadogo waweze kupenda shule na kusoma ni kaunzisha miakati ya kunywa maziwa hasa kwa watoto wadogo wa darasa la awali mpaka darasa la nne.”amesema na kuongeza kuwa

“Tunaposema  udumavu, ni ukuaji wa mtoto unakua umeathirika sasa tukishakuwa na watu ambao hawakui vizuri sijui hilo linakwenda kuwa ni Taifa la aina gani maana yake ukuaji ni pamoja na ukuaji wa ubongo  kama ubongo haujaukua vizuri huyu mtu atakuwa na mikakati kweli yakuendeleza nchi ,anaweza kuwa na mikakati ya kuboresha uchumi?,haiwezekani sasa haya mambo ni ya msingi sana na tusilichukulie kama suala la kawaida.

Ameomba kongamano litoke na mikakati ambayo ndiyo itakuwa faida kwa wadau hao kufanya kongamano katika mkoa wa Dodoma na sisi watendaji tupate kitu cha kusmmamia na kuonyesha katika kongamano la mwaka ujao,tunaweza kualikwa tukatoa taarifa kwamba tumefanya hivi na hapo ndipo dhamira ya kweli itakapotimia .

Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Nchini Zacharia Masanjiwa amesema,bado kuna changamto ya unywaji maziwa hapa nchini huku akisema,licha yakuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na mifugo mingi katika Bara la Afrika lakini bado kuna changamoto ya unywaji maziwa ambapo mtu mmoja hunywa maziwa lita 62 badala ya lita 200 kwa mwaka.

“Lakini hata hivyo kwatakwimu hizo inawezekana wanaokunywa maziwa mengi ni watu wazima sasa tunataka tulenge kwa watoto katika kuhakikisha wanakunywa maziwa shuleni.”

Kwa upande wake Msajii wa Bodi ya Maziwa nchini George Msalya amesema,wadau lazima sasa waanze kutekeleza suala la unywaji maziwa shuleni kwa vitendo na siyo kuendelea kufanya kwa mazoea.

                                                                    

 



 

Share:

Wanachama zaidi ya milioni 2 wajitokeza kuwania nafasi ,NEC yaongeza muda wa kuchukua fomu ngazi ya mkoa na NEC Taifa

KATIBU wa Halamshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka

 

Wajumbe wa Halamshauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) jijini Dodoma ukumbi wa White House wakiwa katika kikao cha uteuzi wa wagombea ngazi ya wilaya
                

           

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa watu zaidi ya milioni mbili wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kuanzia ngazi ya mashina hadi Taifa.

Aidha Shaka amesema kuwa chama hicho kimeongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya Halamshauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) huku kionya wanaokiuka taratibu za chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa vikao vya juu vya chama hicho chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma vilivyoketi kwa ajili ya kufanya teuzi za wagombea wa nafasi za ngazi ya wilaya Shaka amesema,kwa watakaokiuka taratibu hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na kufuta chaguzi husika.

“Kamati Kuu ya CCM Taifa imeongeza muda wa kuchukua na kurejesha kwa hiyo kuanzia tarehe moja hadi tarehe tatu,zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa ngazi za mikoa na Taifa zoezi hilo litafanyika ,

“Kufunguliwa kwa dirisha hilo tutapata viongozi wengi zaidi ambao wanaingia kwenye ushindani hatimaye tuwekuwapata wale watakaowakilisha ngazi ya Taifa na ngazi ya mkoa.”amesema na kuongeza kuwa

“Eneo moja tutakalosimamia kwa nguvu zote ni eneo la matumizi mabaya ya madaraka kwa maana kwamba kutumia rushwa ili kuweza kupata madaraka ya uongozi ,hii ni kuhakikisha tunapata viongozi bora na siyo bora viongozi.”

Aidha amesema hatua ya wanachaa zaidi ya milioni mbili kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho inaonyesha jinsi ambavyo chama hicho kina watu wengi na wenye sifa za uongozi.

Shaka amesema,Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na mambo mengine imefanya uteuzi wa mwisho wa nafasi za wagombea wangazi za wilaya nchi nzima.

“Kwa hiyo tumeteua na tumeshapata wagombea ambao watakwenda kusimama kwenye uchaguzi wa ngazi ya wilaya ambao utafanyika Oktoba Mosi na mbili mwaka huu nchi nzima”amesema Shaka

Amewataka wanachama wote wenye sifa ya kushiriki kuwachagua viongozi hao wa wilaya wajitokeze kwa wingi katika maeneo yao katika tarehe hizo kwa mujibu wa ratiba ambazo zitapangwa na mkoa na ngazi ya wilaya.                        


Share:

Wanufaika 640 wa Samia scholarship kugharimu sh.3 bilioni

 

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknlojia Profesa Adolf Mkenda 

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema ufadhili wa 'SAMIA SCHOLARSHIP' una thamani ya shilingi   bilioni 3 Huku akisema katika ufadhili huo ,Serikali itagharamia kwa asilimia (100%) masomo ya chuo Kikuu kwa wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za Teknojia,Uhandisi,Hisabati na Tiba huku wanafunzi 640 wakichaguliwa katika ufadhili huo.

Akizungumza leo Septemba 27,2022  jijini Dodoma Profess Mkenda amesema ufadhili huo no maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kidato Cha sita waliopata ufadhili wa juu katika mtihani wa Taifa mwaka 2022.

Amesema mwanafunzi mwenye sifa ya kupata ufadhili huo ni yule ambaye amepata udahili katika katika programu za Sayansi, teknolojia, uhandisi, Hisabati au tiba katika chuo kikuu hapa nchini kinachotambuliwa na Serikali ambazo zimetajwakatika kundi la kwanza (Cluster) katika mwongozo wa utoaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2022/2023.

"Ufadhili huu ni kwa vyuo vya hapa nchini lakini pia ni kwa wale wanafunzi waliopata udahili katika tahasusi zilizotajwa na katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali."amesema Prof.Mkenda

Aidha amesema kuwa Ufadhili huo utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kugharamia maeneo yafuatayo ambapo ni Ada ya Mafunzo ,Posho ya chakula na malazi,Posho ya Vitabu na Viandikwa Mahitaji Maalum ya Vitivo Mafunzo kwa Vitendo ,Utafiti Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu,Bima ya Afya na Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharamiwa kati ya miaka mitatu (03) hadi mitano (05) kulingana na programu husika walizodahiliwa.

"Maombi ya Samia Scholarship yatawasilishwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku 14 kuanzia Septemba 28, 2022." Amesema ptof Mkenda na kuongeza kuwa

"Ufadhili huu ni wa asilimia mia moja ambao kikomo chake kitazingatia miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.Orodha ya majina ya wanafunzi husika inapatikana kupitia www.moe.go.tz na www.heslb.go.tz .


UCHAMBUZI WA WANUFAIKA 640 wa SAMIA SCHOLARSHIP

Kuhusu uwiano wa kijinsia wa wanufaika 640 wa Samia Scholarship  prof.Mkenda alisema  Wasichana 244 sawa na asilimia 38% na Wavulana ni 396 sawa na asilimia 62% ambapo Wanafunzi kutoka shule za serikali ni 396 sawa na asilimia 62% wakati Wanafunzi kutoka shule za binafsi ni 244 sawa na asilimia 38%.

"Wanafunzi wenye ufaulu wa juu kiwango cha Alama tatu (3) ni 60 (9%)Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Visiwani ni 43 (7%)Wanafunzi kutoka shule za Tanzania Bara 597 (93%)"

Aidha amesema,jumla ya wanafunzi 11 wenye mahitaji maalumu watanufaika na Samia Scholarship.Hawa ni asilimia 100 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu waliopata darala la kwanza katika tahasusi zinazolengwa na Samia Scholarship mwaka 2022/23

Shule zilizotia fora kwa kuwa na idadi kubwa za wanufaika wa Samia Scholarship ni pamoja na Tabora Boys wanafunzi 79 (12%)St.Mary’s Mazinde Juu wanafunzi 51 (8%)Mzumbe Sekondari wanafunzi 46 (7%)Tabora Girls 39 (6%)Kisimili wanafunzi 31 (5%)

Kwa upande wake Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdugulam Hussein alisema kuwa ufadhili huo utaongeza chachu kwa wanafunzi wengi kusoma masomo ya Sayansi,Teknolojia, uhandisi,Hisabati na Tiba.

"Idadi iliyopo mwaka huu naamini mwakani itaongezeka sana hivyo Mhe.Mkenda kama utaweza kuongea na Mhe.Rais tena aongeze walau Bilion zingine 3 kwa mwakani ziwe 6 kwa sababu naamini idadi itaongezeka maradufu kutokana na hamasa hii,"Amesema Mhe.Ali Abdugulam Hussein 

Share:

Wadau waaswa kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa PJT-MMMAM

 


MKURUGENZI wa Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Watoto ( TECDEN) akiwa katika hafla ya uzinduzi wa PJT-MMMAM ngazi ya mkoa (mkoa wa Dodoma)


MKURUGENZI wa Shirika liliso la Kiserikali Action for Community Care (ACC) linalotekeleza mradi wa toto Kwanza Pendo Maiseli 


BAADHI ya wadau wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) mkoa wa Dodoma.

NA JOYCE KASIKI,DODOMA

MKURUGENZI wa Mtandao wa Malezi na Makuzi ya Watoto nchini (TECDEN) Mwajuma Rwebangila amewaasa wadau wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wenye malengo ya watoto washirikiane na Serikali kuhakikisha Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto  (PJT-MMMAM) itakayowezesha watoto kulelewa na kufikia utimilifu wao.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa Programu hiyo kwa ngazi ya mkoa,Mkurugenzi huyo amesema,wadau  wana kila sabahu ya kuelimisha jamii umuhimu wa kuwekeza kwa watoto wadogo .

“Kuwekeza kwa watoto wadogo ni muhimu sana,inawezekana Taifa tunalolieona sasa hivi lina mwanzo wake ,na tunaamini kwamba ukibadilisha mwanzo wa hadithi ,umebadilisha hadithi nzima,

“Kwa hiyo tubadilishe mwanzo wa hadithi toka mimba inatungwa mtoto alelewe katika kuhakikisha anakuwa na afya bora,lishe ya kutosha,ulinzi na usalama wa mtoto,Malezi yenye mwitikio na fursa za ujifunzaji wa awali.”amesema Rwebangila na kuongeza kuwa

“Watoto wapewe fursa za kucheza ,na kwa kucheza mtoto anajifunza vitu mbalimbali,anaweza kutengeneza kitu na ukimwambia akuelezee atafanya hivyo,hiyo inatosha kufanya akili na ubongo wake kufanya kazi kwa haraka.”

Kwa mujibu wa Rwebangila  TECDEN wanashirikiana na Umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) kupitia Shirika lisilo la kiserikali linaoshughulika na masuala ya Malezi na Makuzi ya Watoto (CiC) linalotekeleza mradi wa miaka mitatu wa Mtoto kwanza.

Rwebangila amesema,mradi huo umelenga kuchochea utekelezaji wa PJT-MMMAM katika kuhamasisha sekretarieti za mikoa kuhakikisha Programu hiyo kubwa ya Taifa inafahamika na itekelezwa katika ngazi za Mikoa na Halmashauri.

Naye Meneja Programu Mradi wa Mtoto kwanza unatekelezwa mkoani Dodoma na  Shirika lisilo la Kiserikali la Action For Community Care (ACC) Magret Mukama amesema,mradi huo umejikita kusaidia watoto walio na umri wa miaka 0-8 ili kuharakisha upatikanaji wa matokeo chanya ya Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika utoaji wa huduma za malezi jumuishi .

 “Maana wataalam wanasema katika kipindi hicho mtoto ubongo wa  mtoto unakua kwa kasi na mtoto anakuwa na uwezo wa kujifunza na kuelewa kwa haraka ,ndiyo maana mradi umejikita katika kusaidia kundi la watoto hao kwa ajili kuwa na Taifa lenye tija kwa Taifa hapo baadaye.”alisema Mukama

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Salome Francis amesema, mpaka sasa Programu imeziduliwa kwenye Mikoa tisa  ya Tabora, Morogoro,Lindi, Arusha, Manyara, Mbeya, Rukwa, Kagera na Dar Es Salaam huku Dodoma ukiwa mkoa wa 10 Kuzindua programu hiyo.

Aidha amesema, baada ya uzinduzi huo wataalam kutoka kada mablimbali za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Afya, Lishe, Elimu, na Mipango Pamoja na Asasi za Kiraia kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma  watajengewa uelewa kuhusu PJT-MMMAM na baadae kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa kipindi cha mwaka mmoja kwa kila Wilaya ambao utasaidia katika kupima utekelezaji wa Programu.






Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.