Elimu ya VETA yamsaidia kijana kujikwamua kiuchumi na kuajiri wengine




Published from Blogger Prime Android App

Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

MWANAFUNZI  aliyekuwa akisoma kozi ya Hoteli na Utalii katika Chuo cha VETA Njiro Fredrck Mlay , amefanikiwa kuibadili kabisa hali yake ya kiuchumi na kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine kwa kujiajiri mwenyewe baada ya kuhitimu masomo yake.

 Fredrick alianza kozi hiyo mwaka 2023 na kuhitimu Mei 2025 akiwa na Cheti na Diploma, elimu ambayo imekuwa nguzo kubwa ya mafanikio yake ya sasa.

Kupitia kiwango cha cheti, alipata maarifa kuhusu jinsi ya kuongeza idadi ya watalii wanaovutiwa na mbuga za wanyama  huku kiwango cha diploma kikimuwezesha kuelewa mbinu za ubunifu na uuzaji wa vinywaji mbalimbali katika hoteli  ikiwa ni pamoja na vinywaji vikali na laini vinavyotengenezwa kwa matunda.

Akizungumza Julai 2,2025  katika Banda la VETA kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya 49  Fredrick amesema,"Elimu ya VETA imenipa ujuzi ambao umeniwezesha kujiamini, kujiendeleza na sasa kuajiri vijana wenzangu,”

Fredrick amesema kwa   anatengeneza vinywaji kama juisi , cocktails na pombe kali , akitumia matunda na viambato halali. Vinywaji hivyo hutumika katika hafla mbalimbali kama harusi na matamasha.

Aidha amesema, alichagua kozi hiyo ili aweze kuitumia kama daraja la kujiajiri. "Katika kozi hii nimejifunza mengi  ikiwemo namna ya kuhudumia wageni, masoko, usimamizi wa shughuli, pamoja na kutengeneza cocktails kwa kutumia matunda na alcohol,” anaeleza.

Mbali na kujiajiri amesema elimu hiyo imemsaidia pia kuwa sehemu ya suluhisho kwa vijana wasiokuwa na ajira ambapo kwenye shughuli zake, huwashirikisha vijana ambao wengi wao hawakuwa na ujuzi, lakini sasa wanajifunza, wanapata uzoefu na kipato.

“Katika kazi zangu, hasa kwenye matukio kama harusi na sherehe, huwa nachukua vijana kufanya kazi nami. Hii imenisaidia mimi kiuchumi na pia kuwapa wao fursa ya kipato na maarifa. Wengine wameendelea na kazi hadi sasa,” anasema kwa fahari.

Kijana huyo amesema,mpango wake wa baadaye ni kufungua mgahawa mkubwa wa kisasa, ambao utatoa ajira kwa vijana wengi zaidi wakiwemo wale ambao hawakubahatika kusoma VETA kutokana na changamoto mbalimbali.

Anahitimisha kwa kuwasihi vijana wa Kitanzania kujiunga na vyuo vya VETA ili wapate ujuzi wa kuwasaidia kujiendeleza kimaisha na kuchangia katika maendeleo ya taifa. “Ujuzi ndio msingi wa mafanikio ya kweli, na VETA ndio sehemu sahihi ya kuanzia,” amesema.













Share:

TMDA yaendelea kuhakikisha Usalama wa Dawa Sokoni — Mkurugenzi Mkuu



Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

 
MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA), Dkt. Adam Fimbo, amesema kuwa TMDA inaendelea kuhakikisha kuwa dawa zinazosambazwa na kutumiwa na wananchi nchini ni salama, zenye ubora unaokubalika na zinafanya kazi iliyokusudiwa bila kusababisha madhara kwa binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3,2025  katika Banda la TMDA kwenye Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Dkt. Fimbo alisema moja ya majukumu makuu ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa kila dawa inayotumiwa na binadamu haimdhuru, bali inamponya kwa mujibu wa madhumuni ya matumizi yake.

 “Dawa yoyote inayotumiwa na binadamu haipaswi kumdhuru, Jukumu letu kama TMDA ni kuhakikisha dawa hiyo inafanya kazi iliyokusudiwa , yaani inatibu, siyo kuleta madhara,” alisisitiza Dkt. Fimbo.

Alieleza kuwa TMDA hufuatilia kwa ukaribu madhara yanayoweza kujitokeza kwa watumiaji wa dawa baada ya matumizi na huchukua hatua stahiki ili kuzuia madhara zaidi kwa umma.

 Aidha, alisema mamlaka hiyo imewekeza katika maabara za kisasa ambazo zimethibitishwa kimataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO), na ni miongoni mwa maabara chache zenye uwezo mkubwa wa kupima ubora wa dawa barani Afrika.

 “Tunapima bidhaa za dawa kwenye maabara zetu zilizoidhinishwa na WHO,maabara yetu ni miongoni mwa maabara Bora Afrika zenye viwango vya kinataifa"amesisitiza

Ni maabara chache za aina hii, na sisi ni miongoni mwao. Hivyo, tunaruhusu dawa tu ambazo zimekidhi viwango vilivyowekwa kimataifa,” alieleza.

Mbali na udhibiti wa dawa amesema , TMDA pia inasimamia bidhaa za tumbaku, kwa lengo la kuwalinda wananchi dhidi ya madhara yanayotokana na matumizi ya bidhaa hizo.

 Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi ya kudhibiti usambazaji na matumizi holela ya bidhaa hizo ili kuhakikisha usalama wa afya ya jamii.

 Dkt. Fimbo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na TMDA kwa kutoa taarifa za dawa au bidhaa zinazohisiwa kuwa na madhara, ili kuchukua hatua za haraka.

Aidha Fimbo ametumia nafasi hiyo kuwaasa  wananchi wote kufika katika banda hilo  kupata elimu kuhusu usalama wa dawa, vifaa tiba, na vitendanishi .

Share:

Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

Published from Blogger Prime Android App


🔴🔴Mazingira Wezeshi ya Serikali Yafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Kupitia TAWA

📍  Milango ya uwekezaji bado iko wazi

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuimarisha mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hatua inayolenga kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta mbalimbali, hususan sekta ya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa TAWA, Bw. Beatus Maganja, amesema taasisi hiyo inaendelea kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza  katika maeneo mbalimbali ikiwemo utalii wa picha na uwindaji wa kitalii.

“Tunawaambia Watanzania na wawekezaji  wote kwa ujumla kuwa TAWA ni mahali sahihi kwa uwekezaji, unapotaka kuwekeza unakaribishwa sana. Ikumbukwe kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa mazingira wezeshi Kwa wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi yetu ” alisema Maganja.

"Kama alivyofanya Mhe. Rais na sisi tunamuunga mkono Kwa kuhakikisha kwamba fursa hizi zinakuwa wazi Kwa wawekezaji wote na ndio maana tuko hapa kuwatangazia waje kuwekeza katika hii taasisi" amesisitiza Afisa Habari huyo.

Aidha Maganja ameongeza kuwa TAWA inasimamia maeneo yenye rasilimali adimu, vivutio vya kipekee, na mandhari ya kuvutia ambayo yanatoa fursa kubwa ya uwekezaji endelevu kwa maslahi ya taifa na uhifadhi wa maliasili.

Bw. Maganja alitaja baadhi ya maeneo yaliyo  tayari kwa uwekezaji kuwa ni Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park (Arusha), Wami-Mbiki (Morogoro), Mpanga/Kipengere (Mbeya na Njombe), Tabora ZOO, Ruhila ZOO na maeneo mengine mengi yenye fursa mbalimbali.

Kwa upande wake, Afisa Mhifadhi Mkuu kutoka TAWA, Dkt. Gladson Mlay, aliwahamasisha wananchi kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho hayo, ambapo wanaweza kujionea wanyamapori hai wakiwemo simba, chui, fisi, mamba na spishi mbalimbali za ndege.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaalika wananchi kuonja na kununua kitoweo cha nyamapori choma kilichoandaliwa kwa umahiri, akisema kuwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha matumizi ya rasilimali za maliasili kwa njia endelevu.

“Kwa wale ambao wanasema hawajawahi Kula nyamapori choma, nyama hiyo ipo hapa, mishikaki pia ipo na nyama ya kupeleka nyumbani nyumbani. Kwahiyo watu  wote mnakaribishwa mje kuonja, Kula na kuona ka
Kweli maliasili ni za kwetu wote” alisema Dkt. Mlay
Share:

Wazazi wasaidizi wa ndoto, safari ya kukuza vipaji vya watoto





Published from Blogger Prime Android App
Mtoto akiwa katika  banda la VETA kitengo cha ushauri 



Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM


WAZAZI wameaswa kutokatiza vipaji na ndoto za watoto wao kwa kuwachapa au kuwakanya wasirudie kufanya kitu ambacho wao wanadhani ni uharibifu kumbe ndiyo kipaji Cha mtoto ambacho kinapaswa kiendelezwe.

Akizungumza Julai Mosi 2025 katika maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba katika Banda la VETA kitengo cha ushauri,Mwalimu anayefundisha somo la electronics Rick Sambo kutoka VETA  amesema ,mtoto anapofanya kitu labda amevunja au amefungua radio ,ina maana anaanza kuonyesha mapema kuwa hicho ndiyo kipaji chake.

"Kwa mfano, kuna mtoto anayeonekana ni mtundu kila mara anafungua redio, pasi, au vifaa vya umeme vilivyo karibu,kwa macho ya mzazi, hilo linaweza kuonekana kama utundu au uharibifu wa mali,

" Mara nyingi, matokeo yake ni mtoto kuchapwa au kukemewa,lakini kwa macho ya VETA, hapo ndipo vipaji vinapojificha,mtoto huyo anahitaji kuelekezwa, si kukataliwa."amesema Mwalimu huyo

Amesema,kufuatia hali hiyo,katika Banda lao ,wameanzisha kitengo cha ushauri ili waweze kuwasaidia katika kugundua vipaji vya watoto na kuwaelekeza wazazi cha kufanya ili kuendeleza vipaji vya watoto hao.

"Katika banda letu, tunapokea watu wa rika mbalimbali  kutoka watoto wadogo hadi watu wazima  ambao hawana elimu rasmi ya ufundi lakini wana vipaji vya asili,

"Na kwa sababu watoto wengi wanakuwa wameshasoma mambo mengi kwa nadharia,wakifika hapa tunawaonyesha vifaa vya umeme na electronics  na kuwapa  ushauri kuhusu namna ya kuanza kujifunza taaluma hizo kwa usahihi na usalama."amesisitiza Mwalimu huyo

Vile vile amewaasa wazazi kuangalia nini mtoto anahitaji kusoma ili mtoto asipoteze muda kwa kusomea kitu ambacho anakitaka mzazi.

"Unakuta mtoto anahitaji kusomea fani Fulani,lakini mzazi hataki hiyo anataka mwanae asomee kitu kingine kabisa na anachotaka mtoto,sasa wazazi kama hao wakifika kwenye Banda letu wakiwa na watoto wao tunawashauri na mambo ya naenda sawa." amesisitiza na kuongeza

" Kwa hiyo tunawaleta wazazi na watoto pamoja ili kuwasaidia kuelewana mzazi asikilize ndoto ya mtoto, na mtoto apewe mwongozo wa kitaaluma. Kwa kufanya hivyo, tunamjenga mtoto kuwa mtaalamu bora wa baadaye





Share:

UDOM yaibuka na Dawa za Asili: Tiba Mpya kwa Malaria, Vidonda vya Tumbo na Kisukari


Published from Blogger Prime Android App


Na Joyce Kasiki,DAR ES SALAAM

CHUO  Kikuu cha Dodoma (UDOM) ubunifu wa tiba mpya kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 49 Sabasaba , unaotegemea rasilimali za asili za mimea ya Kitanzania.

Mwalimu Dismas Tullo ambaye ni mmoja wa wabunifu hao kutoka UDOM, amefichua kuwa chuo hicho kimefanikiwa kubuni dawa tatu mpya zinazoweza kuwa suluhisho kwa maradhi sugu kama malaria, vidonda vya tumbo na kisukari,changamoto zinazotikisa maisha ya maelfu ya Watanzania kila siku.

Akizungumza Juni 30 ,2025 kwenye maonyesho hayo katika Banda la chuo hicho Tullo amesema ,"Tumetumia rasilimali zetu za mimea na mizizi ya asili kutengeneza dawa ambazo tayari zimeanza kuonyesha matokeo chanya kwa wagonjwa waliopatiwa dawa hizo ,” alisema Tullo 

Dawa Tatu Zinazolenga Suluhisho Endelevu

Dawa ya kwanza ni Gymerine, ambayo inalenga kudhibiti ugonjwa wa kisukari. Tullo amesema dawa hiyo tayari imefanyiwa majaribio ya awali katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na baadhi ya wagonjwa waliotumia wameripoti kuimarika kwa afya zao.

Kwa upande wa vidonda vya tumbo, UDOM imebuni dawa iitwayo Ulcerexia, ambayo kwa sasa ipo kwenye hatua za majaribio, lakini wagonjwa waliotumika kama sampuli wameripoti nafuu kubwa na dalili za kupona.

Lakini pengine uvumbuzi wa kusisimua zaidi ni Malaherb  dawa mbadala ya malaria ambayo Tullo anasema ni rahisi zaidi kwa mgonjwa kuitumia tofauti na dawa mseto zilizopo sasa.

“Kwa sasa, dawa mseto ndiyo inatumika kutibu malaria, lakini changamoto kubwa ni kwamba wagonjwa wengi hushindwa kumaliza dozi kutokana na wingi wa vidonge. Hali hiyo husababisha malaria kujirudia na kusababisha matatizo mengine kama ya figo. Malaherb ni dozi fupi, rahisi kutumia, na haina madhara kwa sababu haina kemikali,” alieleza.

Mbali na Dawa, UDOM Yaleta Lishe Tiba

Mbali na dawa hizo, Tullo amesema UDOM pia imebuni lishe maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari na ini, watoto wenye utapiamlo, pamoja na watu wanaoishi na VVU. Lishe hiyo imeundwa kwa kutumia vyakula asilia visivyoongezwa viuatilifu hatari, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutibu kwa njia salama zaidi.

Tiba Asili Zinavyoweka Tanzania kwenye Ramani ya Kisayansi

Bunifu hizi kutoka UDOM si tu zinathibitisha uwezo wa wasomi wa ndani ya nchi kutoa suluhisho kwa matatizo ya kiafya, bali pia zinaashiria mwelekeo mpya wa Tanzania katika kutegemea tiba asilia kama mbadala wa dawa za viwandani.

Katika dunia inayoshuhudia ongezeko la usugu wa dawa na madhara ya viuatilifu, hatua kama hizi zinaweza kuwa mwanzo wa mageuzi makubwa katika sekta ya afya nchini.

Wakati Maonyesho ya Sabasaba yakiendelea, banda la UDOM limekuwa kielelezo cha kile kinachowezekana tukitumia maarifa, maliasili na dhamira ya dhati kubadilisha maisha ya Watanzania.

Share:

Watumishi Wizara ya Fedha waagizwa kufanya kazi kwa bidii



Published from Blogger Prime Android App



Na. Farida Ramadhani, WF, Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaagiza viongozi na watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu ili kuendelea kusimamia uchumi wa nchi.

Ametoa agizo hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba, wakati wa Kikao cha watumishi wa Wizara hiyo ambacho kinatoa fursa kwa watumishi kukutana kwa pamoja, kukumbushana na kubadilishana uzoefu, taarifa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Serikali kwa ujumla.

Dkt. Nchemba aliwakumbusha watumishi hao kutambua kuwa Wizara ya Fedha ni moyo wa Serikali hivyo ikiyumba tu nchi itayumba na kuleta madhara kijamii na kiuchumi.

Aliwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano pamoja na kufanya marekebisho katika maeneo yenye changamoto ili kuboresha utendaji wao na kufikia malengo yaliyowekwa.

”Tutumie kikao hiki kurekebisha maeneo yote yenye changamoto, hakuna binadamu aliyekamilika na ukijiona mkamilifu ujue unamkufuru Mwenyezi Mungu, hivyo inabidi tukubali kubadilika ili kuboresha utendaji wetu”, Alisisitiza Dkt. Nchemba.

Aidha, aliwapongeza watumishi hao kwa kufanya kazi kwa weledi na kuiwezesha nchi kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na kuhimili changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea ulimwenguni.

’’Mmekuwa mstari wa mbele kuliwezesha Taifa kuhimili misukusuko ya kiuchumi chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na usimamizi imara wa uchumi unaendelea licha ya misukosuko inayoendelea duniani’’, alibainisha Dkt. Nchemba.

Aliongeza kuwa utendaji wa watumishi wa Wizara hiyo umeiwezesha nchi kutekeleza miradi ya maendeleo lakini pia kuwaongezea sifa binafsi Waziri na Naibu wake Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb).

Dkt. Nchemba alisema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kufanya vizuri zaidi katika majukumu yao na kuiwezesha nchi kufikia malengo yake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, aliwaasa Watumishi wa Wizara hiyo kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mapato na matumizi ya mali na fedha za umma ili kufikia malengo ya Serikali katika mwaka wa fedha 2025/26.

Alisema ni muhimu kwa watumishi hao kutumia weledi na uzoefu walionao kuongeza tija katika usimamizi wa sera, sheria, kanuni na miongozo ya masuala ya fedha na bajeti ili kuwezesha Wizara kutekeleza kwa ufanisi malengo yake na Serikali kwa ujumla.

”Ninapenda kuwakumbusha watumishi wote kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia malengo, shabaha na mpango na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge pamoja na kutunza siri na kuhifadhi nyaraka muhimu za Wizara na Serikali kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Mwamba. 

Aliwataka Wakuu wa Idara/Vitengo pamoja na watumishi wote kuzingatia maelekezo hayo kwa ukamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo alisisitiza umuhimu wa kufanyakazi kwa upendo, umoja na mshikamano pamoja na kuendelea kusimamia maadili ya kazi ili kuwezesha wote kufikia malengo yao. 

”Wote tunategemeana hakuna mtu anayejua kila kitu, hivyo ni muhimu kupeana nafasi ya kuweza kufikia mafanikio yetu, hakuna mtu anayeweza kufanikiwa bila kuwezeshwa”, alisisitiza Bi. Omolo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Usimamizi wa Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya, aliwapongeza watumishi wa Wizara hiyo kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa majukumu yao.

Alisema watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo, kujitolea na kukesha kuhakikisha shughuli mbalimbali za Serikali zinatekelezwa kwa wakati na kwa mafanikio makubwa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayesimamia Fedha za Umma, Bi. Amina Khamis Shaaban alisisitiza Wizara hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa fedha za ndani ili kuwezesha nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Aidha alihimiza watumishi wa Wizara hiyo kusimamia upatikanaji wa mikopo nafuu ili kuiwezesha nchi kutumia fedha hizo kama kichocheo cha kujenga uwezo wa ndani na kujinasua kwenye utegemezi wa muda mrefu.

Bi. Amina aliongeza kuwa katika kupunguza utegemezi huo suala la Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ni muhimu, na kusisitiza watumishi wa Wizara hiyo hususan wale wanaohusika na PPP kuibua na kusimamia kikamilifu miradi ya ubia.

Kwa upande wao Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA (T), Leonard Mkude na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai, walisema kuwa ushirikiano uliotolewa na watumishi umewezesha wizara kukamilisha majukumu ya kimalipo katika mwaka wa fedha 2024/25.

Aidha, waliongeza kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo imeweza kutekelezwa pamoja na kukamilisha ufuatiliaji na tathmini katika miradi hiyo.

Katika kikao hicho viongozi walihimiza utulivu, uwajibikaji, uadilifu, kutunza siri na mali za umma pamoja na kujilinda katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali huku wakisisitiza watumishi hao kushiriki zoezi hilo kikamilifu kwa maslahi mapana ya nchi.


Share:

Ushiriki wa TAWA katika maonyesho ya 49 Ya Biashara ya Kimataifa



Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App
Picha mbalimbali zikionesha wananchi walivyotembelea na kuvutia na banda la Maliasili na utalii


Katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kwa mwaka 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam smbapo,kupitia maonesho haya, TAWA inatumia fursa hii kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali zinazohusiana na utalii na uhifadhi zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

📍Unapotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, utakutana na maofisa wa TAWA ambao watakupa maelezo kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo,fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika maeneo mbalimbali yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA, ikiwa ni pamoja na:Makuyuni Wildlife Park (Arusha),Pande (Dar es Salaam),Wami-Mbiki (Morogoro na Pwani),Tabora Zoo (Tabora),Ruhila Zoo (Ruvuma) .

Pia unapata fursa ya Kujionea Wanyamapori Hai kupitia bustani ya wanyamapori iliyopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa viingilio vya bei nafuu kwa Watanzania,vivutio vya Utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAWA, pamoja na taarifa za gharama na namna ya kuyatembelea na ofa  Maalum ya Ziara ya kutembelea Hifadhi ya Pande, iliyopo Jijini Dar es Salaam, kwa gharama nafuu katika msimu huu wa Maonesho ya Sabasaba.

Aidha ,utsona shughuli za Utalii na Uhifadhi zinazofanywa na TAWA, ikiwa ni pamoja na elimu kwa umma kuhusu namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, na kuelewa tabia zao na fursa ya Kufurahia Nyamapori Choma iliyoandaliwa kwa umahiri na kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu Kwa bei ya kizalendo.

Wananchi wote mnakaribishwa kkwa wingi katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, mjifunze, muelimike na mjionee huduma na vivutio vya kipekee, hasa wanyamapori hai waliopo ndani ya banda hilo.








Share:

TTCL kutoa huduma inayojibu mahitaji halisi ya sasa



Published from Blogger Prime Android App


Published from Blogger Prime Android App




Na Mwandishi wetu

 Meneja wa Banda la Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL)   Janeth Maeda, ametoa wito kwa Watanzania na washiriki wote wa maonesho ya Kimataifa ya  Biashara ya 49 yanayoendelea jijini Dar es Salaam , kutembelea banda la TTCL  ili kujionea huduma za kibunifu zinazojibu mahitaji halisi ya sasa ya taasisi, mashirika, sekta binafsi na wananchi wa kawaida.

Akizungumza katika banda hilo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere  Juni 30,2025 ,Mawda amesema 
“TTCL ni suluhisho la sasa na la baadaye katika huduma za TEHAMA,na hii ndiyo sababu Serikali imeendelea kutuamini kusimamia miundombinu ya kitaifa yenye umuhimu mkubwa kwa usalama wa Taifa na maendeleo ya uchumi,” alisema Maeda.

Amesema TTCL inashiriki maonesho haya ili kuuhabarisha umma kuhusu namna shirika hilo linavyotekeleza wajibu wake kwa wananchi, likiwa limeaminiwa na Serikali kusimamia miundombinu ya kimkakati ya Taifa ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC).

Maeda amebainisha kuwa kupitia huduma hizo, TTCL inatoa mchango mkubwa katika kuboresha utendaji wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi. huku akizitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Wizara zote, mashirika ya kiserikali, taasisi za kifedha, sekta ya afya, elimu, madini, usafirishaji, utalii na mashirika yasiyo ya kiserikali.

“Kupitia teknolojia yetu ya fiber optic, tumeweza kuwahudumia mashirika haya kwa kasi ya kuaminika, jambo ambalo linaongeza tija na usalama katika utendaji wao wa kila siku,” ameongeza Maeda.

Amefafanua kuwa matumizi ya huduma za TTCL yamechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uendeshaji, kuongeza ufanisi, na kuimarisha usalama wa taarifa katika taasisi nyingi nchini, huku akisisitiza kuwa huduma hizo zinapatikana ndani ya nchi na kwa kuzingatia viwango vya juu vya usalama wa kimtandao.

 Maeda Maeda ametumia nafasi hiyo kuwaalika wananchi, wadau wa biashara, taasisi, mashirika, kampuni na wageni kutoka mataifa mbalimbali kutembelea banda la TTCL kujionea huduma za kisasa za mawasiliano na teknolojia ya kidigitali.

“Tunawakaribisha kuona huduma bora za Data Center, kujifunza namna bora ya kuhifadhi taarifa kwa usalama, kutumia huduma za mawasiliano ya uhakika, na kujifunza njia za kupunguza gharama za uendeshaji kupitia TEHAMA,” amesema.

Ameongeza kuwa katika msimu huu wa Sabasaba, TTCL imetoa punguzo maalum kwa vifaa vya mawasiliano ikiwemo Router, USB Modem, na MIFI, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia miongoni mwa Watanzania na kuwawezesha kufurahia ulimwengu wa kidigitali kwa gharama nafuu.

Kwa ujumla, ushiriki wa TTCL katika maonesho ya Sabasaba mwaka huu inadhihirisha dhamira ya shirika hilo kuendelea kuwa mshirika wa kweli wa maendeleo ya TEHAMA nchini, na kuhakikisha Watanzania wote wananufaika na huduma bora, salama na za kuaminika za mawasiliano.

Xxxxxx



Share:

TRA yaendelea kutoa Elimu ya Kodi kwa Umma katika Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa



Published from Blogger Prime Android App


Na Mwandishi wetu

MKURUGENZI  wa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Richard Kayombo, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika banda la TRA kwenye Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ili waweze kupata elimu muhimu kuhusu masuala mbalimbali ya kikodi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo,  Kayombo amesema kuwa ushiriki wa TRA kwenye maonyesho hayo ni sehemu ya jitihada za kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu haki na wajibu wao wa kikodi.

“Tunawahamasisha wananchi wote kufika katika banda letu ili wapate uelewa wa kina kuhusu masuala ya kodi, ikiwa ni pamoja na mabadiliko mapya ya kisheria na taratibu zilizopo,” amesema  Kayombo.

Amebainisha kuwa TRA inatoa elimu kuhusu masuala yote ya kikodi ikiwemo namna ya kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), fursa za vivutio vya kodi katika sekta mbalimbali kama kilimo, na huduma nyingine zinazotolewa na Chuo cha Kodi (ITA).

Aidha, alisisitiza kuwa wananchi wanaotembelea banda hilo wanaelimishwa pia kuhusu mbinu za kutambua bidhaa bandia, kwa usaidizi wa wataalam waliopo kwenye eneo hilo.

 “Tunatoa pia elimu kuhusu namna ya kutoa taarifa dhidi ya watumishi wa TRA wanaojihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili ili hatua za kinidhamu na kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao,” ameongeza Kayombo.

TRA imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwa karibu na wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa ulipaji sahihi wa kodi kwa maendeleo ya taifa. 

Amesema banda lao lipo wazi kwa wadau wote wanaohitaji msaada au elimu ya kikodi wakati wote wa kipindi cha maonyesho hayo.



Share:

SELF yaja na fursa mpya ya mikopo maonyesho ya Sabasaba



Published from Blogger Prime Android App




Na Joyce Kasiki ,Dar Es Salaam 



MENEJA  Masoko na Muhamasishaji Mkuu wa Mfuko wa mikopo wa SELF Linda Mshana  amewaasa watanzania wachangamkia fursa za mikopo hasa ya Nishati mbadala inatolewa na mfuko huo.umetua rasmi kuwatangazia Watanzania habari njema kuhusu fursa mpya zilizopo katika banda lao.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la mfuko huo lililopo kwenye banda kubwa la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 49 yanayoendelea jijini Dar Es Salaam,Linda amesema SELF wamekuja na huduma na bidhaa mpya zinazolenga kumkomboa Mtanzania wa kawaida na kumuwezesha kiuchumi kupitia mikopo nafuu, elimu ya fedha, na bima kwa ajili ya biashara na maisha.


"Katika maonesho haya, SELF tumekuja na mikopo mipya ya 2025  inayolenga kuchochea maendeleo endelevu na kuwaunganisha Watanzania wote kwenye masuala ya kifedha ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla"amesema Mshana


Amesema mikopo mipya inayotolewa na SELF ni pamoja na mkopo ya Nishati Mbadala kwa wajasiriamali wanaojihusisha na uuzaji wa bidhaa za sola, gesi, na teknolojia mbadala ya kuni na mkaa ambapo amesema,mfuko huo  utapunguza  riba kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo, ili kuhakikisha biashara zao zinakua na mazingira yanatunzwa kwa kizazi kijacho.


"Tumekuja Sabasaba kuwahamasisha Watanzania wachangamkie fursa hizi mpya,kama unafanya biashara ya sola, gesi, au bidhaa mbadala ya kuni na mkaa hii ni fursa yako,SELF tuko tayari kushika mkono wako na kukuinua kiuchumi,” amesema Linda


Vile vile.amesema ipo mikopo ya Vikundi  kwa watu walioungana na kusajili kikundi chao rasmi, SELF wanatoa mikopo kwa ajili ya shughuli za pamoja za uzalishaji mali huku akisema ni nafasi ya kipekee kwa watu wasio na duka au sehemu rasmi ya biashara, lakini wenye nia ya pamoja ya kujiendeleza.


Pia amezungumzia mikopo ya Kuboresha Makazi ya Wafanyakazi ambapo amesema,kwa wafanyakazi wanaotaka kuishi maisha bora zaidi, SELF wanatoa mkopo wa kuboresha makazi yao .


Pia amesema ipo mikopo ya Biashara na Ujasiriamali  kwa wafanyabiashara ambapo  SELF wanatoa mikopo rafiki kwa ajili ya kukuza mitaji, kuongeza uzalishaji, na kufanikisha ndoto za kimaendeleo.


Katika hatua nyingine amesema pia katika maonyesho hayo wanatoa elimu ya fedha na Biashara pamoja na elimu ya bima.


"Kwa wale wanaohitaji msaada wa kitaalamu kuhusu kuandaa bajeti, kusimamia biashara, au kupanga malengo ya kifedha, SELF wametenga sehemu maalum ya ushauri na elimu ndani ya banda lao. Huduma hizi zitatolewa bure kwa wote watakaotembelea,


"SELF pia wanajali ustawi wa biashara na maisha ya Watanzania. Kupitia bima mbalimbali tunazozitoa, tunahakikisha kwamba mali, afya na biashara za wananchi zinalindwa dhidi ya majanga yasiyotegemewa."amesema na kuongeza kuwa


Maonesho haya yanatoa nafasi ya kipekee kwa kila Mtanzania kufika, kujifunza na kuchukua hatua. SELF wanawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kujionea mikopo na huduma mbalimbali zilizobuniwa kwa ajili ya maendeleo ya watu wote  hata wale waliokuwa wametengwa na mifumo ya kifedha ya awali.
Share:

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Labels

Recent Posts

Unordered List

  • Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  • Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  • Vestibulum auctor dapibus neque.

Pages

Theme Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.