Mkurugenzi wa T-Pesa Lulu Mkudde akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye maoneaho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam .
Na Joyce Kasiki Dar Es Salaam
SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL) limesema ,hadi sasa limesambaza mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini huku zaidi ya wilaya 98 nazo zikiwa zimefikiwa na mkongo huo ambao unarahisisha mawasiliano na kuleta matokeo chanya kwenye shughuli za kiuchumi
Hayo yamesemwa leo Julai 12 na Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL Pesa Lulu Mkudde wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Amesema juhudi hizo zote zinalenga katika upatikanaji wa huduma za elimu ,afya na maendeleo kwa ujumla yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini .
Amewahakikishia wananchi kwamba TTCL itahakikisha huduma za mawasiliano zinakuwa nzuri ili kuwapa fursa wananchi kupata huduma mbalimbali lakini nao kujiingizia kipato kupitia mtandao bora wa TTCL kwa gharama nafuu.
Kwa mujibu wa Mkudde Mkongo wa Taifa ni moja ya miradi ya kimkakati inayofanywa na TTCL huku akiitaja miradi mingine kuwa ni kutoa mafunzo mbalimbali , kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu.
Kuhusu ushiriki wao kwenye maonesho hayo amesema,katika kuunga mkono kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu isemayo Tanzania ni mahalo sahihi pa uwekezaji Mkkude amesema, wanatumia fursa hiyo kufungua milango kwa wawekezaji na wafanyabiashara kufanya kazi zao kidigitali na kuleta matokeo chanya.
Vile vile amesema katika maonesho hayo TTCL limekuja na huduma ya mtandao (WiFI T-Cafe ) ambayo imelenga kuwaondolea adha wafanyabiashara, waandishi wa habari na wataalam wa masuala ya ushauri na yeyote anayetaka kufanya kazi nje ya ofisi yake ,na kupata huduma hiyo bure.
Pia amezungumzia huduma ya 'fiber nyumbani kwako' inayopatikana kwa gharama nafuu ambapo amesema elomu ya huduma imetolewa kipindi chote cha maonesho.
"Na tayari tumepokea maombi mapya mengi ,wanaohitaji huduma ambayo imekuja kuleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifufushi vya kawaida, ambapo sasa shirika limeleta huduma hii ambayo inamwezesha mteja kutumia internent ambayo haina ukomo.
Amewasihi wananchi ambao bado hawajaomba nafasi hiyo kutumia tovuti www.ttcl.co.tz kisha taarifa zao zitachukuliwa na kuanza mchakato wa kuwafungia huduma hiyo .
Katika hatua nyingine amesema shirika katika huduma yake ya T-Pesa wamekuja na huduma ya akaunti ambayo inamwezesha mteja kufungua akaunti ya TTCL Pesa bila kuwa na hitaji la sim card.